Tanesco mnasubiri nini kwa yule aliyekuwa na Tanesco yake Njiro? Au hamna habari?

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,188
1,576
Ukienda Arusha wanakwambia wazi kuwa kipindi cha mgao wa umeme kuna tajiri wa Arusha alikuwa na mashine au jenerata za kufua umeme Arusha Njiro alikuwa anawambia Tanesco wakate umeme Arusha yeye anawasha umeme pesa inaingia kwake, lakini ktk hatua za kampain za mwisho haswa baada ya kuona Magufuli anaelekea kushinda, hizo mashine ziliondoshwa na kufichwa maeneo fulani.

Je, Tanesco na watu wa usalama hizi habari hawana na kama hawana waende Arusha wajue kwa kina hilo jipu. Lkn nikisema tajiri wa Arusha nimefungua njia kidogo ya kuelewa wataanzia wapi.

Majipu mengine wananchi wanayasema kwa chini chini kwa kuogopa lkn watumishi wawe wazalendo.
 
Taja ni nina na kama unaogopa kutaja jina, eleza mahali hayo majenerata yalipo. Acha uoga usio na tija kwa taifa. Ukishataja tutafuatilia wenyewe na polisi wakienda kuchukua posho tunapiga picha tunamtumia Magufuli na Pm KMK
 
Mkuu hizo jenereta zina ukubwa gani na zilikuwa zikisambaza vipi umeme, au zilikuwa zinaunganishwa na nyaya za umeme wa tanesco au tajiri alikuwa na njia zake za kupitishia umeme huo kwenda kwa wateja wake?
 
"WAENDE ARUSHA" hapa nna mashaka na wewe kijana huwenda arusha unaiskiaga redioni halafu hii lafudhi yako inakera,?...."FURANI"ILO"WAZARENDO" badilika kijana!!!!!!!!
 
Hata hivyo huu muda ni wa kufanya Auditing kwa tanesco na najua watafika tu huenda wameisha fika tayari.
 
Back
Top Bottom