Tandale Kwa Mtogole

Tandale Kwa Mtogole

Keykey

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2006
Posts
3,251
Reaction score
750
Mtogole.jpg

This is life for this resident of Tandale kwa Mtogole in Kinondoni, Dar es Salaam, as he rests outside his house surrounded by perennial sewage discharged from neighbouring houses. The picture is similar in most residences in the area, with few signs that the situation will improve any time soon.

Picha kwa hisani ya IPPMedia
 
Haya ndo maisha bora kwa kila mtanzania heri yangu sijasema.
 
Mtogole.jpg

This is life for this resident of Tandale kwa Mtogole in Kinondoni, Dar es Salaam, as he rests outside his house surrounded by perennial sewage discharged from neighbouring houses. The picture is similar in most residences in the area, with few signs that the situation will improve any time soon.

Picha kwa hisani ya IPPMedia

hili eneo kama sikosei lipo kiondoni sehemu ambayo inasemekana kila mtu anayematter dar es salaam anatoka. Angalia alivyokaa, mawazo kibao, jinsi anavyofikiria next move mwenyekiti wa kitongoji, then mtaa, then diwani, then mbunge, then waziri then....

Kila kiongozi anatoka kinondoni kutokana na mawazo kama aliyonayo mtanzania huyu. Watanzania wengine wana matatizo ila hawafikirii sana jinsi ya kuyasolve kama watu wa kinondoni.
 
hii ni baada ya miaka karibu 50 ya Uhuru! Na viongozi wanapata usingizi usiku? Shame on! kwani laana mwajiletea wenyewe. Kaangalieni kale ka binti kwa pembeni mbali kidogo, je maisha yake yatakuwaje? Pia nawahakikishia kuwa huyo bwana wala si mkubwa sana kwa umri, bali ni mazingira na mkabala wa dhiki unaomkabili unamzeesha mapema. Je, kipindupindu, maleria et al vitatokomezwa nchini?
 
Mwashangaa haya nendeni India tena New Delhi muone.
 
all in all lakini wananchi hatupaswi kuacha kufikili na kutatua matatizo yetu. jamani kila kitu serikali? hivi huo hapo si uchafu jamani? nimeona mitaa mingi ni michafu kupita kiasi na watu hawataki kufanya usafi ni kulalama tu. jamani tubadilike kifikra. kuacha uchafu namna hiyo kunaathiri sana afya zetu
 
hili eneo kama sikosei lipo kiondoni sehemu ambayo inasemekana kila mtu anayematter dar es salaam anatoka. Angalia alivyokaa, mawazo kibao, jinsi anavyofikiria next move mwenyekiti wa kitongoji, then mtaa, then diwani, then mbunge, then waziri then....

Kila kiongozi anatoka kinondoni kutokana na mawazo kama aliyonayo mtanzania huyu. Watanzania wengine wana matatizo ila hawafikirii sana jinsi ya kuyasolve kama watu wa kinondoni.

Hili ni eneo kabla hujafika kwa "Tumbo" ambako ukitaka kufahamu umefika utapokelewa na harufu kali ya mtaro.Kifupi Dar es salaam ni mji ambao haukuwa planned kwa maeneo yake mengi, hiki ndio kinasababisha watu kujenga kwenye maeneo yasiyostahili
 
all in all lakini wananchi hatupaswi kuacha kufikili na kutatua matatizo yetu. jamani kila kitu serikali? hivi huo hapo si uchafu jamani? nimeona mitaa mingi ni michafu kupita kiasi na watu hawataki kufanya usafi ni kulalama tu. jamani tubadilike kifikra. kuacha uchafu namna hiyo kunaathiri sana afya zetu

Hata kama utawalaumu wananchi kwa kutofanya usafi mazingira yao lakini ukweli unabaki palepale kuwa unaitaji miundombinu inayokidhi ili nawe huo uchafu utakaosafisha uweze kuwekwa mahala panapositahili.
 
Baadhi yetu watabisha na kukataa kwamba labda hali haiko hivyo lakini wale wanaokaa 'USWAZI' Dar es Salaam wtakubaliana na mimi kuwa Tandale kwa Mtogole inawakilisha maeneo mengi ya miji yetu ambako hali ya usafi ni msamiati usiojulikana

3233304341_519bd494fc.jpg

20090626_Tandale.jpg

3233303465_a521391677.jpg

3233303875_7576f330b6.jpg

3233304175_f41048acb3.jpg
 
Hv kumbe ukombozi wa inji hii uko mbali kiasi hiki....!
Mungu saidia!
 
Magezi, mtizamo wako tofauti kweli. Kwa kuwa India wana hali mbaya zaidi kama unavyoelekea kudai, basi tusijali ya kwetu! Na kura nyingi za CCM zinatoka maeneo haya, maajabu.

Hivi kweli, ni ghrama kubwa kiasi gani kuboresha maisha ya huyu wa Mtogole; jamani hata nguvu kazi (labour only) tusingeweza tukarekebisha hayo maji machafu yakapita haraka zaidi na kando kando tukaweka uoto wa majani ukawa kama bustani! Mengine ni ule utaratibu wa kusubiri serikali ije ilete maisha bora....na hapa ndio maaana napenda ule ujumbe mzito wa waraka wa Katoliki ; TUSISUBIRI AJE MWINGINE AU SERIKALI atuletee maendeleo
 
wengine ni uzembe tu wa kufanya usafi. sasa huyu anasubiri diwanni aje,
watanzania wenge hatuna ile spirit ya uwajibikaji hata kidogo,
lipo huyu jamaa anasubiri serikali iingilie kati
 
Ni mfumo mbovu wa mipango miji ambao unakwamisha maji taka kuweza kuondoka kwenye hayo maeneo na kupunguza hatari ya magonjwa ya milipuko!
 
Mabwana afya wapo? kwingine wanapiga fine.. Lakini yote kwa yote ... hakuna mtandao wa kueleweka wa maji machafu Dar
 
Heee eeee kazi ipo na wananchi nao wanasemaje maana wao ndio wadau wakubwa na waathirika,mbona kama wameridhika vile,walonge na mabwana na bibi afya wako wapi waache kuzunguka na viti vya wachina maofisini
 
Katika wilaya 3 za Dar es salaam inawezekana Kinondoni ndio inaongoza kwa uchafu.Halafu hii tabia ya uchafu inaambukiza.Ukikaa kwenye mtaa wa watu wachafu kuna uwezekano mkubwa na wewe utakuwa unachukulia kila kitu hivyohivyo.Mambo mengine hata hayahitaji serikali,hii ni tabia yetu watanzania wengi.
 
Duh! mbunge wa kinondoni anafanya nini sasa? Alafu hapo kwa mtogole ndio kunasifika kwa vibaka,sasa vijana hao wafanye nini kama wametengwa kiasi hiki? Maisha bora wanayoyasema yako wapi?
 
Back
Top Bottom