Jana tulikaribishwa nyumbani kwa rafiki yetu ili tuangalie fainali za kombe la dunia hiki mitaa ya tegeta basi wakati tukiangalia mtanange huo umeme ulikuwa unaongezeka mara unapungua mara tu baada ya mpira kwisha tulisikia bonge la mlio uliotufanya wote tuogope tulipoangalia juu tukakuta taa ya umeme ikiwaka moto hivyo tulifanya juhudi za kuizima na bahati moto tuliudhibiti