Tamko la UVCCM mkoa wa Arusha kuhusu Lowassa

amina ngalo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
309
170
TAMKO KUTOKA UVCCM MKOA WA ARUSHA.

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Arusha umeshtushwa nakufadhaishwa na kauli ya aliyekua mgombea wa urais kwa tiketi ya Ukawa Ndg Edward Lowasa kwamba Chama Cha Mapinduzi ni cha msimu na kwamba kimejaribu kununua madiwani wa upinzani kwa Tsh million 20.
Kama Umoja wa Vijana tulidhani Ndg Lowasa aliposhindwa kwenye uchaguzi mkuu angetekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kwenda kuchunga mifugo yake na kuacha kuendeleza maigizo aliyoyaanzisha ya kuendelea kuwalaghai na kuwachonganisha chama cha Mapinduzi na wananchi wake ambao nao
wameshazielewa hila zake.
Ndg Lowasa anasema CCM ni ya wezi n wanyanganyi na kwamba watanzania wote wanajua yeye ndiye mshindi wa uchaguzi mkuu. Tunamshukuru sana kutukumbusha alivyoasisi genge la kidhalimu ndani ya CCM, tunakiri kwamba chama hiki ni kweli kilikua kiwe cha msimu na kisingeaminika kabisa, hii ni kutokana na uwepo wake na kikundi hicho kilichodhamiri kugeuza taifa hili kuwa pango la walanguzi.

Ambacho Ndg Lowasa amesahau kuwaambia wananchi wa monduli ni kwamba alishapiga dili na walanguzi wenzake kuondoka ndani ya Chama hiki tukufu July mwaka jana, na kwamba wachache waliobaki tutaendelea kuwasafisha na kuwatupa kwenye dampo letu linaloitwa Ukawa ili kurejesha utakatifu wa Cham hiki.

Ndg Lowasa Umoja wa Vijana wa Arusha unakutaka urudi kijiji cha Ngarash mara moja ukachunge mifugo yako umuache mteule wa Mungu aliyepewa dhamana na watanzania wote kutufikisha katika nchi ya neema Mhe.John Pombe Magufuli aendelee kufanya vitu vyake.

Ni heshima mbele za Mungu kumpa mtu anachostahili, na kwa Ndg Lowasa alifanikiwa kupasua CCM lakini Mungu akawa upande wetu, aligawa vijana Mungu pia akasimama na alijaribu kuaminisha watanzania kuwa pesa ndio kila kitu jambo ambalo ameshuhudia aliposhindwa na kama kuna jambo anastahili nalo pongezi ni hiyo hulka ya kuwagawa watanzania.

UVCCM mkoa wa Arusha inawaaminisha na tunasema kam Ndg Lowasa ataendelea na harakati zake za kuikejeli serikali hii hatutamvumilia kamwe.
Imetolewa na Umoja Wa Vijana CCM mkoa wa Arusha....... Imetolewa na COMRED MUNISI MWKT UVCCM MKOA
 
Teh,teh UVCCM Arusha,mbona CCM ilishafutwa Arusha?huyu munisi si ndo yule mchumia tumbo anayeshirikiana na jambazi maarufu anayefahamika kwa jina la mjusi anayejificha chini ya kivuli cha UVCCM amemaliza roho za wahindi Arusha
 
Nasikia huko Arusha hakuna upinzani wowote kwenye chaguzi za ndani. Watu hupeana tu vyeo kwa sababu ya uchache wa wanachama. Nasikia wanachama wa CCM hapo Arusha Mjini hamzidi 20, sasa haya matamko ya kazi gani?
 
Nasikia huko Arusha hakuna upinzani wowote kwenye chaguzi za ndani. Watu hupeana tu vyeo kwa sababu ya uchache wa wanachama. Nasikia wanachama wa CCM hapo Arusha Mjini hamzidi 20, sasa haya matamko ya kazi gani?
Arusha Magufuli alipata kura zaidi ya elfu 65
 
Nasikia huko Arusha hakuna upinzani wowote kwenye chaguzi za ndani. Watu hupeana tu vyeo kwa sababu ya uchache wa wanachama. Nasikia wanachama wa CCM hapo Arusha Mjini hamzidi 20, sasa haya matamko ya kazi gani?
hujasikia pia lowasa ameanza kampeni 2020 chadema imeshaa mteua ??

nasikia mtamsafisha fisadi mwingine
nasikia ruzuku kuna milioni miambili inasaini na kuwekwa kwenye AC maalumu mtu akihoji Mbowe anamwambia achakazi
nasikia Mnyika kakaataa kabisa kufanyakazi nayule ambaye kwamiaka nane mlimwita fisadi kwa miezi miwili mkataka kumsafisha ikashindikana
 
Ndiyo tamko gani hilo sasa? Hilo ni tamko au hisia? Hivi viongozi wa CCM mkoa wa Arusha walishapatikana wengine baada ya wale wa awali wote kujivua gamba?
 
Teh,teh uvccm arusha,mbona ccm ilishafutwa arusha?huyu munisi si ndo yule mchumia tumbo anayeshirikiana na jambazi maarufu anayefahamika kwa jina la mjusi anayejificha chini ya kivuli cha uvccm amemaliza roho za wahindi arusha
ulifuta ww ??
 
Polen sasa UVCCM Arusha labda nikukumbushe kitu. Monabani tulimvuruga vibaya alafu tukamzima sasa hivi anauza unga na mafuta alafu hapa Arusha CCM iliisha futwa siku nyingi sana. Sisi vijana wa Arusha. Tunajitambua sana atushawishiki kwa kukamua majibu sisi ni makamanda atuangalii nyuma
 
Back
Top Bottom