Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,586
- 4,274
Ni habari Njema kwa Stiglers George kuanza kutoa umeme tangu Feb 25th, hivyo tuna amini mgao wa umeme utapungua sana kama sio ukisha kabisa.
ANGALIZO
Kwa kuwa stiglers tumeambiwa in outlets (vinu 9) na jana wamewasha kimoja tu; Pengine wahakikishe hawawashi vyote ili tuwe na backup pale panapotokea matatizo.
Nimesema hivyo kwa sababu zifuatazo;
1. Kuwasha vinu vichache, itatuhakikishia kuwa na maji mengi yatayotosheleza kutoa umeme hata kipindi cha kiangazi kwani kwa vinu vichache maji yanatiririka kidogo kidogo.
2. Tutakuwa na mitambo (vinu vya akiba) vitakavyo tumika kubalishana pale mtambo mmojawapo unapokuwa na hitilafu au pengine tunapo hitaji kuifanyia mitambo service
3. Habari ya kuweka mgao wa umeme kwa kigezo cha kufanyia mitambo service au kuharibika kwa mtambo mmoja haina nafasi tena kwa karne hii
4. Habari ya kuweka mgao kwa sababu maji yamepungua kwenye mabwawa mengine itakuwa historia kwani tutakuwa na uwezo wa kuwasha kinu kingine(cha akiba) kukabiliana na hali hiyo
5. Kwa sasa tujikite kwenye kuwa na umeme wa uhakika kwa matumiazi ya ndani kwa asilimia 100% kwa mwaka mzima na sio kwa kipindi cha Mvua. Suala la kufikiria kuuza umeme nje, lisiwe kipaumbele kwa sasa kwani tukiwasha vinu vingi kwa ajili ya kuuza umeme, msimu wa kiangazi tunaweza kurudi kulekule kwenye giza.
MWISHO
TANESCO wawe na tabia ya kufikiria (forecast) changamoto za umeme miezi au miaka kadhaa kwani wanachi wanaolipia huduma, wanataka matokeo/umeme wa uhakika, wa bei nafuu na huduma za haraka.