TANESCO: Rationing is back!

TANESCO: Rationing is back!

Duh.. Kwa hiyo Mkuu unataka kutuambia shida yote hii ya umeme itaisha pindi Ngeleja akienda kuomba radhi kwa Kakobe..? Wewe mwenyewe unaamini hivyo au unataka kutuaminisha sie tu humu jamvini..?

Usiwe na shaka yoyote kuhusu hili.
Wewe jiulize, kwa nini nchi inaingia kwenye mgao wa umeme wakati mitambo yote ya uzalishaji umeme iko poa kabisa.
Tena huo huo mradi wa umeme uliopitisha nguzo kubwa za umeme pale kanisani kwa Kakobe haujazinduliwa mpaka leo (miaka miwili sasa).
Mchungaji Kakobe alisema wazi kabisa "nchi haitaweza kuondokana na tatizo la mgao wa umeme mpaka waziri Ngeleja aende akatubu na kuomba msamaha mwake (Kakobe)".

Hebu check link hii: Ngeleja ukitubu kwa Kakobe tu, umeme huo! Utaenda? - wavuti.com*
 
[h=1]POAC yaamua kuondoa genereta nyumbani kwa Mkurugezi Mtendaji wa TANESCO[/h]
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco),
William Mhando,
Midraji Ibrahim
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, amesema ingawa suala la kupatiwa umeme lipo kwenye stahili za mkataba wake, hawezi kubishana na uamuzi wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wa kuondoa jenereta nyumbani kwake.
Akizungumza kufuatia agizo la POAC kuondoa jenereta hiyo nyumbani kwake jana, ili aonje uchungu wa kukatika kwa umeme, Mhando alisema alishtushwa na hatua hiyo kwa sababu ni suala la mkataba, lakini hawezi kubishana na kamati.
“Mkataba ninao jana (juzi) nilishtuka kuhusu agizo hilo kwa sababu niliajiriwa na bodi na mwenyekiti wangu alikuwapo tutakaa tuangalie, lakini siwezi kupingana na maagizo ya kamati,” alisema Mhando.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa wa Bodi ya Tanesco, Jenerali mstaafu Robert Mboma, alisema watatii agizo la POAC la kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani kwa mkurugenzi huyo.
“Tumeagizwa na kamati tutaangalia jinsi ya kulitekeleza agizo hilo la kuondoa jenereta, tupeni siku tatu au nne hivi mtaona,” alisema Jenerali Mboma.
Alipoulizwa kama kuondoa jenereta hiyo haitakuwa kinyume na mkataba wa ajira unaoonyesha stahili za mkurugenzi huyo, Mboma alisema: “ Unadhani tutafanya nini kama tumeagizwa tuiondoe, hatuna jinsi hata kama kuna mkataba sisi tutatekeleza tuliyoagizwa.”
Mhando alisema suala la kukatika kwa umeme unaondelea hivi sasa, halisababishwi na menejimenti bali inatokana na kutokuwapo kwa uwekezaji muda mrefu kwenye shirika hilo, baada ya kuwekwa chini ya Shirika la Kubinafsisha na Kuuza Mashirika ya Umma (PSRC).
“Tangu mwaka 1999 hadi 2007 hakuna uwekezaji uliofanywa kwa Tanesco baada ya shirika kuwekwa chini ya PSRC, kwa hiyo kukatika kwa umeme kunaokoonekana hivi sasa ni matokeo ya ubinafsishaji uliolengwa,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kukatika kwa umeme kunatokana na uchakavu wa miundombinu, lakini siyo kuzidiwa na kwenye uzalishaji kwa sababu hivi sasa wanazalisha Megawati 782.51 ilhali mahitaji ni Megawati 772.15.
“Mfano pale City Center (katikati ya jiji), tulikuwa na transfoma mbili zote zimetumika zaidi ya miaka 30, Februari mwaka huu zimeharibika, tumeagiza kutoka Uturuki na sasa zimefika Dubai, tatizo ni miundombinu imechakaa,” alisema.
Kuhusu Aggreko na Symbion Dodoma kuzima mitambo yao, Mhando alikiri kuwa hatua hiyo inatokana na deni ambalo linafikia Sh62 bilioni na kwamba, IPTL imepunguza uzalishaji kutoka Megawati 100 hadi 50. Aggreko inadai Sh58 bilioni na Symbion Dodoma Sh4 bilioni.
“Mgawo kwa maana ya uwezo wa kuzalisha hatuna, ila hii kukatikakatika kwa sababu ya transfoma hiyo ipo. Tupo kwenye hatua mbalimbali za kukarabati miundombinu hiyo na baada ya kipindi tatizo hilo litatoweka,” alisema.
Mhando alisema hivi sasa wamepata dola 85 milioni za Marekani kwa ajili ya Dar es Salaam, Euro 25 milioni kutoka Finland na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) imetoa dola 40 milioni za Marekani.
Juzi, Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe, alisema lazima jenereta lililoweka nyumbani kwa mkurugenzi huyo liondolewe kwa sababu linatumia mafuta ya Serikali.
 
Wamkataze hata kununua kibatari ajue watu tunavyotaabika.
 
iyo ni sawa maana kama mgao wa umeme usiwe na ubaguzi, huyo bwana akitaka umeme anunue jenereta kwa pesa yake na mafuta atoe pesa yake mfukoni.
Nyama ikioza na harufu mbaya kutanda kwake atajua jinsi walalahoi tunavyoteseka, lakini pia wafanyakazi wa shirika walipe bili za umeme maisha yataenda sawa.
Tunapolia na hali kuna wenzetu hawajui hilo, pongezi kamati makini ya POAC.
 
28 MARCH 2012






*Makamba adai TANESCO inadaiwa mil. 269/-
*Asema hali itakuwa 'tete' zaidi kuanzia Agosti

Na Grace Ndossa

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), linadaiwa sh. bilioni 269 na Kampuni ya Kufua Umeme ya Aggreko ikiwa ndio sababu ya shirika hilo, kushindwa kutoa huduma ya umeme kwa ufanisi.

Kutokana na deni hilo, Kampuni ya Aggreko imelazimika kuzima mitambo yake baada ya kukosa fedha za kununulia mafuta yanayotumika kuendeshea mitambo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Bw. January Makamba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Bw. Makamba alisema, Serikali iliombwa kuikopesha TANESCO sh. bilioni 408, lakini fedha hizo hadi sasa hazijatolewa ili kusaidia kulipa deni hilo.

"Hata kama TANESCO watapewa hizi fedha, kwanza tunapaswa kulipa deni la sh. bilioni 269 na kiasi ambacho kitabaki hakitoshelezi kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hii," alisema.

Alisema Kampuni ya Aggreko ilizima mitambo yake tangu Desemba 2011 kwa sababu ya kukosa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo.

"Kimsingi tatizo la mgawo wa umeme litarrudi kama zamani kutokana na vyanzo vya maji ambavyo vinatumika kuzalisha umeme kupungua, kwa sasa umeme tunaopata unatokana na vyanzo hivi.

"Maji yaliyopo kwenye mabwawa ni kidogo, ikifika Agosti mwaka huu itakuwa kipindi cha kiangazi sasa hali itakuwa mbaya zaidi, njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kuharakisha ujenzi wa bomba la gesi ambalo Rais Jakaya Kikwete alitoa tamko lijengwe kwa miezi 18 tangu 2011," alisema Bw. Makamba.

Alisema kukamilika kwa bomba hilo, kutaondoa mgawo kwani umeme wa uhakika utakuwa ukipatikana muda wote.

"Kama tutaendelea kuzalisha umeme kwa kutegemea mafuta, nchi yetu itaelekea kubaya kwani gharama za mafuta zinaongezeka siku hadi siku," alisema.

Kuhusu utaratibu mpya wa kuagiza mafuta kwa pamoja ambao umeanzishwa hivi karibuni kwa Sheria ya Bunge, Bw. Makamba alisema haujasaidia kupunguza bei ya nishati kama ilivyotarajiwa.

Akizungumza na wadau wa mafuta, Bw. Makamba alisema hivi sasa kamati yake itakaa na kupitia upya kanuni na sheria ili kuangalia njia mbadala za kupunguza bei ya nishati hiyo kama ilivyokusudiwa.

Alisema kati ya kampuni zilizokubaliwa kununua mafuta kwa pamoja, hadi sasa zabuni mbili zimeagizwa na mara ya kwanza ilikuwa Januari na Februari.

Aliongeza kuwa, kipindi hicho ziliingia meli 16 zenye shehena ya mafuta ambapo awamu ya pili ilikuwa iwe Machi na Aprili mwaka huu kwa kuingia meli 17 lakini hadi sasa zimeingia meli mbili tu.

Bw. Makamba alisema meli zimekuwa zikichelewa tofauti na walivyokubaliana kuwa zitaingia zote ambapo changamoto iliyopo ni bei ambayo haijashuka.

Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa Masoko kutoka Shirika la Maedeleo ya Petroli nchini (TPDC), Bw. Leo Lyayuke, alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto nne.

Changamoto hizo ni kampuni za kuagiza mafuta, upatikanaji wa zabuni, ongezeko la bei na uchelewaji wa meli.

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Godwin Samuel, alisema imebainika baadhi ya mafuta yanayoingizwa nchini hasa petroli hayana ubora wa kutosha.

Alisema kutokana na hali hiyo, hivi sasa wanachukua sampuli ya mafuta yanayobaki bandarini na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini yana matatizo gani
 
laana ya kuingia madarakani kwa hila na ufisadi itautafuna sana utawala huu dhalimu
 
Na Grace Ndossa

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), linadaiwa sh. bilioni 269 na Kampuni ya Kufua Umeme ya Aggreko ikiwa ndio sababu ya shirika hilo, kushindwa kutoa huduma ya umeme kwa ufanisi.
Kweli nashindwa kuelewa. Kwa nini serikali isinunue mitambo yake kwa mabilioni haya imeng'ang'ania kukodi tu?
 
Du hatareee ngoja tusibirie hyo agosti,mkuu edit hapo juu kwamba ni bil269.
 
Sasa kama ata JK anasema yeye sio mungu kuleta mvua unatarajia nini?
Yaani angekuwa ameajiliwa na kampuni ya kizungu JK kwa majibu hayo hana kazi.
Tatizo la umeme Tz ni ulaji wa watu fulani ebu imagine ela zinazoongelewa apo ni Billions tuu kwa kwenda mbele.
Naona ndo wanafanya primitive accumulation ya mataji wa 2015
 
Kweli nashindwa kuelewa. Kwa nini serikali isinunue mitambo yake kwa mabilioni haya imeng'ang'ania kukodi tu?


Mkuu watu wanatoana mamcho kugombea uongozi ili wasimamie hiyo mikataba,
Hivi nani wa kwenye serikali mwenye uwezo wa kuamua kuwa serikali inunue mitambo yake? Tanzania ni zaidi ya uijuavyo
 
kazi ipo... kila siku tunaambia megawati megawati.... zimeongezwa.. mtu 1 anadanganya watu m 45 na bado yupo tu anakula gudtm wengine ndio hao wakobize na machanguduo-moro looh kazi ipo.. hii nchi ukiwaza sana unaweza kufa hata kabla ya siku zako kwa hasira.. haya tujiandaa kufunga vimigahawa, salooon , na tujiandae na mafuta kupanda bei... hii ndio mbongo bwana wakubwa tayari wameshajipanga kutengeneza super profit na 10 % kwa kuleta jenereta feki.. Mungu tusaidii

Aaaaaaa!! sasa nimefahamu maana ya mega wati yaani mega=bandua pande kubwa, wati= nini unataka kumega( mega pesa= mega wati)
 
Mpaka 2015 wtz tutakuwa tumenyooka,

Mimi naona wacha tu hii iendelee ili tushike adabu, tulichagua wenyewe magamba, misikitini walisema tuchague mwislam mwenzetu na awamu yake ya kwanza maaskofu kama 2 hivi nao walisema huyu ni chaguo la Mungu, kwakua huu mgao unakwenda hadi misikitini na makanisani, twende tu hivyo hivyo may be siku moja na mahubiri/mawaidha yatabadirika huko kwenye nyumba za ibada.
 
Back
Top Bottom