Waziri Makamba avunja Kitengo cha Habari na Mawasiliano TANESCO kwa tuhuma za kushindwa kulisemea Shirika

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwandishi wetu, Arusha

Waziri wa Nishati, January Makamba ameagiza kuondolewa Mara moja Afisa Habari wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) huku akiagiza kuvunjwa kwa idara ya uhusiano wa shirika hilo na kuwekwa watu wapya.

Mbali na agizo hilo pia amegiza hatua za haraka zichukuliwe kwa watendaji ambao ni wazembe ndani ya shirika hilo ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha.

Waziri Makamba ametoa maagizo hayo leo wakati alipotembelea kituo cha kupoza umeme cha mkoani Arusha kilichopo Njiro jijini hapa na kukagua hali ya upatikanaji wa umeme mkoani hapa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kukatika kwa umeme Mara kwa Mara.

Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kukamilisha ziara hiyo Makamba alisema kwamba ifikapo Febuari mosi mwaka huu ateuliwe msemaji mpya wa shirika hilo.

"Ninaelekeza msemaji abadilishwe ifikapo febuari mosi mwaka huu achaguliwe mpya" alisema Makamba

Waziri Makamba alisema kwamba kumekuwa na changamoto kwa Tanesco kuwasiliana na wateja wake pindi umeme unapokatika ghafla hali ambayo imekuwa ikipelekea malalamiko mengi na lawama kwa serikali.

"Tanesco lazima iwasiliane na wateja wake kwa wakati hii ni changamoto umeme unapokatika hivyo ni lazima wawasiliane na wateja wao kwa wakati" alisema Makamba

Hatahivyo,alisisitiza kuwa idara nzima ya uhusiano ndani ya shirika hilo lazima ivunjwe na wawekwe watu wapya wanaoweza kuendana na kasi na uweledi ndani ya shirika hilo.

"Mnawasikia wasemaji wa vilabu vya soka vya Simba na Yanga hivi mmeshamsikia msemaji wa Tanesco?" Alihoji Makamba

Hatahivyo,Makamba alisema kuwa serikali haifurahishwi na hali ya kukatika kwa umeme Mara kwa Mara na kuitaka Tanesco kutojificha nyuma ya mgongo wa waziri.

"Hatutaki waziri wa nishati ageuke kuwa msemaji wa shirika tumewaambia menejimenti wasijifiche nyuma ya wizara" alisisitiza Makamba

Waziri Makamba alisema kuwa serikali inakusudia kubadilisha mfumo teknolojia wa Luku ndani ya miezi 18 kuanzia sasa ambapo wateja watakuwa wakinunua umeme moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi na kisha kupata umeme bila kuweka tokeni.

"Mtu ananunua umeme kupitia simu yake ya mkononi na unaingia moja kwa moja kwenye mfumo na sio kuchukua tokeni na kwenda kuingiza kwenye mita" alisema Makamba

Alisema kwamba ifikapo mwezi Juni mwaka huu wateja wote takribani elfu 80 wanaosubiria kuunganishiwa umeme wataunganishiwa umeme huku akibainisha kuwa serikali inatarajia kubadilisha mfumo wa maombi ya umeme ambapo utakuwa kupitia mtandao.

Waziri Makamba alibainisha kwamba serikali inakusudia kubadili mfumo wa usambazaji wa umeme kote nchini ili uendane na kasi ya ongezeko la wateja kwa kuwa mfumo uliopo kwa sasa ni wa kizamani.

Mwisho.

IMG-20220125-WA0041.jpeg
IMG-20220125-WA0042.jpeg
 
Maneno meeeeeeeeeeeeeeeengi.

Mara wasemaji wa Tanesco waondolewe,Mara mfumo mpya wa luku na blah blah blah kibao

Wkt the real issue ambayo Ni umeme kukatika hovyo unai rukuruka,Ila nimekumbuka kitu mama anaupiga mwingi sana.
 
Msemaji kama hapewi info za kutoa na wakubwa wake, inamuhusu nini!

Hataki kudanganya, sasa unamuondoa ili iweje.

Waziri umechemka na maji moto yenye na degree 1000, umeongea mengi na wewe hujasema why tatizo lipo.

Umefeli as hao wote sio kiini, hawataki kutudanganya.

Mnakula tu kwa urefu wa kamba zenu.
 
Kwenye kiwanda chetu cha ufyatuaji tofali tumekua tukiharibu Cement mara kwa mara na hili linatokana na kitengo cha mawasiliano TANESCO kutotutaarifu kwamba kutatokea changamoto ya kukatika kwa umeme.
Inasikitisha pale ambapo wanakata umeme bila taarifa, ni bora waseme ili mtu ujue moja, kuwa leo kazi isiwepo kuliko kupata hasara
 
Waziri wa Nishati Mh Makamba amevunja kitengo cha habari na mawasiliano Tanesco akikituhumu kimeshindwa kulisemea shirika na kulitetea shirika kwenye nyakati ambazo kitengo na watu wake kimetakiwa kufanya hivyo!

Ikumbukwe kitengo cha habari na mawasiliano kinaongozwa na mwana dada Badra Masoud kwa misingi hiyo amekali kuti kavu.

Maswali ya kujiuliza...
Ni kweli kitengo hichi ndicho tatizo kwenye shirika?
Ni kweli wameshindwa kuitetea Tanesco?

IMG_0609.jpg
 
Makamba anavyodai kitengo kimeshindwa kuitetea Tanesco ana maana gani? anataka kitengo kiwe kinazalisha propaganda au kifanyeje?

Navyojua hao watu wa idara ya habari wanatakiwa kupewa taarifa za majibu ya kero za wateja kutoka kwa wahusika (waziri, naibu wake, katibu mkuu nk) then wao ndio watangaze taarifa hizo kwa umma.

Sasa mfano wananchi wakiulizia ujio wa ile winchi ya tani 26 toka huko ilipoagizwa mbona mpaka leo kimya? Makamba anataka hao jamaa wa kitengo cha habari wajibu kitu gani kama hajawapa majibu?
 
Serikali kwanini haitaki kukiri kuwa kuna mgao wa umeme? Kwahiyo wakibadilishwa ndio umeme utaacha kukatika.
 
Back
Top Bottom