Tanesco arusha: Mtaua!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
Unapoingia kwenye geti la Hospitali ya Mount Meru, mkono wa kulia kuna Transfoma ya Tanesco, ambayo iko katika njia ya waenda kwa miguu.

Jana nikiwa natoka ofisini kwangu, niliona kwa mbele yangu Mdada mmoja akipiga makelele na kurukaruka huku akiwa amenaswa kwenye waya unao'support Transfoma hiyo.

Mara wakawa wamekusanyika watu wengi sana kumsaidia dada huyo, lakini kwa bahati nzuri alifanikiwa kujitoa, lakini alikumbwa na mshituko mbaya sana kiasi alikuwa akihema na kutoa jasho jingi.

Katika maelezo yake anasema kuwa akiwa anapita eneo hilo alishikilia waya hiyo, ambayo ni ya ku'support transfoma, (ni zile zinazoshikilia nguzo, na kisha kuchimbiwa ardhini) na katika hali ya kawaida waya hizo hazina umeme, lakini alipigwa shoti ya hatari, na katika mshituko sandal yake moja ikavuka, na ndo hali ikawa mbaya, akawa amenga'ng'ania hapo akishindwa kujitoa, huku akirushwarushwa!

Watu waliokusanyika wanasema kwamba hali hiyo imeshawahi kujitokeza tena mara kadha mahali hapo, na waliripoti Tanesco, lakini hakuna kilichofanyika.

Nami kwakuwa nilikuwa na namba ya simu ya Meneja nikaamua bila kujiuliza kumpigia, ambapo simu yake aliyoitoa kwa Public haikupatikana!.
Lakini nimeweka kwenye ratiba yangu kuwa nitapita hapo ofisini kwao muda wowote kuwaeleza juu ya hatari hiyo.

Tafadhali Staff wa Tanesco, ondoeni hatari iliyopo eneo hilo, maana wakati mwingine itakuwa ni kilio na majuto.
 
Watu waliokusanyika wanasema kwamba hali hiyo imeshawahi kujitokeza tena mara kadha mahali hapo, na waliripoti Tanesco, lakini hakuna kilichofanyika.
Mpaka wafe watu kama watano hivi ndio mamlaka husika itakaposhtuka.
 
they are never proactive....hata inapokuja kwenye suala muhimu kama maisha ya watu
tufanye nini eti bht
tuandamane?
tususe?
tuwadunde?
tulie?
tunyamze?
tusikitike?
Au tuwaache wafanye watakavyo?

Naomba jibu pls
 
Tanesco wana kitengo chao cha dharura ama emergency na ndio kazi yao masaa 24/7. Sema sasa jamaa nao hawako makini wakipewa taarifa. Na inawezekana walishapewa taarifa wakazikalia nina uhakika.
 
Tanesco wana kitengo chao cha dharura ama emergency na ndio kazi yao masaa 24/7. Sema sasa jamaa nao hawako makini wakipewa taarifa. Na inawezekana walishapewa taarifa wakazikalia nina uhakika.
hii kawaida sana hapa bongo, wenyewe wanasema fanya follow up mwenyewe mwenye tatizo otherwise itakula kwako
 
hii kawaida sana hapa bongo, wenyewe wanasema fanya follow up mwenyewe mwenye tatizo otherwise itakula kwako

Kinachosikitisha zaidi, huyu mama Hiza ambaye ni Meneja wa Pale ametoa namba kwa Public ambayo inatakiwa kuwa hewani muda wote, lakini ni ajabu sana humpati ukimpigia, sijui ni uwajibikaji wa wapi!
Na tatizo la watu wa Emergency nao ukipiga simu utaambiwa ..oohh wako Masai kempu...wako Ikiding'a, maeneo ambayo ni mbali mno na mji...
Lakini Tuombe Mungu....
 
tufanye nini eti bht
tuandamane?
tususe?
tuwadunde?
tulie?
tunyamze?
tusikitike?
Au tuwaache wafanye watakavyo?

Naomba jibu pls

Tuwa dunde au tuandamane itakuwa yote bora kwani wanakiburi sana na majigambo, kwani utekelezaji wao wa kazi huwa ni wamuda mrefu na ukiuchunguza haunaga mpangilio yani waweza kuta kaaanzia juu mara karudi chini mara yuko kati Honestly they dont have proper procedure plan
 
tufanye nini eti bht
tuandamane?
tususe?
tuwadunde?
tulie?
tunyamze?
tusikitike?
Au tuwaache wafanye watakavyo?

Naomba jibu pls

Sipo tuwadunde....aiseee wananiudhi!!!!!!! tuwachape salala migongo iwe ka imechorwa tatoo
 
Kinachosikitisha zaidi, huyu mama Hiza ambaye ni Meneja wa Pale ametoa namba kwa Public ambayo inatakiwa kuwa hewani muda wote, lakini ni ajabu sana humpati ukimpigia, sijui ni uwajibikaji wa wapi!
Na tatizo la watu wa Emergency nao ukipiga simu utaambiwa ..oohh wako Masai kempu...wako Ikiding'a, maeneo ambayo ni mbali mno na mji...
Lakini Tuombe Mungu....

Masai kempu wapi weewe....wanakuwa pale kwa mama seberee pale ilboru kuna gongo kali hamna mchezo, muulize Xpin
 
Kinachosikitisha zaidi, huyu mama Hiza ambaye ni Meneja wa Pale ametoa namba kwa Public ambayo inatakiwa kuwa hewani muda wote, lakini ni ajabu sana humpati ukimpigia, sijui ni uwajibikaji wa wapi!
Na tatizo la watu wa Emergency nao ukipiga simu utaambiwa ..oohh wako Masai kempu...wako Ikiding'a, maeneo ambayo ni mbali mno na mji...
Lakini Tuombe Mungu....

Nasikia Tansco ya hapo A town ni kiboko ati ukipiga simu Emergency wanakujibu nguzo imeanguka mahali fulani na haswa kile kipindi cha mgao ndio ilikuwa komesha mbaya wanajibu tu ilimradi umejibiwa ati order imetoka Dar bro wangu alikuwa akitusimulia nakjua kweli Hili shirika lian shida sana na ninavyojuwa watu wa Arusha wanavyo penda pesa mbele kwanza mhhhh poleni sana,

Nasikia hata Hapo Mt.Meru Hospita hawana tofahuni na Mwananyamara Hostpl huko Dar Huduma ni mbovu usipime wanawake wajawazito wanapoteza watoto mara kwa mara na madaktari ati wanajibu huwa ni kwaida mtoto kufia tumboni mwa mama yake na hawakupi reason why that happen na kuna madoctr specialist wa kina mama!!! Jamani poleni sana ila 2010 ndi mabadiliko yaja chagueni vijana hapo A town ndio awe mbunge wenu hao wazeeee wanalindana sana

Mambo ya MtMeru Hosp nitakuleteeni thread yake...Ni soo!
Kweli Pesa imewekwa mbele sana hapa Atown, sijui ni maisha ya huku yanalazimisah...!
Enewei...muda unaruhusu...ndo kama hivi tunachapchapa mdogomdogo, wenye masikio ya kusikia wanasikia!
 
Tuwa dunde au tuandamane itakuwa yote bora kwani wanakiburi sana na majigambo, kwani utekelezaji wao wa kazi huwa ni wamuda mrefu na ukiuchunguza haunaga mpangilio yani waweza kuta kaaanzia juu mara karudi chini mara yuko kati Honestly they dont have proper procedure plan
Nimekudondoshea SENKS kwa jibu zuri na moyo wa ujasiri jethro
Rudi pale na wewe udondoshe moja Mkuu
 
Mambo ya MtMeru Hosp nitakuleteeni thread yake...Ni soo!
Kweli Pesa imewekwa mbele sana hapa Atown, sijui ni maisha ya huku yanalazimisah...!
Enewei...muda unaruhusu...ndo kama hivi tunachapchapa mdogomdogo, wenye masikio ya kusikia wanasikia!

Nakukumbushia usije sahau kutumwagia hiyo Thread ya Mt. Meru Hospital.

Duuh Sasa kama pesa ndio Kipaumbele basi kuna gap kubwa sana kati mtu wa kipato cha juu na yule wa kipato cha chini, kodi ya nyumba sijui hapo ikoje, usalama wa rai na utakuwa ni wakusua sua sua kutokana na uchumi ulivyo sasa na nasikia matukio ya kuvamia bar nayo huko yapamba moto siju Huyo RPC wa hapo kazi yake ni nini?
Hebu tudondoshee iyo thread one day maaana twapata tu habari toka Dar tuuuuuuuu, je Huko Mwanza hakuna mwana JF tusikie kunini??Maana Nako Rock City Ujambazi umerudi nakumbuka enziii ya 1980's mzee wangu alikuwa serikalini kulikuwa na ujambazi mkali ukiongozwa na Jambazi anaitwa Nyamuhanga na akauwawa mchana peeeeee nakumbuka RPC was David Maji. since then it was safety place but recently nasikia kumekuwa ni soooooo, uyo RPS naye kazi imemshinda

Back
Top Bottom