Mada yangu ni swali, je kuna uwezekano wa kuwa na makampuni ya kushindana na TANESCO?Mkuu kama umesoma pysiscs angalau hadi kidato cha nne umekutana na kanuni hii; "At the given state, energy can change from one state to another but can not be neither created nor destroyed"
Kwa maana hiyo ili umeme uusafirishe lazima uubadilishe uende kwenye state nyingine swali langu ni kuwa utaubadilisha uwe nini ndio uusafirishe? Utaunasili uwe sauti? Au uwe heat? Au utafanya muujiza gani wa kuubadili kwenye energy nyingine ambayo itakatiz a kwenye solar system ambapo napo pana energy ya kutosha tu? Kuliko kuwaza kusafirisha umeme wireless kwa nini usivune tu kutoka kwenye jua na kuupata wa bure kabisa kwa kununua solar panel? Au kwanini usinunue mitambo ya upepo ukazalisha umeme wako wa bure?
Mkuu tuache porojo mawazo yako hayawezekaniki milele.
Dah! washa waacha gizani mapema hivi?Hawa wapuzzi wanakata kata sana umeme..imagine asubuhii saa kumi na mbili kasoro wamekata umeme jtatu yote hii...jpili wamekata..jmosi...ijumaa why...[emoji32][emoji32]
Mkuu kwenye maelezo unasema kinu kimoja kinauzwa USD 250 billions, kabla sijasema kitu, je hiyo figure ipo kwenye billions au millions?[Labda ulijichanganya?].......Maana USD billions 250 ni zaidi ya 500 Trillions Tshs.
Nadhani Tanesco ipo siku watajapata ushindani,kwani kuna project niliiona mtandaoni ikisema yakuwa kuna umeme wa wileless utakuja kuja baada ya miaka kadhaa ijayo huku barani africa ila kwa ulaya nadhani ushaanza huo umeme wa wileless
Sawa Mkuu,....hata kwenye ku-search kwangu nimegundua hii issue ni tata kuliko tunavyoweza kufikiri.Mkuu nashukuru kwa kurekebisha ni 250mil usd kwa limited edition gas plant na nearly 1bilion usd kwa full fledged gas power plant with 300MW capacity...
Nilipitiwa tu na typing....thanks though bruh!
Kama pangekuwepo na makampuni mengi, TANESCO wangecharuka na kujitahidi. Hebu imagine kama tungekuwa na Kampuni moja ya mtandao wa simu, gharama za kutumia simu si zingekuwa juu sana?
Toeni kero zenu kwa kuainisha wapi mlipo(maeneo) ili tuwafungie safari hao wazinguaji!. Hatutaki ujinga enzi za Hapa kazi tu.
Ukiyatazama makampuni ya simu, utagundua kwamba yanaajiri watu wa masoko wenye kufanya kazi nzito sana kuanzia january mpaka desemba.
Hii ni kwa sababu ya ushindani uliopo sokoni, kila kampuni ya simu ni lazima itoke nje na kuingia mtaani kwa ajili ya kupata wateja wapya.
Nadhani ufike wakati ambapo TANESCO isiwe ndio kila kitu katika masuala ya umeme. Nchi imeumizwa sana kwa sababu ya ukiritimba wa kampuni mmoja tu yenye kushughulika na usambazaji wa umeme nchi nzima.
Nchi zilizoendelea wananchi wanayo machaguo ya kutosha kwenye masuala ya nishati ya umeme. Kampuni moja ikijisahau na kushindwa kuendana na mahitaji ya wateja, watu wanaachana nayo na kuangalia ustaarabu mwingine.
Huu ukiritimba sio wa dunia ya viwanda, sio wa dunia ambayo serikali inafanya biashara kwa kiwango kidogo sana. Huu na uwe ni muda sahihi kwa watu wenye mtaji na ufahamu kwa maana ya elimu kwenye masuala ya umeme, kuweza kuingia sokoni.
Maendeleo ya nchi yanakuwa yanawekewa mipaka ya kukua kwa sababu ya gharama kubwa za nishati, gharama ambazo kwa nchi nyingine haziwaumizi vichwa kwa sababu ya wigo mpana wa wazalishaji na wasambazaji wa umeme.
Hakuna lisilowezekana kama nia ipo. Naamini sababu ya msingi ya kuondokana na ukiritimba wa TANESCO ipo.
Exactly! Well noted!kaka munajidanganya hapa jamii forum, natamani mujue haya mambo yanavyoenda, umeme sio frequency za redio, umeme sio frequency za mitanda ya simu........................................La msingi unatakiwa kujiuliza aliyeatangaza ni DG wa ewura aliyetumbuliwa ni mkurugenzi wa tanesco while mandate ya kuikataa proposal ilikuwa chini ya mikono ya EWURA.......................lugha nyepesi hapo ni kulikuwa na kuna kuelewana kati ya MRAMBA na MUHONGO hasa kwenye mambo yaliyokuwa yametangulia
Mkuu umeelezea kitu kizuri sana, naaminj umetufungua wengi.Usijidanganye. Hata sasa hivi kunaushindani kwenye kuzalisha umeme. Tatizo ni mikataba yakifisadi ambayo Tanesco imeingizwa na viongozi wa serekali. Na swala la usambazaji ni inefficiency kuwa na makampuni mawili ya kusambaza umeme. Kwana vitu kama national grid ni swala la national security huwezi kuachia makamupuni binafsi kama PAP kuendesha. Sana sana wanaweza ku privataze local distribution kama mkoa kwa mkoa. Nigeria wamefanya hivyo lakini haija saidia. Kwakifupi huwezi kuwa na option ya kupata umeme kutoka makampuni mawili tofaiti kwenye mji mmoja. Hoyo inawezekana kwenye Telco services lakini sio umeme. Sana sana kama bongo wangekua na sheria nzuru basi ingewezekana kipata makampuni yanakuja kukuwekea solar panel kwenye paa zanyumba bila kuzinunua ila unakua unalipia umeme kwa mwezi. Tatizo la hio option ni CAPEX na inaitaji serekali labda iweke tax exemption na sheria za kuweza kuingia na wateja mkataba wa miaka kama kumi. Pia kuna wizi pia.
Nchi ambayo kwa sasa hapa africa swala la umeme na bei yake iko chini ni Ethiopia. Ambao umeme wao unatokana na hydro power. Nchi imemekuwa committed kuzalisha megawatt kwa megawatt ili kuendeleza uchumi. Hawa kamaa ni very creative. Wamefikilia swala na kutumia fossil fuel na natural gas ni shida kwani unahitaji investment kubwa sana kwenye uchakataji na pia mwisho wasiku gharama ya umeme itakuwa juu tu. Tanzania ni nchi iliyojaliwa mito mingi sana. Kwanini wasije na aidea ata ya kujenga hydro power angalua nne au tano kwenye mto rufiji. Yaani wafanye kama wenzao walivo fanya huko Ethiopia kwenye chanzo cha mtu nile. Huwa nafikilia sana. Sisi tumekomaa na gas tuu ambayo pia nasikia sio yetu na inauzwa bei ya juu zaidi ata ya bei ya gas ya dunia.Mkuu umeelezea kitu kizuri sana, naaminj umetufungua wengi.
Hivi mfano haiwezekani kua na kampuni nyingine ambayo itazalisha umeme kwa kutumia windmills?
Au kutumia malighafi zingine ambazo teknolojia ya TANESCO bado haijawa na uwezo nayo?