TANESCO, mgao huu una sababu gani tena?

Bado tu hamjajua sababu ya kuitwa malofa na mzee Mkapa? Kweli mijitu mingine bado tumelala huku tunalilia umeme. Mtamkumbuka Muhongo
 
Arusha imekuwa ni kawaida sasa, wanasubiri oct 25.

kwa sababu Arusha ni kitovu cha mabadiliko hauna maji wiki ya tatu (3) sasa, na hakuna Umeme maeneo mengi ya mkoa huu. mfn. jana wamerudisha umeme saa tano za usiku na kuukata sa tisa usiku huo huo.

Wananchi wamepeleka malalamiko ya kukosa huduma muhimu kama maji, shirika (AUWSA) Badala ya kutuma wataalam wao wametuma wasoma mita!
 

Nako NSSF mambo ni hayo hayo tu!
 

Acha ukanjanja na Porojo wewe.
 
Nadhani bado hujatoa sababu za kisayansi kwanini umeme hautoshi na siku za nyuma ilikuwa inatosheleza??????
 
Mkuu umewauliza wafanyakazi wapi, shirika linamsemaji wake...... kwa nini usimuulize kupata ukweli.

Sio kila mfanyakazi ni msemaji wa TANESCO.

Ulishawahi kumuona Msemaji wa Shirika/Taasisi yoyote akitoa Habari hasi inayohusu Taasisi/Shirika analolisemea?
Hawa kazi yao si ni ya kukanusha tu chochote kinachosemwa kuhusu Taasisi/Mashirika yao hata kama ni cha kweli.
 

Na zinatakiwa MW ngapi? Kukidhi mahitaji kwa Nchi zima?
 
Koleba:- Ukweli ni kwamba TANESCO inatimiza mataka ya waasiasa kwa kutosema ukweli maana Visima ya gesi haviko vya kutosha kwa sasa kufikia pressure ya above 60bars kwenye bomba la 36" ili angalau Symbion A itembee at 80%. Kinyerezi plant ndo kwanza piping hajakamilika maana wachina wa TPDC walikuwa hawana vifaa muhimu kama Isolation valves na 8" pipes na tunajua hawako tayari forany plant commissioning kwa sasa.
Kwa kifupi gas ya Mtwara kwa sasa inazalisha only 80MW badala ya expected 300MW kwa sababu ya matatizo ya kiufundi na kimikataba kati ya TPDC na wawekezaji na siyo swala la kuwasha Mitambo. Tell the truth t Tanznians please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona TANESCO hawajatutangazia mgao wa umeme, pia mitaa ya kwetu umeme upo.
....Jamaa atakuwa anaishi Masaki coz huku uswazi (Kibosho Road) umeme unakatika Asubuni hadi saa 12jion,kisha saa 12:45jioni hadi saa 5 usiku.So natumia umeme dakika 45 kwa siku.Najiuliza hayo matengenezo yanafanyika wakati wa taarifa za habari tu?,..Wananikera sana siyo siri...
 
Hawa tuwawajibishe tarehe 25 Oct. kudanganywa tumechoka, tujaribu chama kingine tuone, wamezoea. Mwanzo Tanesco walisema umeme utakaa vizuri mwishoni mwa wiki ya kwanza ya Septemba, sasa tuko mwishoni mwa Septemba.
Wameanza kudai tena mwishoni mwa Octoba. Cha kushangaza kama kuna matukio ya CCM umeme unakuwepo. Tunajua kuunganisha moja na mbili. Tarehe 25 Oct. itakuwa kiama endeleeni kutuudhi, ili tukose huruma kabisa.
 
Mkuu umewauliza wafanyakazi wapi, shirika linamsemaji wake...... kwa nini usimuulize kupata ukweli.

Sio kila mfanyakazi ni msemaji wa TANESCO.
...kama wewe ni mfanyakazi wa TANESCO naoumba mbadilike kwa kweli sababu mnatuathiri vibaya sana...
 

Mkuu kwani wewe ulifikiri ni ukweli sababu walizotoa Tanesco ??
 
....Hiyo mitambo inazimwa wakati wa taarifa za habari tu..
 
Nitafurahi kusikia jibu. Can you imagine katikati ya jiji (Dar es Salaam) umeme kukatika asubuhi Jumatatu siku nzima na usiku wake (24 hours and counting)!
 
...Hili tatizo linaitwa Vacuum chemba analysis,na tumerifanyia upembuzi yakinifu kwa kina zaidi.Na liko under inspection capucha zone...
 
Hili jibu kwetu sisi ni la kisanii! Je wamezima na mitambo ya IPTL, SYMBION na ya aina yake? Unawezaje kuwazimia watu umeme kwa zaidi ya masaa 24 mfululizo na ukatoa sababu dhaifu hii?
 
Kuna mtu anaamini kwamba gesi hii itatunufaisha? Mbona gesi ya kupikia inapanda bei kila siku? au hiyo gesi ya mtwara haina uhusiano na hii gesi ya kupikia??? CCM kwa uongo bwana! ndio maana hawaelewi kwa nini nchi hii ni maskini.
 

Eti litakamilika baada ya uchaguzi haha
 
Haya maelezo hayana mantiki yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…