TANESCO Shy fanyeni mgao wa umeme kwa haki

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,298
3,973
Tunasikitika kwa hali ya mgao wa umeme na tunasema ipo siku kama mtawala alifanya hila kukomoa maskini,ipo siku kila mtu atavuna alichopanda.

Hata hivyo ninyi TANESCO shinyanga mnawezaje kukata umeme masaa 12 mtaa mmoja na kesho yake mnakata tena wakati mitaa mingine haipati mgao mkali namna hii?

Kwa vile mgao upo, kwa nini msifanye kwa haki kila mmoja apate machungu ya mgao huu?
 
hakuna mgao ni matengenezo watanzania hivi vitu viwili bado vinawapiga chenga
Matengenezo zaidi ya miez 4? Maana hili tatizo sugu la kukatikakatika hovyo kwa umeme ni la muda mrefu ila hii miezi mi 4 limekua sugu na siku zinavyozidi kwenda linazidi kuwa sugu zaidi ya jana
 
Matengenezo zaidi ya miez 4? Maana hili tatizo sugu la kukatikakatika hovyo kwa umeme ni la muda mrefu ila hii miezi mi 4 limekua sugu na siku zinavyozidi kwenda linazidi kuwa sugu zaidi ya jana
matengenezo hayana muda sahihi ni jambo la mara kwa mara ili kuboresha huduma, huwenda eneo hilo ni korofi mkuu
 
matengenezo hayana muda sahihi ni jambo la mara kwa mara ili kuboresha huduma, huwenda eneo hilo ni korofi mkuu
Toka wewe wakati mwingine kaa kimya ungejua hawa tanesco wameniludisha kwenye dimbwi la umasikini kiasi gan hapa kahama daa nimetelekeza duara langu huko mwime kisa umeme sa hv nafanya vibarua tuu roho inaniuma vibaya sanaa
 
Back
Top Bottom