(Tahadhari baadhi ya picha zinaweza kukera)Ukweli kuhusu kunaswa na umeme na namna ya kujiokoa

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
MASHAMBULIO MAKUU YA UMEME DHIDI YA BINADAMU NA NAMNA YA KUMUHUDUMIA

Kabla ya kujua namna umeme uavyo mshambulia binadamu hadi mara nyingine kuweza kumuua,ni vizuri tukafahamu vitu vikuu vinavyo unda umeme.

Kwanza tutambue nini maana ya umeme.

Umeme ni mtiririko wa electrons ndani ya kipitisho.Electrons hizi zinaundwa na vitu vidogovidogo vinavyoitwa atoms, hii ndiyo nishati husika ambayo hutarajiwa kutengeneza nguvu flani ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali.

Kwa uchache vitu muhimu vinavyo unda umeme ni kama vifuatavyo.

Voltage-Hii ni nguvu ya msukumo wa electrons katika kipitisho,Msukumo huu ndiyo hubeba electrons kutoka sehemu moja hadi nyingine ya kipitisho cha umeme.

Current-Huu ni mtiririko wa electrons katika kipitisho,mtiririko huu ndiyo hutegemeana na nguvu ya msukumo wa voltage katika kipitisho,

Kipitisho-Hiki ni kitu ambacho electrons zinakua zikipita ndani yake,(njia ya umeme) Mfano Waya,Hewa ,Maji n.k


JINSI UMEME UNAVYO MSHAMBULIA BINADAMU.

Katika akili ya kawaida wengi hudhani kiasi kikubwa cha Voltage ndicho huweza kumuua bnadamu kirahisi zaidi.Mfano ni rahisi kuamini kuwa Volt 10000 inauwa kirahisi zaidi kuliko volt 100.Hapo ndipo utasikia wengine wakisema "umeme huu wa bongo mdogo bana hauuwi wala nini"

Lakini kitaalamu si kweli kwani ili binadamu apate shambulio la umeme lenye kumtoa uhai haitaji voltage nyingi,hivyo umakini ni muhimu pale unapokuwa unajihusisha na vifaa vya umeme au umeme wenyewe.

Mfano kifaa cha kuulia mmbu kina voltage nyingi sana kufikia 2400voltage mara kumi ya umeme wa majumbani lakini hakiwezi kumuua binadamu sababu current yake ni kidogo sana!

zapper.jpg

Kitaalamu binadamu anaweza akapoteza uhai kama tu kiasi cha mtiririko wa Electrons(Current) ni kikubwa hata kama Msukumo(Voltage) ni kidogo.


AINA YA MASHAMBULIO YA UMEME DHIDI YA BINADAMU

SHAMBULIO LA KWANZA: Shambulio la kuleta maumivu ya viungo na mshituko wa akili.


wrfa.jpg wrfa.jpg

Shambulio hili husababishwa na kiasi cha electrons kuanzia 0.01Ampere sawa na 10miliAmpere pale kinapo pita katika mwili wa binadamu.

Mtu ambaye atagusana na umeme ambapo kiasi cha electrons hicho hapo kikapita mwilini mwake basi,mtu huyu hujirusha pembeni kwa nguvu na hushituka sana,Kujirusha huku mara nyingi si kwasababu ya umeme kumrusha,mara nyingi binadamu hujirusha yeye mwenyewe kutokana na mifumo yake ya fahamu kumlazimisha kufanya hivyo ili kujitoa katika eneo ambalo linaonekana kuwa hatari kwake.

Mara nyingine shambulio la aina hii humfanya mtu akapoteza kumbukumbu kwa muda,Mfano mtu amaweza akawa ameshambuliwa na umeme sebuleni ,baada ya kushambuliwa akapoteza kumbukumbu,labda anaweza akatoka sehemu hiyo ya umeme hadi sehemu nyingine mfano chumba kingine,au nje ya nyumba.

Pale akili itakapo mrudia mtu huyu huhisi karushwa na umeme kutoka pale aliposhika umeme hadi pale alipo.Mfano mtu utamsikia amerushwa na umeme kutoka sebuleni hadi chumbani,sio kweli umeme haumrushi mtu ila kinachofanyika ni huyu katika harakati zake za kujiokoa mara nyingine hupoteza kumbukumbu kutokana na shambulio hilo,hivyo akili itakapo mrudia hujiona kama amefika hapo alipo kwa kuruka na sio kwa miguu yake mwenyewe.

Shambulio hili la kwanza halina madhara makubwa zaidi ya maumivu ya viungo na kuto kujisikia vizuri kutokana na mshituko.


NAMNA YA KUMUHUDUMIA MTU ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA KWANZA

1.Mhanga akae eneo ambalo lina hewa ya kutosha,hii itasaidia mfumo wake wa hewa kufanya kazi vizuri na kumbukumbu zake kurejea katika hali yake ya kawaida.

2.Mhanga ajikague au akaguliwe kama kaumia sehemu yoyote ya mwili wake wakati wa harakati za kujiokoa na kama kuna sehemu kaumia ahudumiwe kwa mujibu wa jeraha husika.

3.Aitwe mtaalamu wa umeme na kumwonyesha eneo au kifaa kilichosababisha shock ya umeme kwa mhanga,Ili aweze kuondoa tatizo.Usiendelee kuishi na kifaa au sehemu iliyoleta shock bila kuondoa tatizo kwani yaweza kuleta madhara makubwa zaidi badae.

SHAMBULIO LA PILI:Shambulio hili husababisha mwili kuungua,mifumo ya mapafu kushindwa kufanya kazi na mara nyingine kupoteza fahamu kabisa.

Shambulio hili husababishwa na kiasi cha mtiririko wa umeme(current) zaidi ya 200miliApere sawa na 0.2Ampere kupita katika mwili wa binadamu.

Katika shambulio hili binadamu ana naswa na umeme,kwa muda mrefu bila kujinasua.Hapa mtu huendelea kukaa katika mkondo wa umeme kwa zaidi ya sekunde tano hadi kumi,kitendo hiki husababisha ukinzani kati ya mwili wake na mtiririko wa electrons katika mwili wake ukinzani huu ndio husababisha kutokea kwa joto ambalo ndio huuchoma mwili wa mtu huyu.

M3350205-Electrical_burns-SPL.jpg iooo.jpg MTOTO NA TRANSFOMA 1.jpg

Tambua kuwa electrons zinapopita katika kipitisho chenye ukinzani husababisha kutokea kwa joto mfano kama vile pasi inavyo fanya kazi.Hivyo kwakua kiwango hicho cha current kitakua kinapita katika mwili wa binadamu na kutokana na ukinzani uliopo katika mwili wa mtu huyo joto hutengenezwa na hatimaye mwili huungua kabisa kama mtu aliyeungua na moto wa kawaida,kwani ngozi ya mwili huachana na nyama.

Kutokana na shambulio la namna hii mtu huyu mara nyingine hupoteza fahamu na kuanguka baada ya umeme kumwachia,na pia mara nyingi mapafu yake huwa hayafanyi kazi vizuri kutokana na maji mengi kukauka mwilini mwake hivyo upumuajia huwa wa shida sana.Mtu huyu huweza kupona kama atapewa huduma ya kwanza vizuri.

Kwanini mtu huyu huachiwa na umeme ingawa alikua hawezi kujinasua.Jibu ni kwamba mtu huyu hufikia hatua umeme ukamwacha licha ya kumnasa kwa sekunde kadhaa kwasababu tayari nanakua amesha poteza maji mengi mwilini hivyo mwili wake unaongezeka ukinzani zaidi,hivyo anakua sio kipitisho kizuri cha umeme tena hivyo umeme hushindwa kauendele kumshika na hatimaye mtu huyu ataanguka chini.

Kuachiwa kwa mtu huyu na umeme baada ya kunaswa kunategemeana pia na mkao wa aliye naswa,kama tu aliyenaswa anakua kalala juu ya waya,zenyewe inakua ngumu kwake kutoka katika eneo la hatari sababu anakua yupo juu ya waya zenyewe hivyo hata umeme ukipunguza uwezo wa kupita mwilini mwake bado atakua kalala juu ya hizo waya hivyo anaweza akaendelea kuungua na ahatimaye kufariki.japo umeme wa namna hii hauuwi moja kwa moja lakini kama kuna mazingira kama haya kifo kinaweza kutokea.

Udaku Special.Ajali.jpg umeme.jpg



NAMNA YA KUMUHUDUMIA MTU ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA PILI

1.Kama unashuhudia tukio haraka zima switch ambayo inapeleka umeme katika eneo ambalo mhanga amenasa,kama switch kuu ya kuzima umeme nyumba nzima ipo jirani jitahidi kuizima switch hiyo mapema.

2.Kama switch zote hujui ziko wapi hakikisha umevaa viatu vya soli ndefu na ujitahidi kumnasua mhanga kwa kutumia vifaa visivyo pitisha umeme,kama vileUbao mkavu,Plastic,au kitambaa kikubwa,au kwa kutumia mto wa kulalia au wa kukalia.Epeka kumgusa ,moja kwa moja mhanga ambae bado yupo kwenye mkondo wa umeme kwani na wewe unaweza kunasa pia.

what-can-i-do-In-case-of-an-electric-shock.jpg

3.Unaweza kumsukuma kwa kutumia vizuizi vya umeme katika namna ambayo ataanguka salama,Jitahidi kuyafanya haya katika akili ya utulivu na kwa haraka.

4.Baada ya mhanga kuondoka katika mkondo wa umeme jitahidi kuhakikisha eneo hilo linahewa ya kutosha kwa kufungua madirisha na milango.Kwakuwa wahanga wa shambulio hili huwa na tatizo la kupumua hakikisha unamsaidia kuhema kwa kumpulizia hewa mdomoni(kiss of life),Na pia kwa kumsaidia mapafu yake kufanya kazi vizuri kwa kumsukuma tarafibu eneo la kifua tazama picha.

NbMH2Ul.jpg hhhpp.jpg


Hakikisha unafanya hivyo hadi pale mhanga atakapo anza kupumua mwenyewe vizuri.Kisha piga simu kuomba msaada wa watu wengine na watu wa hospitali.

5.Mgonjwa wa shambulio hili huwa amepoteza maji mengi mwilini hivyo ni vizuri akawaishwa hospilali kwa msaada zaidi,pia wakati wa huduma ya kwanza mtu huyu aliye ungua afunikwe mashuka mengi mwilini.Ili kuepuka kupoteza maji mengi zaidi.

6.Aitwe mtaalamu wa umeme na kumwonyesha eneo au kifaa kilichosababisha shock ya umeme kwa mhanga,Ili aweze kuondoa tatizo.Usiendelee kuishi na kifaa au sehemu iliyoleta shock bila kuondoa tatizo kwani yaweza kuleta madhara makubwa zaidi badae.

PIGO LA TATU:pigo la umeme linalo pelekea kifo cha mtu moja kwa moja.

Kiwango cha cha mtiririko wa umeme kinacho sababisha kifo ni kidogo kuliko kile kinacha sababisha pigo la pili(mtu kuunguzwa na umeme).

Kiwango kinacho sababisha kifo kwa mtu aliyenaswa na umeme ni kati ya Ampere 0.1 hadi 0.2Ampere sawa na 100miliAmpere hadi 200miliAmpere.

stock-vector-illustration-representing-a-person-receiving-an-electric-discharge-in-a-high-voltag.jpg


Kiwango hiki cha umeme kinakua rahisi kumuua binadamu kwasababu kinasababisha mishipa ya fahamu kukaza.Hivyo kiwango cha umeme kama hiki kikipita katika mwili wa binadamu kitakacho tokea ni kwamba,mishipa ya fahamu ya binadamu hujikaza na hivyo kumzuia binadamu kufanya maamuzi yake ya hiali hivyo humfanya binadamu akashindwa kujinasua kutoka katika umeme.

Baada ya binadamu huyu kuondolewa uwezo wake wa maamuzi umeme huu pia hukaza mishipa inayohusiana na kuendesha moyo.Kwakuwa mishipa ya fahamu inayoendesha moyo huwa inacheza cheza wakati wa kuendesha moyo hivyo ikitokea electrons za namna hii zikaingia mwilini husababisha mishipa hiyo ya moyo kukaza na kushindwa kufanya kazi kama kawaida yake hivyo mtu huyu hupata shambulio la moyo na kufariki hapohapo.

Matendo haya yanafanyika kwa kasi kubwa ndani ya dakika moja madhara makubwa yanaweza yakawa tayari yamesha kutokea.

Hata baada ya kufariki mtu huyu anaweza akaendelea kunaswa na umeme hadi pale maji yatakapo isha mwilini mwake na hapo ndipo anaweza kudondoka.

NAMNA YA KUMUHUDUMIA MTU ALIYEPATWA NA SHAMBULIO LA TATU

1.Unatakiwa ufate hatua zote kama ulivyo fanya katika shambulio la pili.

2.Hakikisha unaendelea kumsaidia mhanga kuhema na kummpa huduma ya kwanza huku ukiwasiliana na watu wa hospitali.

3.Watu wa hospitali wakifika ndo wanaweza kukupa majibu ya mtu huyu kama ni mzima au amesha fariki.


SHERIA ZA JUMLA ZA KUJIKINGA DHIDI YA SHOCK YA UMEME.

1.Kagua vifaa vyako vya umeme unavyo vitumia mara kwa mara kama vipo salama au la,unaweza ukawa unamwita mtaalamu wa umeme kila baada ya muda flani kwa ajiri ya kukagua vifaa na miundombinu ya umeme wa nyumba au eneo lako.

2.Usifanye kazi ya umeme yoyote kama huna taaluma nayo,kama vile kufunga na kufungua switch,kubadilisha taa n.k.Kama utaamua kufanya hakikisha umeme umezimwa na haufiki eneo ambalo unafanya kazi hiyo katika waya za umeme.

3.utakapo hisi kifaa chako kinakutetemesha kila unapokitumia wasiliana na wataalamu wa umeme waje wakiangalie na kuondoa tatizo.

4.Funga vifaa ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuzima umeme nyumba nzima endapo mtu atakua amenaswa na umeme mfano wa vifaa hivyo ni RESIDUAL CIRCUIT BREAKER (RCD) pamoja na EARH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER (ELCB).

Tambua kuwa vifaa vya kulinda circuit kama vile MINUTER CIRCUIT BREAKER(MCB) havina uwezo wa kujizima pale mtu anavyo naswa na umeme

5.Kwa nyumba ambazo waya zake zimepita juu ya ukuta(surface wirering)Hakikisha unakagua waya zake mara kwa mara kama hazijachubuka na pia watu waepuke kuegamia ukuta wa aina hii ya wirering.

6.usifanye kazi yoyote ya kutengeneza umeme katika saketi ambayo umeme wake haujazimwa.

7.Vaa vifaa muhimu unavyo jishughulisha na utengenezaji wa umeme,mfano viatu vyenye soli pana zaidi ya sentimeter moja.Pamoja na groves.

8.Usiwashe kifaa chochote cha umeme ambacho hujui ufanyaji wake wa kazi.

9.Epuka kugusa vifaa vya umeme ukiwa haujavaa viatu vyenye soli pana,hasa vifaa kama vile friji,jiko la umeme pasi ya umeme n.k

10.Hakikisha waya zilizo chubuka katika nyumba yako zinabadilishwa au kufungwa insulation tape.

11.Epuka kuingiza vitu vya chuma ndani ya switch wakati wa kaupachika vifaa kama vile chaji n.k

12.Mfumo wa earth katika nyumba yako ni lazima uwe katika ubora ili kuhakikisha leakage zote ambazo zinaweza kuleta madhara zinaondolewa.

13.Kamba za kuanikia nguo zisiwe za chuma wala waya,pia ziepuke kufungwa maeneo ambayo yapo jirani na waya za umeme.

14.Watoto wasiruhusiwe kuchezea switch au waya za umeme,Vifaa vinavyo fungwa hakikisha ni rafiki kwa maisha ya watoto wadogo dhidi ya hatari ya umeme.

Children-Playing-with-Electrical-Outlet-Scaled1-300x232.jpg


15.Epuka kufanya kazi za umeme za line kubwa kama huna elimu ya umeme huo,pia hakikisha una vifaa muhimu vya kufanya kazi hiyo.

ZINGATIA
Madhara ya umeme hutokea katika muda mfupi sana,hivyo ni bora kuchukua tahadhari ili kuepuka matatizo kutokea kwani kama yatatokea utakua huna nafasi ya kujiokoa.

Umeme unao weza kumuuwa binadamu ni kiasi kidogo sana cha umeme tenda pengine kulikokile kinachotumika kuchaji simu yako,hivyo usidharau umeme.

Tambua kuwa hauhitajiki umeme mwingi kumuua binadamu,sababu ubongo wa wanadamu unafanya kazi kwa mfano wa umeme sasa umeme mwingine unapo ingia mwilini husababisha kuchanganyikiwa kwa ubongo na hatimaye kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo na hivyo mtu huyu hufariki dunia.

MAKALA HII IMEANDALIWA NA Ndugu Transistor.



Unaweza ku-share makala hii na rafiki zako.

Kwa makala nyingine za umeme tembelea HAPA
 
Umeibariki sana jumapili yangu kwa elimu mujarabu,hakuna kitu ninachokiogopa kama umeme,tahadhari inapaswa kuchukuliwa mara zote tutumiapo umeme na vifaa vyake
 
Mkuu asante sana kwa elimu. Mimi nina Washing machine nimeiweka chooni. Juzi wakati nazima switch nikatetemeshwa. Jee unadhani tatizo ni nini?

Pili nlipokua mdogo kitandani kulikua na sehemu ya switch lakini ilikua haikuwekwa hivyo waya zilikua nje. Sasa mimi kwa akili zangu za kitoto nikipanda kitandani nachezea zile waya lakini sirushwi na umeme. Jee ni kwa nn?
 
k4real kuna masuala hayapendez kuingiza utan acha ushamba..sio lazma kuongea kama huna cha kuongea.
 
Nifafanulie hapo kwenye kipitisho (ukiwa na maana ya conductor bila shaka) umeme, umetaja waya, hewa na maji. Wasiwasi wangu ni hapo kwenye hewa hebu weka sawa.
 
Asante kwa hili somo; ila nina swali ambalo linauliza, je! mtu anaweza kutopigwa shoti endapo akishikilia wire mmoja wa live na bila yeye mwenyewe bila kugusa kitu chenye uhusiano na ground au neutral?
Na swali lingine linatokana na jinsi ulivyosema kuwa umeme huwa unaunguza, sasa inakuwaje pale katika long transmission wires huwa hazifungwi insulator ila kwa zile zinazopita mitaani huwa zinafungwa insulator?
Asante.
 
Kipindi hiki cha mvua ningependa ku-share article hii japo ya kitambo ila bado tamu.
 
Back
Top Bottom