TANESCO kuna nini?

TANESCO kuna nini?

Ufafanuzi

Mteja mwema na mwenye nia njema anashauriwa kuwa anatoa ushirikiano kwa kuwa bila kufanya hivyo hakuna hatua zinazoweza kuchukuliwa, hata ukienda bank hauwezi kusema sina acc namba angalieni kwenye database, hivyo ni vema wateja wetu mkajenga utamadumi wa kutoa taarifa kamili kwa huduma bora.wakati mwingine tumeshuhudika wengine wakiandika page nzima lalamiko mnamfikia hana tatizo lolote anasema nalalamikia wengine ndio maana tunashauri kutoa taarifa kamili.
Taarifa ni kwamba Tanesco ya Mlandizi ni rushwa tupu hakuna mnachofanya .

Maombi yamejaa kila siku mnasingizia hamna vifaa
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja
Hakika shirika letu limekuwa UTOPOLO wahed.

Yaani mmekata umeme Kibaha kisha watu wanaulizia nini tatizo mnawaomba namba ya taarifa na anuani zao?

Mungu atusaidie hili shirika ligawanywe na kubinafsishwa.
 
Ila huyu jamaa wa tanesco anayejibu hizi msg ni muungwana sana daaah.
Umeme kukatika Kibaha anahitaji namba ya tukio, na anuani ya mtoa taarifa.

Yaani hana haja kujua kama umeme umekatwa Kibaha. Yeye anajua umeme umekatwa nyumbani kwa mtu mmoja


TANESCO hii ni taabu. Wanatukomesha
 
Mbagala pia mmekata umeme asubuhi hii kweli?!! Na mnajua leo ni siku gani alafu unataka taarifa za mtu na ameshakupa taarifa shida ipo wapi.
Sio kila tatizo ni la kuliaproach kama bots inaboa kwa kwrli
 
Na unaona Upo sawa. Watanzania tumezoea Matatizo
Heb vaa viatu vyake mkuu kama ungekuwa wewe ungefanyaje!ungeenda kuwateka waje wafunge kwa nguvu?

Usifikiri mtu hafuatilii anafuatilia sana ila akifika Tanesco anaambiwa subiri utapigiwa simu unadhani akijibiwa hivyo mara tano atahangaika nao,na pakulalamika hamna na wengi wanaofanyiwa hivi ni wale wa REA ila wateja wa cash ndani ya wiki tatu mtu anapata moto.
 
Taarifa ni kwamba Tanesco ya Mlandizi ni rushwa tupu hakuna mnachofanya .

Maombi yamejaa kila siku mnasingizia hamna vifaa
Mimi nilikuwa najua wote wanaoishangilia CCM mna maisha mazuri kumbe na nyie mnaunga unga?

Wewe ukiwa kama mwanaccm damu na upo bega kwa bega na mama changia uchumi wa shirika onyesha mfano wa uzalendo kwa kutoa 525,200/= upate mwanga siyo kulalamika rushwa rushwa kwani rushwa nyie wenyewe si ndo mnaoilea?
 
JamiiForums na Moderator Tafadhali ifungieni Account ya TANESCO kwa muda au ficheni post zote ambazo imekuwa ikiomba taarifa za watu Binafsi au wekeni mfumo wa hizo taarifa kuonekana kati ya watu account hizo tu (account ya Tanesco na Mtu husika)
 
Hili shirika kuna watu wakubwa wanahusika Inakuwaje Waziri wa Nishati anasema nguzo za Lv BURE ila Kodi sshs 27000/- je hasara ya bei halisi ya nguzo inabebwa na nani? Au tozo? Tanesco mzigo unawalemea acha siasa za mbwembwe itafitisika
 
Heb vaa viatu vyake mkuu kama ungekuwa wewe ungefanyaje!ungeenda kuwateka waje wafunge kwa nguvu?

Usifikiri mtu hafuatilii anafuatilia sana ila akifika Tanesco anaambiwa subiri utapigiwa simu unadhani akijibiwa hivyo mara tano atahangaika nao,na pakulalamika hamna na wengi wanaofanyiwa hivi ni wale wa REA ila wateja wa cash ndani ya wiki tatu mtu anapata moto.
Unachosema ni sahihi, nimelipia umeme tangu October mpaka leo kimya na umbali wa kutoka kwenye nguzo mpaka nyumbani ni chini ya Mita tano lakini sijaunganishiwa umeme mpaka leo. Niliweka ratiba ya kwenda kila wiki mara mbili kufuatilia lakini majibu yao ni subiri utapigiwa simu mpaka nikaamua kununua Solar. Kiukweli wanakera sana wala sio Siri na Kwa kuwa ni Monopoly system huna cha kuwafanya unabaki kulalamika huku maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom