TANESCO: Rationing is back!

Nadhani vitu ambavyo vimeanziwa na Herufi "T" vina laana/matatizo maana kadri siku zinavyokwenda majina ya T yamekuwa kero.Mfano TIGO na TANESCO bila kumsahau baba mwenye nyumba wao TANZANIA.Tuungane kuiondoa herufi T kwenye ALPHABET
 
Kama kweli Mkataba wa William Mhando unasema kwamba atapatiwa umeme wa GENERATOR na sio kutoka kwenye GRID ya TAIFA. Basi nchi hii tuna matatizo makubwa and solution of power rationing in this country is a far fetched idea!

Usemi wa CHARITY BEGINS AT HOME has no any meaning to Tanzanians! No wonder waziri wa ELIMU anapeleka mtoto wake OPRIVATE school, Waziri wa viwanda biashara na masoko, fenicha katika ofisa yake zote ni za kutoka Germany, Waziri wa Kilimo hajawahi kunywa/kununua chai, kahawa, sukari ya Tanzania. the list goes on
 
Tanesco itangaze muflisi ufungwe halafu tujipange upya.

Nchi ina gas kibao lakini mitambo ya kuzalisha umeme mingi inatumia mafuta.

Nilitegemea mitambo ya kuzalisha umeme nchi nzima ingefungwa huko huko Songo songo.
 
Nadhani vitu ambavyo vimeanziwa na Herufi "T" vina matatizo maana kadri siku zinavyokwenda majina ya T yamekuwa kero.Mfano TIGO na TANESCO bila kumsahau baba mwenye nyumba wao TANZANIA.Tuungane kuiondoa herufi T kwenye ALPHABET
 
Generator halitoki hapo mtaniambia, ni siasa tu hapo zinachezwa! Kama kawaida solution ya matatizo mengi ya nchi yetu tunadhani tutayamaliza kwa kuendekeza siasa kila sehemu.
 

well said mkuu kimbunga unajua key issue hapa ni moja HAWA JAMAA HAWA THE SO CALLED MAFISADI WAKALAMU kwenye energy sector huku wameona kuna loophole tena kwenye PROCUREMENT ya mitambo na vitendea kazi vya nishati ya umeme .... NISHATI YA UMEME NI DILI KUBWA SANA NA KWA KUTAMBUA HILO WENZETU WAMEONA MWANYA HAPO WANAKULA TU BILA HURUMA ... WANAJUA TENA WANAJUA YA KWAMBA EMERGENCY BACK UP POWER - HIYO DHARURA DHARURA HIYO SIO SULUHU NA KIUHALISIA UWEZI KUENDESHA UCHUMI KWA DHARURA UMEME NI MOYO WA UCHUMI HALAFU KILA SIKU UMEME NI DHARURA KWELI... ISSUE KUBWA HAPA NI KWAMBA WANAJUA WANAPATA SANA PESA KWA HIZI DHARURA .....NDIO MAANA PROJECT KUBWA ZA UMEME ZIMEBAKI MAKARATASINI TU ....
SULUHISHO LA KUDUMU SIO KUISAKAMA TANESCO MARA SIJUI ALETWE COMPETITOR MARA MANAGEMENT MBOVU
SULULU NI KUWA NA VIPAUMBELE TUKUBALI KWA UMEME NI MOYO WA UCHUMI TUWEKEZE KWENYE MIRADI MIKUBWA YA UMEME ... WAKATI MWINGINE TUACHANE NA POROJO NA KUDANGANYA WATU HAPA
 

Katika hili ninaipongeza kamati ya POAC, kwani viongozi wengi wa serikali na mashirika ya umma wamejisahau sana kiasi kwamba matatizo ya wananchi hayawahusu. Nadhani huu uwe ni mwanzo tu na kamati nyengine nazo ziige mfano huu kwa wale wote wasiowajibika ipasavyo.

Katika muktadha huo huo nadhani POAC wasishie kwa mkurugenzi mkuu pekee, bali waende mbele zaidi na kwa wakurugenzi wengine kama wa Thermo Generation, Hydro generation, CFO, Human Resources, Transmission e.t.c


Kama wangekuwa makini katika kutenda kazi zao wangetambua kwamba hizo transformer za city centre zimeshachoka na kununua nyengine mapema kwa ajili ya kufanya replacement. Kusubiri hadi zimeshindwa kufanya kazi na sasa imepelekea wananchi kuingia gizani ni dalili za uzembe na kutokuwajibika, na kimsingi kama ingewezekana wao(Tanesco) walitakiwa kuingizwa kwenye mgao hadi transformer zitakapokuwa zimefungwa na mgao umekwisha.
 
tukiacha siasa tukija kwenye sheria, kamati ya bunge inavunja sheria. Kama umeme wa jenereta ni sehemu ya stahili kwenye mkataba wa ajira baina ya Tanesco na bwana Mhando, kuondoa kwa namna yoyote isiyo na makubaliano baina ya pande mbili katika mkataba huo (Tanesco vs Mhando) ni uvunjifu wa mkataba kisheria. Mhando kama mwajiriwa yoyote katika nchi hii anayo haki. Sehemu ya haki hiyo imo ndani ya mkataba wake wa ajira na sehemu nyingine ipo katika sheria ya ajira na mahusiano kazini (sheria na 6/2004), na sehemu nyingine ipo ktk sheria ya mikataba (2002, sura ya 345) vitu vyote hivyo vitatu vinalinda haki zake kisheria. Tunaposhabikia haki zake kuvunjwa, tunashabikia haki za mwajiriwa awaye yeyote yule kuvunjwa. Mboma naye ni mbumbumbu wa sheria. Anashindwa kujua kua hata kamati ya bunge haipo juu ya sheria. Unatakiwa utii only lawful order. Ndiyo maana hata sheria ya ajira na mahusiano kazini na. 6/2004 inahesabu kuwa ni usitishaji wa ajira usio wa haki endapo mwajiri atamfukuza kazi mwajiriwa aliyekaidi amri isiyo halali. Amri ya POAC si halali kisheria.
Ushauri wangu: POAC na serikali kwa ujumla vitatue tatizo la umeme kisayansi zaidi badala ya kisiasa kwa kudhulumu haki ya kisheria ya mwajiriwa mmoja. Mhando amesema tatizo la umeme lipo wapi. Mkimwondolea jenereta miundombinu itaacha kuwa chakavu ghafla na kuwa mipya? Hayo madeni yatajilipa kwa kuwa tu Mkurugenzi naye analala kizani? Let us think out of box.
 

Hilo la kuondoa Jenereta amesema tu, amemuagiza nani akatoe,Mhando hawezi kulitoa, sio fundi (ni CEO). Ana mechanism gani ya kuhakikisha kuwa linatolewa.
 
Hivi ile trilion na kitu ilitolewa bungeni ili wabunge wapitishe bajeti ya wizara ikisemekana ni ya kufanya hali ya umeme iwe ya uhakika imeenda wapi vile
 
Hii ni hatari kwelikweli! nchi inachezewa kama kichwa cha mwendawazimu.
Hivi kweli nchi hii kuna kiongozi anayeweza kutoa maamuzi kwa maslahi ya taifa?
Huyo jk akili yake ilishagota ukingoni siku nyingi, anasubiri tu miaka yake mitatu iishe, alishawahakikishia watanzania mwaka gani ule, kwamba kufikia desemba yake tatizo la umeme litakuwa ni historia, akiulizwa leo hatua ipi ilichukuliwa atajibu nini?
 

Mkuu umenena sasa tuchukulie agizo lao limetekelezwa je ndio shida ya umeme imeisha?
 


Hii kitu haiwezi kwisha ikiwa watu wanaofaidika na utengenezwaji wa huu umeme wa dharura ndiyo hao hao wenye nguvu na ushawishi katika maamuzi ya hii sekta ya nishati hapa Tanzania.

umeme wa dharura unawapa watu hela katika kusupply mafuta, hizi generators na kwa sababu bei ya umeme ni kitu kigumu kuwa determined jamaa wanapanga tu bei zao na tanesco haina jinsi inabidi ilipe. Wahusika wote kuanzia hawa wawekezaji IPTL, Songas, Symbion na wanasiasa wahandamizi katika sekta na nje ya sekta wananufaika na hii migao yaI umeme isiyokwisha.

Hamna kitu katika taifa hili kinachoonyesha wazi wazi ubinafsi uliokithiri wa hawa viongozi wetu zaidi ya hili la umeme.
 
Mchungaji Zachary Kakobe alishamuonja Ngeleja kuwa nchi haitaweza ondokana na tatizo la mgao wa umeme mpaka Ngeleja aende akatubu na kuomba msamaha kwa Mchumnaji Kakobe.
Ngeleja alionyesha jeuri na dharau kubwa kwa Kakobe wakati ule wa swala la upitishaji wa nguzo kubwa za umeme pale Mwenge karibu na Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship.
Ngeleja alidhani ni utani, sasa nchi inapata taabu ya umeme kwa sababu yake.
 

To be fair, waziri tunamlaumu sana lakini haya ni matatizo yaliyotengenezwa miaka 50 iliyopita. Huwezi kupata short term solutions kutoka kwa Ngeleja utake usitake. Tumlaumu kama hapo alipo hana longterm plan ya kutatua tatizo hili! Jiulize ni kwa nini reli ya kati haitengenzwi (kwa ajili ya usafirishaji wa mafuta), kwa nini hatutengenezi mabwawa mapya. Utakuta kuna matatizo makubwa zaidi kwenye hii sekta
 

Duh.. Kwa hiyo Mkuu unataka kutuambia shida yote hii ya umeme itaisha pindi Ngeleja akienda kuomba radhi kwa Kakobe..? Wewe mwenyewe unaamini hivyo au unataka kutuaminisha sie tu humu jamvini..?
 
dili za majenereta zikiisha everything wil be history. Tatizo la umeme haliwezi kuisha kamwe kwa style hii. Mi naona Tanesco wanazimazima umeme tena city centre ili watu wapige kelele kama hivi then agreko walipwe ili watu wachukue chao. ni uhuni tu hakuna chochote. Tanzania hii ni aibu kuu. Na anaemtetea Mhando ni mbavu tu. hivi akichukuliwa machinga muuza viatu bar akaambiwa aagize mita za luku toka september mpaka leo march angekuwa bado hajazileta tu? huu ni u**nge kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…