Kifaa cha kuzuia vifaa vya smart electronics kuungua na umeme

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Kabla ya kujua ubunifu wa leo unahusu nini;naomba nikuulize maswali yafuatayo.

JE? ulisha wahi kushuhudia:-

* Flat TV au TV ya kawaida wakati wa kuwasha au wakati unaangalia ghafla inaungua?

*Radio ambazo ni smart mfano Home Theatre ikiungua wakati unaitumia/ikiwa stand-by au wakati wa kuiwasha?

*Simu aina ya Smartphone zikiungua au kilipuka ghafla kama bomu wakati wa kuzi-charge kwa kutumia umeme?

*Computer Desk-top au (Laptop wakati wa kuicharge)zikiungua ghafla wakati zimepachikwa kwenye umeme?

*Baadhi ya taa za umeme katika nyumba yako hazimalizi hata siku mbili zinaungua hovyo?

*Unalipa bili ya umeme kubwa kuliko matumizi yako,japo umejaribu kufatilia wirering ya umeme ya nyumba yako na mambo mengine yote unaona yako sawa lakini bill ya umeme bado iko juu?

Uharibifu huu unasababishwa na mabadiliko ya tabia ya umeme yanayo tokea ndani ya sekunde kadhaa tu;lakini huacha uharibifu mkubwa kwa vifaa vya umeme.

Hali hii kitaalamu inaitwa Voltage surge(kama tatizo limetokana kutokana na voltage) au Current surge(kama tatizo limetokana na Current)

Japo wengi wanaitambua kwa umaarufu wa jina moja tu yaani VOLTAGE SURGE!

Zingatia

SURGE haiwezi kuzuiliwa na na stabilizer ya kawaida, ndio maana unaweza ukawa unatumia stabilizer lakini bado kifaa chako kikaungua, Vifaa vya kuzuia surge ni vifaa maalumu vilivyo tengenezwa kwa ajili ya kazi hiyo tu!

Vifaa vingi vinavyo ungua na surge mfano TV au computer, ukipeleka kwa fundi mara nyingi utaambiwa kuwa POWER SUPPLY ndiyo imeungua!

Lakini simu ikiungua kutokana na voltage surge mara nyingi huwa ni ya kutupa!

*Kwa kuorodhesha tu vyanzo vikubwa vinavyo sababisha kutokee Voltage Surge katika nyumba yako ni:-

1.Radi

2.Mashirika ya usambazaji wa umeme husababisha kutokea kwa voltage surge kwenye makazi ya watu kutokana na kuzima na kuwasha umeme mara kwa mara, pamoja na mifumo mibovu ya usafirishaji wa umeme kutoka katika transformer hadi kwa wateja kama vile loose connection n.k

3.Fridge au Freezer

4.Wirering Mbovu

5.Air Conditioners

6.Motor(za visima vya maji, kufungua mageti, na lift n.k)

7.Photocopy machines

Ni takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa toka nilipo leta mada yangu hapa jamvini yenye kichwa cha habari "VOLTAGE SURGE"ni hatari ambayo wegi wanaishi ndani yake.

Kifaa hiki kina-suppress vitu vikubwa viwili ambavyo ni hatari kwa vifaa vyetu majumbani ambavyo ni Voltage surge pamoja na Current surge, hivyo kifaa hiki sio voltage surge protector tena bali ni Voltage and Current Surge Protector(VCSP) .ambacho ni hiki hapa chini

Kabla sijaanza kuelezea kitaalamu jinsi kifaa hiki kilivyo tengenezwa,ningependa nisiwachoshe wale wasiopenda kusoma maelezo marefu kwa kueleza kwa kifupi tu kifaa hiki kinavyo fanya kazi.
-Kifaa hiki kina Circuit muhimu MBILI
1.Delay and control circuit

Hii ni saketi ambayo inasaidia kuchelewesha kifaa chako cha umeme ulicho kipachika kwenye VCSP, kupokea umeme pale unavyo washa switch au umeme unapo rudi baada ya kukatika.
Kifaa hiki huzuia umeme huo kwa sekunde kadhaa ili kusubili umeme huo utulie kabisa ndipo kifaa hiki kita uruhusu umeme kuingia kwenye kifaa chako iwe simu,TV n.k.

Hivyo kamakuna surge yeyote ilikua imeambatana wakati umeme unarudi au wakati unawasha switch surge hiyo haita pata nafasi ya kukidhuru kifaa chako.
Saketi hii ina indicators ambazo zianaonyesha delaying process wakati umeme umeingia kwenye VCSP kabla ya kuingia kwenye kifaa chako Saketi yenyewe hii hapa!

Saketi ya pili ndiyo saketi muhimu zaidi na ndiyo inayo beba jukumu kuu la kulinda vifaa vyako

2.Surge suppresser circuit

(a)Kazi ya Varistor(Metal oxide varistor (MOV) katika saketi hii

MOVs kazi yake ni kuondoa kiwango cha umeme ambacho kinazidi kiwango cha kawaida katika mfumo wa umeme.

Kama ikitokea umeme ukazidi kiwango cha kawaida MOVs huanza kutengeneza ukinzani ambao utaondoa excess voltage katika line ya umeme.

Kwakuwa Voltage surge ni kitendo cha kuongezeka kwa kiwango cha umeme

ghafla kunako sababishwa na kitu kama vile radi au loose connection na ambacho hutokea kwa sekunde kadhaa tu,MOVS kazi yake ni kuondoa ongezeko hilo la umeme kwenye line ili isifike kwenye kifaa chako na kuleta madhara.

(b)Kazi ya Themistor katika saketi hii

Thermistor;ni kifaa maalumu ambacho kazi yake ni kuzuia inrush currents mara tu umeme unavyo rudi au switch inapo washwa.

Tambua kuwa kila kifaa cha umeme kina mahitaji yake ya kiwango cha current,hivyo kuruhusu kiwango chote cha current kuingia katika kifaa husika mara nyingine huleta madhara ya kifaa hicho kuungua;ndio maana vifaa vingi vya umeme huungua wakati wa kuwashwa;hii inasababishwa na inrush currents.

Kuondoa tatizo hilo thermistor hutumika ambapo umeme huanza kuingia katika thermister ndipo huingia katika kifaa cha umeme.

Baadaya ya umeme kuwaka thermister huwa na ukinzani mkubwa sana hivyo kuzuia kiwango cha current kisiingie moja kwa moja katika kifaa chako,baada ya hapo kwa kuwa kifaa husika kitakua kinahitaji kiwango fulani cha current ili kifanye kazi,kitavuta kiasi cha current ambacho chenyewe kinahitaji;kwa kuwa thermistor imezuia current hizo kuvutwa kwa current na kifaa chako cha

umeme kutasababisha thermistor ipate moto;thermistor ikipata moto ukinzani wake hupungua hivyo kuruhusu kile kiwango tu cha current ambacho kimehitajika na kifaa ulicho kipachika wakati huo!

Hivyo kwa kutumia thermister kifaa kitapewa current kutokana na mahitaji yake bila kuzidishiwa!

Hivyo tatizo la current surge linakuwa limeondoka!

(c) Kazi ya Ceramic Capacitor Y Capacitors-DIP katika saketi hii

Hii ni capacitor maalumu kwa ajili ya kuondoa Cheche zinazo tokea kwenye line ambazo zinaweza kupelekea surge(spaks killer)

Tambua kuwa unapowasha switch kuna cheche ambazo hutokea kutokana na kuungana kwa terminal mbili,au wakati mwingine kama line husika ina loose connection hupelekea kutokea kwa cheche,ambazo huweza kuleta surge;hivyo kuhakikisha tunaendelea kuwa salama dhidi ya surge tunalazimika kuondoa sparks za aina yeyote kwenye line yetu ndo mana Ceramic Y Capacitor-DIP ikatumika.

(d)Kazi ya Filter capacitor katika saketi hii
Kazi ya capacitors hizi kubwa mbili ni ku-smooth umeme unaoingia katika kifaa chako kuhakikisha hakuna mawimbi yasio hitajika yanajipenyeza katika kifaa chako cha umeme ambayo yanaweza kuleta madhara.

Pia kapacitor hizi zinasaidia kuhakikisha VCSP haizalishi mawimbi yatakayo ingiliana na mifumo mingine kama vile mawimbi ya radio,TV n.k

(e)Kazi ya Choke ferrite transformer katika saketi hii.
Kazi ya choke hii ni kuwa na sifa ya ku-Absorb excess voltage kwa kugeuza nguvu hiyo ya umeme iliyo zidi kuwa sumaku(electromagnetism).

Hivyo cke pia ni kifaa kingine muhimu katika kukabiliana na surge.

(f)Kazi ya Fuse katika saketi hii
Kwa kifaa ambacho kinatimia MOVs,ni lazima kifaa hicho kiwe na fuse,kutokana na ufanyaji kazi wa MOVs.

Kama Voltage surge itakuwa kubwa sana kuishina MOVs,kwa kawaida MOVs huzuia umeme kuingia kabisa katika saketi kwa kutengeneza short circuit ili fuse ikate.

Hivyo matumizi ya Fuse sehemu ambapo MOVs zimetumika hayakwepeki.

Hivyo ni vifaa vikubwa sita pamoja na mfumo wa delay ambavyo kila kimoja kila kinafanya kazi yake katika kuhakikisha umeme utakao kuwa unatoka katika output ya VCSP unakuwa Clean and safe kwa vifaa vyako vya umeme dhidi ya vyanzo vyote vya surge kama vile radi n.k

Saketi nzima ya kifaa hiki inaonekana hivi:-

Kwa upande wa nje features za kifaa hiki ni kama zinavyo enekana hapa chini;-

Tambua-Indicator nyekundu itakuwa ikiwaka kuonyesha umeme ni salama kwa matumizi na pia kuonyesha kuwa Thermistor na Varistor zinafanya kazi vizuri!

-Kwa usalama wa vifaa vyako nyumbani,nakushauri utumie kifaa hiki kuvirinda kwani hasara utakayo ipata baada ya simu yako au tv yako au home theater yako kuungua ni kubwa zaidi kuliko kununua kifaa hiki.

Vifaa ambavyo vipo kwenye hatari kubwa ya kuungua na voltage surge ni Flat TVs,Smart phones na Home theaters,kwani zinatumia soft technologies ambayo ipo vulnerable tu surge

Tuangalie youtube kifaa hiki kinavyo fanya kazi

Mkuu bei yake vp

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom