Tanesco, mgao kimya kimya?

Mr. Miela

JF-Expert Member
Aug 2, 2007
1,226
2,055
Wandugu, Nahisi kuna mgao unaoendelea Tanesco kwani huku Arusha ikifika saa moja jioni matatizo! Je kwa vile Tanesco ni damudamu na CCM wanaogopa wakitangaza kipindi hiki kura hazitatosha? Vipi mitambo iliyowashwa kwa kodi zetu? Chama cha walaji kina msaada kwetu?
 
Huku mwananyamala kwa msisiri ndio balaa.Umeme unakatika siku nzima ,unawaka jioni kwa lisaa moja ,unakatika tena mpaka saa nne.
Na siku wakiamua kuuwasha unakuwa mdogo sana.
Wanaogopa wakitangaza utaathiri kura za 2010.Lakini nadhani kuna mgao wa umeme halafu mkali kwelikweli.
 
Ni Kweli kuna "mini-mgao" na TANESCO waliniambia kuwa wangeweza kuto ratiba jana hili kuweka mambo bayana! Sikuambiwa unatokana na nini, lakini uchaguzi unapokaribia kuna hujuma nyingi ufanyika ili hela ya kampeni ipatikane!
 
Sure!!!Arusha sasa ni wiki ya pili,unakatika saa 1 jioni na kurudiswa saa 4....Na nahisi ni maeneo mengi ya mji wa Ausha...

Tuambiwe ili tujiandae na huo mgao.
 
huyu twiga mnyonge keshajichokea nadhani hata wafanyakazi wenyewe wa tanesco wanapokea tu mshahara lkn hawajui ni nini kampuni yao inafanya
 
Mgao kama kawaida hapa Arusha na hata ratiba wametoa lakini wala hata hawa fuati siku na muda wa kukata umeme...
 
Back
Top Bottom