Hata tukibadilisha uongozi wote pale bado hali itakuwa hivi hivi kama tusipobadilisha mbinu za kibiashara za shirika hili na kuondoa siasa kwenye utendaji wake.
Kwa hali ilivyo pale Tanesco, siasa ni nyingi kuliko... Labda tutafute majibu ya maswali haya machache ili tujue hali halisi ilivyo. Hv ilikuwa ni viable kupeleka umeme mabwepande kwenye mahema? Kama jibu ni hapana ile distribution line imegharamiwa na nani au gharama zake zitarudi vp na kwa kipindi gani? The same apply kwa kawawa, kule madale enzi hizo.
Mbona Tanesco wanalazimishwa kujenga hizo line lakin serikali haiwalipi? Mbona taasisi za serikali na wizara zake hazilipi bili zao wakati budget ya matumizi hayo wanatengewa?
Wanatudanganya kwa ruzuku wanazolipatia shirika hili kumbe hata haifiki robo ya madeni yao.