Tanesco jaribuni hii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco jaribuni hii!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MAKOLE, Oct 2, 2012.

 1. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nimeona tangazo la Tanesco kupitia ofisi yake ya uhusiano ikitoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni yao kuwa wanataka tanesco iweje ili kuboresha huduma. Kwa maoni yangu na jinsi ninavyoiamini Jamii Forum ingekuwa ni sehemu muhimu sana kwa Tanesco kupata maoni sahihi na kwa wakati muafaka.

  Namshauri afisa uhusiano wa Tanesco asiogope kujaribu kuitumia Jf ili kufanikisha lengo lao.

  Nawasilisha!
   
 2. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #2
  Oct 2, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  wasi thubutu kabisa ! Mitusi hawataweza kuibeba !
   
 3. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 430
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Si mara zote kuna "mitusi" mbona mara nyingi tu kunakuwa na constructive opinion?
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  huu ni ujinga mwingine wa Tanesco, sipati picha kwa shirika lenye management na board, linarusha jiwe gizani ati wateja ndio wawaeleze shirika liweje bila mwongozo wowote wa maoni!.
   
 5. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  mchillo, na mie napingana na huyo anayedai kwamba Tanesco wataambulia mitusi iwapo wataleta hoja hiyo JF. Katika hizi forums tuna watendaji wa Tanesco wengi tu, ingawa hawajitambulishi rasmi, huwa wanatupatia data za ndani nasi tunawapa ushauri. Naamini katika JF kuna watu wanaofanya kazi katika 'utility company' za aina ya Tanesco kutoka nchi mbali mbali, hivyo wangeweza kutupatia uzoefu wa kuijenga Tanesco mpya toka huko walipo, iwapo Tanesco ingelea rasmi hoja hiyo hapa JF, hata kwa jina bandia. Gama, ni kweli walichofanya Tanesco ni 'uhuni' fulani hivi. Hawajasema wanataka maoni toka section ipi, kati ya tatu walizo nazo i.e. generation, transmission & distribution. Ya mwanzo (generatio)na hii ya mwisho (distribution) ndizo zenye migongano mikubwa ya kimaslahi kwa sababu ndiko ulaji ulipo. Transmission hakuna shida sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  najua ni kwanini wanafanya uhuni huu, mara zote management za tanesco zimekuwa za kimajungu huku kila nayepata nafasi akijihami na kutaka waliomtangulia waonekane wabaya, hakuna anayekuja na hoja zinazolenga kunufaisha shirika, bali kujijenga yeye binafsi na kundi lake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  lile tangazo limekaa kinafiki na kimajungu, yaani wataalamu wote waliojaa humo na ma Masters na PhD, then wapewe ushauri kutoka mtaani ? Hivi m'mechukua muda kidogo kufikiri ?
  I cant buy it !:A S-coffee:
   
 8. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 841
  Trophy Points: 280
  Ukiwa 'jf' unaweza dhani ni huku tu, la hasha! Hata 'fb' kule kuna hali kama hii na wamefungua page yao kule. Siku moja tembelea page za makampuni ya simu kule uone dhahama wanayoipata ndio utaamini
   
 9. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  ..............yaaani mie ndo niwashauri mbinu gani watumie ili umeme upatikane 24/7 !
  Mizaha mingine bora mtu akutukane !
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Utalipwa mkuu_hakuna ushauri usio na malipo....swali_ni je watalipa wangapi..?...maake wote tutatoa ushauri
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  na watachukua ushauri wa nani na waache wa nani?,
   
Loading...