Tamko la serikali kuhusu mauaji Tarime? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la serikali kuhusu mauaji Tarime?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 27, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Polisi wadaiwa kuchoma 'majeneza' ya Chadema  SAKATA la mauaji ya wananchi wanne katika mgodi wa Nyamongo uliopo Tarime, mkoani Mara umechukua sura mpya baada ya ndugu wawili wa marehemu kudai kuwa polisi waliwapiga na kuwalazimisha kuyachoma majeneza waliyonunuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya mazishi.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa ndugu hao walipigwa ili wayachome majeneza hayo na kuyatumia yale yaliyonunuliwa na kukabidhiwa kwao na polisi.Mkono Bhoke ambaye ni kaka wa marehemu Chawali Bhoke, alisema tukio hilo lilitokea juzi baada ya kusimamishwa na askari polisi wakiwa njiani na majeneza hayo kuwahi mazishi.

  Katika mkasa huo, Mkono alisema polisi wakiwa na bunduki, waliwalazimisha wanandugu hao kuyamwagia petroli majeneza hayo mawili na kuyateketeza kwa moto.Kama hiyo haitoshi, Mkono alidai polisi hao waliwapiga na kuwaweka mahabusu kwa muda jambo lililowafanya washindwe kuhudhuria mazishi ya ndugu zao.

  Mkono aliongeza kuwa alikutwa na mkasa huo akiwa na ndugu wa marehemu Mwikabwe Mwita, mkazi wa Kijiji cha Kitunguruma."Kutokana na kadhia hiyo, ilibidi wanandugu kutumia majeneza ya polisi kuzika marehemu wao," alisema Mkono.

  Hata hivyo, habari zingine zimeeleza kuwa wakati ndugu hao wakilazimishwa kutumia majeneza ya polisi kuwazika ndugu zao, ndugu wa marehemu Chacha Ngoka wa Kijiji cha Kewenja na Emmanuel Magige walizikwa kwa kutumia majeneza ya Chadema.Kwa mujibu wa habari hizo, ndugu hao jana walikuwa kwenye mikakakti ya namna ya kuwarejeshea polisi majeneza hayo, huku wakijua kwamba wenzao walikumbwa na kipigo.

  RPC Boaz asema
  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz alipoulizwa kuhusu matukio hayo, alisema haamini kama polisi wanaweza kufanya jambo hilo, ila akaahidi kufuatilia kwa karibu kujua kilichotokea

  "Sikuwapo kazini, ila pia siamini kama polisi wamefanya hivyo. Nitafuatilia kwa karibu nijue kilichotokea," alisema
  Taarifa zilizozagaa mjini Tarime zinaeleza kwamba polisi walitibua kwa makusudi mpango wa Chadema wa kufanya mkutano wa pamoja na ndugu wa marehemu siku ya mazishi kabla ya taratibu za maziko.

  Juzi, wanachama kadhaa wa Chadema, Tundu Lisu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki na wenzake saba walifikishwa mahakamani kwa shtaka la uchochezi.

  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho, Matena Mwikwabe alidai kuwa wananchi wamekosa imani na Serikali ya CCM kutokana mfululizo wa matukio tangu ndugu zao walipouawa.Diwani wa Kata ya Kibasuka, Suleimani Moya (CCM), alikiri kufika kwenye msiba wa Emmanuel Magige na kueleza kuwa hali kwa wapiga kura wake siyo nzuri na kuvilalamikia vyombo vya dola.

  "Mimi ni diwani wa CCM, lakini kwenye ukweli nalazimika kuusema. Vifo vya watu hawa lazima halmashauri tutoe tamko, maana wanaokufa niwapiga kura wetu, kisha zinatolewa lugha zisizo nzuri,"alilalamika.

  Katika hali ya kutafuta suluhu kati ya wananchi, mgodi na polisi, kesho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wassira amepanga kukutana na viongozi wa vijiji vya Kewanja, Nyangoto, Matongo, Genkuru, Nyamwaga, Nyakunguru na Kerende.

  Baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo walilithibitishia gazeti hili lakini wakasisistiza haki za wananchi lazima zipatikane.
  Baadhi ya wakazi wa hapa wanaeleza kuwa tukio hilo limejenga uhasama baina ya wananchi na polisi ambao ni watu wanaopaswa kuhakikisha kuwapo kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

  Tamko la CUF
  Katika hatua nyingine, Elizabeth Ernest anaripoti kuwa CUF imemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha kujiuzulu kutokana na Jeshi la Polisi kuua raia mgodini.

  Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba alisema hayo jana alipokuwa akisoma maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la chama hicho. Alisema chama kinamtaka waziri huyo ajiuzulu kwa kushindwa kusimamia ukiukwaji wa haki za binadamu kunakofanywa na jeshi hilo.

  "Baraza linalaani vitendo hivyo ambavyo huripotiwa mara kwa mara kama ilivyotokea hivi karibuni katika mgodi wa North Mara. Kutokana na hali hiyo, CUF inamtaka waziri mhusika ambaye ndiye mwenye dhamana ajiuzuru kwa hili la Nyamongo," alisema Prof Lipumba.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Sasa najaribiwa kuamini kuwa jeshi la polisi liko kwenye mkakati wa kumwangusha JK kwa makusudi.
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,046
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Sasa kuna haja kuwaunganisha polisi kwenye uadui na kuanza kudeal nao hardly pale itakapokuwa inapatikana nafasi ya kuwapa kichapo,hawawezi kutuzuia harakati zetu,walaaniwe polisi wote!
   
 4. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi waliouwawa si wanatuhumiwa na polisi kwamba ni wezi/majambazi? Inakuaje tena polisi kama vile wanalazimisha kutoa ushirikiano hadi wa kuchangia majeneza kiasi hicho kwa watuhumiwa hao? Hapa lazima kuna jambo, hata mtoto mdogo analiona hilo ...
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hawataki haki itendeke..nimesikia wamemkamata mmarekani mmoja kwa kosa la kupiga picha zile maiti na kuzituma kwao(marekani)..nikajiuliza kumbe ndiyo maana mpaka leo hatujapata picha za marahemu wa nyamogo..
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Habari za kinafik.
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  umeona ehe? Mapolisi ni wanafiki sana,baada ya adui3 tuna ufisadi na sasa tuna Polisi. Watanzania sasa tuna maadui 5 . Tutapigana nao mmoja mmoja na mmoja baada ya mmoja.
   
 8. Ellyson

  Ellyson JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wewe ni mke wa afande nani kweli vile!!?
   
 9. Ellyson

  Ellyson JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2011
  Joined: Nov 13, 2010
  Messages: 1,717
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  WEWE NI MKE WA AFANDE NANI KWELI VILE!!? Una kiherehere unahitaji dozi!
   
 10. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  kuna mnafiki kushinda wewe?
   
 11. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kama huna cha kuongea kaa kimya, usintafute yatakushinda!
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Wewe au umejisahau?
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135


  Police majangiri majangiri
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Join Date : 9th May 2011
  Posts : 383
  Thanks52Thanked 22 Times in 21 Posts

  Rep Power : 21


  Pole mwitongo
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nakubali ni habari za kinafiki!

  Hakuna unafiki uliotukuka kama kuua "jambazi" kisha ukatoa ubani wa milioni 3, ukanunua jeneza na kisha kusafirisha maiti kwenda mazikoni.
  Huduma ya namna hii hata Osama hakupewa zaidi ya kutupwa baharini wao wanaita kuzika. Azikwe baharini kwani alikuwa baharia alofia melini????

  Hakuna unafiki uliotukuka kama Waziri Wasira kuibuka muda huu kwa kile kinachoitwa kupatanisha. Hapa kuna mtu ameua, kambeba maiti wako kenda mtelekeza barabarani na kawafunga wafiwa. Akifanikiwa kuleta mapatano hiyo kesho wallah mimi ntakuwa mpiga debe wake ili akapatanishe waasi na serikali ya Libya.

  Faiza tusaidiane kupinga unafiki huu
   
 16. R

  Radi Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ungekuwa hata mke wa afande nani hii afadhali,si unajua yule ana mke.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tuletee ambazo siyo za kinafiki..au unahamu na kitimoto
   
 18. g

  gambatoto Senior Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha utoto weweeeeeeeeee:dance:................
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Jina tu linajitukuza....Fox Faiza......................
   
 20. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Wewe ni mke wa rafiki wa fisadi na mdini wa chama cha magamba?
   
Loading...