Tanesco Manispaa ya Morogoro, Utapeli huu wa miaka mitano, kulikoni?

Tanesco Manispaa ya Morogoro, Utapeli huu wa miaka mitano, kulikoni?

proisra

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2012
Posts
215
Reaction score
159
Wakazi wa Mtaa wa Bigwa Sokoni (Kilakala), Manispaa ya Morogoro wameelekeza shutuma zao nzito kwa uongozi wa TANESCO Manispaa ya Morogoro kwa hatua ya shirika hili kuwaandikisha majina kitapeli na kuwalipisha fedha zao kwa ajili ya kupatiwa umeme tokea Mwezi wa Juni 2008 hadi sasa lakini huduma hiyo haijatolewa hadi sasa. Wanasema kilichofanywa na TANESCO mwaka huo wa 2008 ni kupima maeneo yao na kuchimbia nguzo mbili ambazo ndizo zitakazobeba transfoma, kama picha hapa chini inavoonesha. Wakazi hawa wanahisi nguzo hizi tayari zimetelekezwa kabisa, kwani siyo kawaida nguzo kuachwa miaka zaidi ya 4 bila kufuatiliwa kinachoendelea.


Baadhi ya wananchi waliohojiwa (majina yanahifadhiwa) wameshangazwa na hatua ya TANESCO Morogoro kuwatelekeza na kutotimiza ahadi yao kama walivyoahidi. Wanasema giza totoro limeendelea kuwepo, huku Meneja wa shirika hili mkoa wa Morogoro akiwa hana majibu ya maana. Maajabu ni kwamba, Mtaa wa Bigwa-Sokoni unapatikana ndani ya kilometa 5 tu kutoka katikati ya Mji, jambo ambalo lisingetarajiwa na mtu yeyote kwenye mji wowote. Miongoni mwa wakazi wa mtaa huu ni wakufunzi na wasomi mbalimbali wa vyuo vikuu vya SUA, Mzumbe, Jordani n.k. Wamekerwa sana na tabia ya uongozi wa shirika hili kuwajali wawekezaji ambao mwaka huu walijenga Hoteli kwenye Milima ya Uluguru jirani na mtaa huu, na tayari wakubwa hawa wameshapelekewa umeme bila kikwazo au longolongo, huku wananchi hawa ambao ni wapiga kura wakiachwa kwenye mataa.

Baadhi ya kumbukumbu za fedha ambazo wananchi hao wa zaidi ya kaya 60 walilipishwa kipindi hicho zinaonesha TANESCO kupokea fedha kama Application forms, kwa uchache kuanzia receipt number 002186842 hadi 002186869 zilizotolewa na TANESCO Morogoro kwa pamoja tarehe 18 June 2008. Kutokana na idadi ya watu katika manispaa kuongezeka, idadi ya wanaosubiria umeme huu hadi sasa katika mtaa wa Bigwa-Sokoni inakadiriwa kuvuka kaya 100. Wameomba serikali kuingilia kati sakata hili, kwani maendeleo yao yamekuwa yakirudishwa nyuma kwa kukosekena kwa umeme muda wote huu, huku uhalifu nyakati za usiku ukinyemelea maeneo yao kutokana na giza.
 

Attachments

  • DSC01372.JPG
    DSC01372.JPG
    408.5 KB · Views: 45
  • DSC01371.JPG
    DSC01371.JPG
    924.2 KB · Views: 55
  • DSC01384.JPG
    DSC01384.JPG
    382.9 KB · Views: 51
  • DSC01386.JPG
    DSC01386.JPG
    371.1 KB · Views: 53
  • DSC01385.JPG
    DSC01385.JPG
    376.3 KB · Views: 34
Poleni sana sie huku kihonda eneo letu tumeambiwa kuna mradi wa mcc mwaka wapili sasa tunalala giza tanzania yenye neema tele inashindikana
 
Huku KINGULWIRA pia walikuja na biashara kama hizo mpaka wakati huu maeneo ya shule ya msingi lakini mpaka wakati huu ni usanii wa BIGWA. Huu MKOA WETU hawa TANESCO mbona wanataka kufanya umeme uwe ni kitu cha ANASA. UCHAPA KAZI WAO UKO WAPI?
 
Back
Top Bottom