3. Kwa mfano, tarehe 23 Aprili, 2009, Bwana Reginald Mengi aliandaa Mkutano wa Waandishi wa Habari (Press Conference) ambapo aliyataja makampuni na wafanyabiashara watano wa hapa nchini, akiwamo Mheshimiwa Rostam Aziz, akiwaita kuwa ni "MAFISADI PAPA" na kuwaornba wananchi kuungana nave iIi kupambana na "mafisadi" hao.
8. Aidha, Serikali imebaini kwamba katika malumbano haya kumekuwepo na "matumizi mabaya" ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Bwana Mengi, (televisheni, magazeti na radio), na kwa Mheshimiwa Rostam Aziz, (magazeti). Kila mmoja ametumia vyombo vya habari anavyomiliki kwa manufaa yake binafsi kinyume na maelekezo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003, inayobainisha wazi kwamba:-
• Chombo eha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji bali kitatumiwa kwa manufaa ya umma;
• Chombo eha habari kiongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika; na
• Chombo eha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuehoehea uhasama.
10. Kutokana na hali hiyo basi, Serikali inawataka Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kupitia vyombo vya habari, na badala yake wawasilishe madai na vielelezo vyao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe,na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.
.
12. Aidha, Serikali inawataka Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz kuvitumia vyombo vyao vya habari kwa manufaa ya Wananchi wote wa Tanzania, na si kwa manufaa yao binafsi. Wakumbuke kwamba malumbano yao hayo kwa kutumia vyombo vyao binafsi, na wakati mwingine kuonekana kana kwamba wanalihutubia Taifa, ni kutowatendea haki watu wengine ama kampuni/mashirika ambayo yametajwa katika malumbano hayo, lakini hawana vyombo binafsi (redio, televisheni, rnagazeti) ambavyo wangeweza kuvitumia kujieleza na kujitetea kama walivyofanya Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Azizi.
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.
14. Aidha, Serikali inawatahadharisha Wahar;,.i wa Wanahabari kwa ujurnla kuwa makini katika kutirniza wajibu wao kwa weledi na kuzingalia maadili ya taalurna yao, badala ya kuandika au kutangaza habari kulingana na matakwa ya mmiliki wa chombo kinachohusika.
16. Mwisho, Serikali kwa mara nyingine inasisitiza kwamba mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi bade yanaendelea, na inawahimiza wananchi wote wenye taarifa za vitendo kama hivyo watoe taarifa hizo kwenye vyombo vya dol a vilivyopewa majukumu hayo, iIi hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Sina shaka yale niliyoyasimamia katika majadiliano humu jamvini serikali imeyaona na kuyachukua na kuyafanya kama sehemu ya tamko lake. Kufikiria huko hakuhitaji PhD bali ni uwezo wa kawaida tu wa kufikiri.
Sasa wale mabingwa wa kufabricate na kubadilisha maneno ili wawalishe wachangiaji wengine waendelee kufanya hivyo bila ya kuwa sahau wale wenye user ID zaidi ya moja nao waendelee kujaza threads.
Kwaaaheriii!!!!