Tamko la UKAWA baada ya Naibu Spika kutangaza kukata posho

Zitto kabwe hachukui posho na haijamzuia kufanya kazi za kibunge kwa uzalendo wa juu. Kama mbunge una msimamo thabiti huwezi kuuacha kwa sababu ya posho. Mshahara wa mbunge unatosha kumweka Dodoma bila athari zozote. Hakuna Mbunge anakaa guest kusema itamsumbua. Mageuzi katika mfumo wowote yana gharama zake ikiwemo la kukosa posho. UKAWA msirudi nyuma. Majitoleo yenu huwezi kulinganisha na CUF kule Zanzibar. Wawakilishi wa CUF-ZnZ walitumia gharama kubwa katika kampeini 2015 lakini wameachia kila kitu! Ni wenye akili ndogo wanadhani fedha ni kila kitu. Dr. Tulia inabidi ajitafakari. Wamepita ma-spika wangani mbona upinzani haujawai kumkataa yoyote isipokuwa yeye? Ni bahati mbaya tulio nje hatuoni nini kinaendelea mle ndani. Hoja za kumtetea za kina Prof. Tibaijuka eti kwa vile ni mwanamke ni mufilisi. Wacha koleo iiitwe koleo na sio kijiko kidogo!!
 
Lazima watarudi...chezea posho weye?
wewe ndio unapenda posho au bado ni kijana wa miaka ya 90 kama sio 1988.

Hujasoma hata bandiko, akili umeweka kwenye WhatsApp, hujui hata bunge la katiba ni nini....kichwa nazi...
 
Mbunge anasaini kuingia ndani ya bunge asubuhi halafu anaondoka kwenda site kusimamia ujenzi wake. Halafu jioni anarudi kusaini kuchukua posho kuendeleza shughuli za ujenzi for next day! Only in Tanzania.

Kama hamjali kaeni kimya. Tuendelee na binge tunaoona sawa hakuna hitilafu
 
Nyie endeleeni kuchonga na kuwananga wabunge wazalendo wa upinzani kwa kigezo cha uchache wao ambapo kunahalalisha ubabe ,kedi,umajinuni unaokaribia uhabithi na unabaradhuli kwa wabunge wa CCM .Majority ya wananchi tunawaangalia tu na kuwafuatilia kwa jicho la subra tukisubiri wakti muafaka kuwashughulikia ipasavyo kwa namna mujarab kabisa ambapo itatoa funzo kwa hayawani wa baadae!
Malofa na wajinga in waiting!
Mkuu 124 Ali kama umenimisquote vile
 
Mkuu umenifurahisha sana
Inaonekana somo la geograph ulifaulu sana kwenye topic ya photograph
Hahhaah alikua anatufundisha Dada mmoja anaitwa Miss Mbaga alikua na aibu balaa maana ile shule ilikua no Boys tupu na Dada alikua fresh from College hahaahahhaa Magamba Secondary hio, tunasoma Jiografia pamoja na "jiografia"
 
Bado sijaelewa vyema ni faida gani inapatikana kwa kususia vikao,maana tunaweza kuona ujinga kumbe ipo faida itokanayo na huo ila kama hamna faida sioni umuhimu wa kufAnya hivyoo!


Hivi hujui faida ya kususia? Faida ni nyingi kwa mfano kwanza inakuwa ajenda ya mazungumzo ili asiye na sauti asikike pia, na nyingine nyingi zaidi
 
Hahahaha inafurahisha sana. Posho watakosa na maana yake watahesabika watoro bungeni. Na kibaya ukiangalia wanachogomea ni upumbavu mtupu! Hivi kuna kitu gani cha maana wanachogomea??? Miongozo ?? au??
Akili ya Lumumba bwana. Sasa kama hujui nn kinaendelea mbona unarukia mada?? Kanawe uje...
 
Itakuwa jambo la maana hii posho iakkusanywa na kulipia ada wanafunzi wa udom waliondolewa mkopo.
 
Ili kuonyesha ukawa ni ngangari wasusie kabisa bunge waondoke warudi majimboni, ila hii ya kuvizia spika anaingia wanatoka mbio kama wamebanwa mkojo haina tija.
 
Upinzani Tanzania ni kutoa matusi, kashfa, dharau kwa serikali badala ya kutoa hoja na sera mbadala kwa ajiri ya maendeleo. Kweli wanasiasa wa Africa walishalaaniwa na MUNGU ndiyo hamna maendeleo.

Wabunge wanalipwa posho na mishahara mbali na biashara zao. Vijana wasiojitambua wanaacha biashara zao zinazowaingia kipayo, wanahamasishwa waandamane na kufanya vurugu, halafu wanalaumu serikali kwa maisha magumu.
 
Bado sijaelewa vyema ni faida gani inapatikana kwa kususia vikao,maana tunaweza kuona ujinga kumbe ipo faida itokanayo na huo ila kama hamna faida sioni umuhimu wa kufAnya hivyoo!
Kususia ni njia moja wapo kati ya zilizopo za kulazimisha haki itendeke,mambo yenye maslahi kwa taifa yakubaliwe pale yanapotoka upinzani,dhuluma na unyanyasaji wa kuzuia taarifa muhimu kwa wapiga kura na WALIPA KODI zikome.
Kama ingekuwa ni baba au mzazi kwa manawe ingekuwa ni kumuadibisha spika,kumkemea na kumkosoa.
 
TAMKO LA WABUNGE WA UKAWA DHIDI YA UAMUZI WA NAIBU SPIKA KUWAKATA POSHO.

Kuwa mpinzani katika nchi za Afrika kunahitaji moyo sana wa uvumilivu na kujitoa mhanga wakati mwingine!!

Azimio la bunge la kuzuia wabunge wa UKAWA kulipwa posho halitabadili msimamo wetu mana tulifanya hivyo ktk bunge Maalumu la Katiba kwa kuacha malipo ya milioni 30 hivyo basi hili si geni kwetu.

Tutasimama imara mpaka dakika ya mwisho kupinga udhalimu unaofanywa na naibu spika katika kuendesha bunge kidikteta dhidi ya upinzani.

Silinde Ernest David(Mb)
Jimbo la Momba
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni - wizara ya Fedha na Mipango.
08.06.2016
Dodoma, Tanzania.
MTARUDI TU. NJAA SIYO MCHEZO. MNGEKUWA WAZALENDO MNGETOA POSHO ZENU ZITENGENEZE MADAWATI
 
Kususia ni njia moja wapo kati ya zilizopo za kulazimisha haki itendeke,mambo yenye maslahi kwa taifa yakubaliwe pale yanapotoka upinzani,dhuluma na unyanyasaji wa kuzuia taarifa muhimu kwa wapiga kura na WALIPA KODI zikome.
Kama ingekuwa ni baba au mzazi kwa manawe ingekuwa ni kumuadibisha spika,kumkemea na kumkosoa.
Asante kwa ufafanuzi tuombe kunachotafutwa kitendewe haki
 
Back
Top Bottom