Wenye mashamba ya miti ya kuzalisha nguzo za umeme msilalamike kuhusu TANESCO kuanza kutumia Nguzo za ZEGE . TANESCO ni Kampuni lazima ifanye biashara na ijiendeshe kiviwango vya kimataifa.Nguzo za Tz hazina viwango baada ya biashara hiyo kuingiliwa na matapeli.Umri wa kuvuna miti,madawa ya kudhibiti ubora wa nguzo nk vimekiukwa.Inakuwaje nguzo inaoza ndani ya mwaka mmoja?Tusijilaumu kama TANESCO hawazitaki tuuze nchi za nje .South Africa acha walete nguzo zao kwa sababu zina viwango kimataifa.