Tamko rasmi la Ray kifo cha Kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko rasmi la Ray kifo cha Kanumba

Discussion in 'Entertainment' started by KIM KARDASH, Apr 25, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba.

  Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.

  Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.

  Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu' bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya.

  Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.

  Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu.

  Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1[SUP]st[/SUP] Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote.

  Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu, Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.

  Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.

  Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.

  Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.


  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA PEPONI
  MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kwa hili andiko naweza kusema Ray ameanza kupevuka, na amefanya kitu sahihi kwa mda sahihi.
  Naipongeza timu yake ya ushauri na wote walioshiriki kumuandikia huo waraka!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Aaache kuweweseka...ne yeye
  hahusiki basi anyamaze
   
 4. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kwan ye hawezi kuandika mwenyewe?
   
 5. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Kwan ye hawezi kuandika mwenyewe?
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Ndiyo shida ya wasanii wetu hapa Nchini
  Ni mpaka aunganishiwe silabi!
  Ila nina shaka bado tutasikia mengi kuhusu kifo ya S . K
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  huyu ndiye kamuua kanumba ..kama sio yeye anaandika andika vutu gani
   
 8. R

  RON PAUL Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 45
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yah ni kweli umeongea vizuri sana hana sababu ya kutapa tapa,yeye akae kimya aache uchunguzi uendelee ukweli utajulikana.
   
 9. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ray hana kichwa cha kuandika maandishi haya, kaandikiwa tu sijui kalipia au ni bure. ila msimbane sana Kanumba S, muda wake wa kuishi ulishapita hivyo Ray muda wake bado mwacheni astarehe msimsingizie mtu unless mna ushahidi.
   
 10. A

  Apta Kayla JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikuwa MTU WA TATU KUJULISHWA...?
  Hii sentensi tata. Alijuaje kama yeye alikuwa wa tatu? Wa tatu kujulishwa na nani? Alipata wapi wazo la kumuuliza aliyemjulisha kama yeye ni mtu wa ngapi kujulishwa?
   
 11. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  RIP Kanumba. Ray, sio kila kitu unatakiwa kukijibu maana unaweza kujikuta unaisaidia polisi kwa maneno ya kujichanganya. Kama hukuhusika kaa kimya...time will prove you right or wrong.
   
 12. M

  MOSHIZZLE Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  jamani mbona mnamdharau sana jamaa kana kwamba wengi mlio humu mko sahihi kwa kila jambo? Kinachostaili angalieni alicho andika bila kuweka hofu yoyote maana hata yeye anahaki na uwezo wakuandika alicho andika. Swala la yeye kujitetea ni muhimu kutokana na shinikizo la maneno ya watu yasemwayo na yaandikwayo kwenye sehemu mbali mbali za habari za udaku na kuaminika.
  Tusizoee kubeza kila jambo tumisikilizeni then kama hatuna haki ya kumuondolea haki yake basi tumuombee mungu watu wasimchukuie vibaya ila afanye ukweli kuharakishwa na kuwezesha haki kutendeka, maana mungu ashindwi kitu. Quote ya mwisho ya ray ni muhimu sana kwa kila mtu kufikiria. Nawasilisha
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ngoja niwaache wafu wazike wafu wao
   
 14. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,089
  Trophy Points: 280
  Pole bro! Huu nao ni U PEPO! Utapita tu!
   
 15. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,824
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuthibitisha haya unayoyasema beyond doubts?!! jamani acheni kuzusha mambo msiyona uhakika nayo...
   
 16. Fekifeki

  Fekifeki JF-Expert Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,163
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimeipenda hii!
   
 17. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,229
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Sidhan kama ray kuandika waraka kama huu ni kuweweseka, nadhani unatambua kuwa kila mtu anajengwa na hisia ambapo hisia zinapozidi hupelekea kufanya kitu fulani au kuamua kufanya jambo fulani. Nadhani Ray amekaa ameona jinsi jamii inavyopotoshwa na kili kinachosemwa tena kukuzwa na baadhi ya vyombo vya habari na kuamua kutolea ufafanuzi.

  Anahaki ya kufanya hivyo na pia ni wajibu wake kuielezea jamii ukweli wa jambo fulani ambalo yeye anatuhumiwa kama muhusika.
   
 18. N

  Ntuya Senior Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ray vs Kanumba(RIP)
   
 19. Deejay nasmile

  Deejay nasmile JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,916
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280

  Deejay nasmile likes your comment
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Lol! Kwani tamko la kukanusha jambo ndo lina prove kuhusika au kutohusika?! Hayo ni maneno tu hata kwenye t-shirt yapo!
  BTW hata kama ni kweli hawezi kukiri,atajua mwenyewe na Mungu wake..
   
Loading...