TANESCO hii ya maombi mapya ya umeme ni mtego wa rushwa

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Shirika la Tanesco siku hizi lina utaratibu wa ajabu kwa mwombaji wa kuunganishiwa umeme. Mteja anajaza fomu na inapokelewa na kisha wanakwambia zamu yako ikifika watakupigia! Hawataji siku wala tarehe na mteja anakaa kusubiri bila kujua hatima yake nini. Huu mfumo unasababisha rushwa ya dhahiri maana haiwezekani mteja kukaa na kusubiri bila kupewa taarifa kuwa ikifika siku kadhaa uje kufuatilia.

Mfumo mbovu wa hovyo unatengeneza mianya ya rushwa maana itabidi umtafute surveyor ili ukadiriwe gharama.

Vv
 
Shirika linaloongoza kwa rushwa halafu kuna mtu anasema mimi rais wa wanyonge!!!!
 
Huo ndio utaratibu halisi, wa ki ofisi ukisema usikilize ya wana siasa, unaweza fikiria matatizo ya shirika hawayajui!!hasa ukimsikiliza waziri unaweza fikiria kuwa nikienda kulipia leo nitapata umeme kesho!!waache siasa!!mala utamsikia kuwa ni marufuku kumlipisha mteja nguzo huu ni mwaka wa tano sasa anasema hilo hilo, lakini hakuna kitu!!hawa wana siasa wana jua kabisa hali ilivyo lakini kutafuta sifa tu!!
 
Wabongo walalamishi balaa. Utaratibu ni huo. Wanakupigia simu ndani ya siku 30. Mara nyingi ndani ya siku 20 wanakuwa washakuja. Sasa wewe na kiherehere chako utake kupata umeme ndani ya siku 3 ndio unaleta rushwa. Kwa hili Tanesco nawatetea.
 
Jaza Maombi mapema. Ukijaza mda mfupi tu unataka umeme hapo rushwa mhimu..wewe Ndio unaetengeneza rushwa.
 
Shirika la Tanesco siku hizi lina utaratibu wa ajabu kwa mwombaji wa kuunganishiwa umeme. Mteja anajaza fomu na inapokelewa na kisha wanakwambia zamu yako ikifika watakupigia! Hawataji siku wala tarehe na mteja anakaa kusubiri bila kujua hatima yake nini. Huu mfumo unasababisha rushwa ya dhahiri maana haiwezekani mteja kukaa na kusubiri bila kupewa taarifa kuwa ikifika siku kadhaa uje kufuatilia.

Mfumo mbovu wa hovyo unatengeneza mianya ya rushwa maana itabidi umtafute surveyor ili ukadiriwe gharama.

Vv
Fuata utaaratibu wa shirika, ukisikiliza siasa utaoza. kwani uko peke yako
 
Na huku kwetu umeme ukikatika utamsikia Mwananchi anasema "jamani si walisema hakutakuwa tena na mgao?" mimi huwaambia "huu sio mgao acheni majungu" basi wanasema "duh afadhali"
 
Wabongo walalamishi balaa. Utaratibu ni huo. Wanakupigia simu ndani ya siku 30. Mara nyingi ndani ya siku 20 wanakuwa washakuja. Sasa wewe na kiherehere chako utake kupata umeme ndani ya siku 3 ndio unaleta rushwa. Kwa hili Tanesco nawatetea.
Mbona hawatupi huo utaratibu wateja wao? Kwa utaratibu wa masijala unatakiwa wakupe namba ya maombi na tarehe ya kufuatilia ikiwa muda waliokupa umepita.

Vv
 
Shirika la Tanesco siku hizi lina utaratibu wa ajabu kwa mwombaji wa kuunganishiwa umeme. Mteja anajaza fomu na inapokelewa na kisha wanakwambia zamu yako ikifika watakupigia! Hawataji siku wala tarehe na mteja anakaa kusubiri bila kujua hatima yake nini. Huu mfumo unasababisha rushwa ya dhahiri maana haiwezekani mteja kukaa na kusubiri bila kupewa taarifa kuwa ikifika siku kadhaa uje kufuatilia.

Mfumo mbovu wa hovyo unatengeneza mianya ya rushwa maana itabidi umtafute surveyor ili ukadiriwe gharama.

Vv
Je umerudisha fomu kwa jina gani?wilaya na namba ya simu
 
Kuna viumbe wanaitwa Saveya,wanakula rushwa kama mchwa...
Saveya wamejiwekea utaratibu wa rushwa ya shilingi thelathini alfu.
Sema tu sitaki kumharibia mtu mwenye familia kazi. Lkn wakiendelea, hasa wale kwenye kile chumba Cha kuchukulia fomu. Hakika watajisoma kwenye magazeti.
 
Kushindwa kutoa taarifa kamili kwetu au TAKUKURU ni kuendeleza kutoa taarifa za uongo ambazo hazisaidii kuratutua tatizi.Unapoamua kulalamika toa ushirikiano ili kujua ukweli maana wakati mwingine mnatoa kwa vishoka na kusema umempa TANESCO
 
Wabongo walalamishi balaa. Utaratibu ni huo. Wanakupigia simu ndani ya siku 30. Mara nyingi ndani ya siku 20 wanakuwa washakuja. Sasa wewe na kiherehere chako utake kupata umeme ndani ya siku 3 ndio unaleta rushwa. Kwa hili Tanesco nawatetea.
Bro wanaolalamika maanake limewakuta! Siyo viherehere!
Yamkini wewe ulibahatika kupigiwa simu within time! Mtoa mada anahoja ya msingi!
 
Hatuzuii malalamiko bali yawe na taarifa kamili ili tujue ukweli halisi
 
Shirika linaloongoza kwa rushwa halafu kuna mtu anasema mimi rais wa wanyonge!!!!
Daah...! Hujafikia hata nusu ya uchunguzi wako. Yaani Tanesco waongoze kwa rushwa?. Unamaanisha wawe mbele ya T.R.A,POLISI TRAFKI,POLISI,TUKUKURA,MAHAKAMA?
 
Back
Top Bottom