Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
Nahisi zamu ya kundi jingine kubwa la Watanzania kuja kujazana ughaibhuni karibu ifike.

Walitanguliza watoto wao kwa fedha ya ufisadi, ufisadi huo huo utawapa free ride kufuata makinda yao hapa Ughaibhuni.

Karibuni sana Waheshimiwa Mafisadi huku Ughaibuni huku hapendwi mtu wala pochi yake linapendwa Box tu.
 
Huu mjadala ushakua kimeo maana watu hawataki kubadilika kabisa. Tunaleana sana bwana, hata kama tumechoka si kihivyo kuna watu humu wanamjua Mengi tu eti kisa ana rangi kama yao....kuna watu maskini hawana hata chembe ya taarifa naye anaingia humu kushindana kihoja. HAWA NDO WANAOPOTEZEA WATU MUDA. Kuanzia sasa nafungu mjadala wangu. Kama kwa siku mbili mfululizo watu wameshindwa kuelewa basi mjadala utakuwa umechanganyika na ushabiki wa mpira tu si bure....tena hao watakuwa lile kundi la ....Asili na ....Kampuni maana pale huwa hakuna SULUHU. Ahsante kwa wale walionielewa na pia kila la kheri kwa wale walioshindwa kunielewa. Looo!!!! Kama tumemeza dawa mseto jamani!
 
:D.......As I have just said... ! I LOVE JForums !! :D :D
 
Udwegile be!( maana yake kusalimu amri kwa ki ilinga)
 
Pole, but you are very right for when the going gets tough, it is only the tough that can prevail. Kama umeshindwa hoja kaa pembeni usianze kuleta viroja - watu tutaendelea kumkoma nyani bila kumtazama sura yake. Fisadi na watetezi wao wote tutawaweka kundi moja na kuhakikisha tumeziba masikio ili vilio vyao visitubabaishe - kamwe hatutakuwa na suluhu nao. Huu ujumbe naomba uwasilishwe kwao kama ulivyo na big up Mengi kwa kutokubabaika katika kumwita fisadi kwa jina lake. I love JF too !!
Kifo kikipiga hodi, miti yote huteleza - ole wenu mafisadi​
 
ina maana ww hufahamu unapoambiwa kuwa kwa mujibu wa sheria chombo chenye mamlaka ya kuamua kama mti mwizi au si mwizi ni mahakama? hapa ndipo alipokesea Mengi, katoa hukumu wakati yeye si mahakama au hata hili ww hulifahamu unafata mkumbo na ushabiki wa mambo tu? siku simtetei RA ila utaratibu uliotumika kumhukumu na bw. Mengi sio unaotumika nchi yetu.
 
Hivi wewe na GT mnalipwa na nani?Ulikunywa maji ya bendera nini?Au na wewe ni wale wale wliotoka tabora kuja maelezo,au mwenzetu unatumia komputa ya RA?Mbona unakuwa mwingi wa kutetea bila kuchambua hoja?Nna hasira ya watu kama nyie mnaotupotezea muda humu ndani kuchangia tapu tapu.Ushaambiwa mkuu wa TaKOKUU alikuwamo RichadMonduli,Yule Felesi ndo wale wale,UWT walimklia RMond,Mkululu kawa Bubu,HIVI WE NANI#%6§
ina maana ww hufahamu unapoambiwa kuwa kwa mujibu wa sheria chombo chenye mamlaka ya kuamua kama mti mwizi au si mwizi ni mahakama? hapa ndipo alipokesea Mengi, katoa hukumu wakati yeye si mahakama au hata hili ww hulifahamu unafata mkumbo na ushabiki wa mambo tu? simtetei RA ila utaratibu uliotumika kumhukumu na bw. Mengi sio unaotumika nchi yetu.
 
Ukweli ni kwamba serikali yetu inafuata sheria pale tu mdogo akifanya kosa.

Mkubwa akifanya kosa au serikali yenyewe ikishindwa kisheria mahakamani hakuna lolote linalofanyika.

Mtikila alishinda kesi Mahakama ya Rufaa mpka leo serikali imeshindwa kutekeleza hukumu hiyo.

Kwa utetezi wako wa kutaka watu wafuate sheria ungetaka wananchiwafanye nini ili serikali itekeleze hukumu ya mahakama ya Rufaa?

Endelea kuamini unacho amini kwa sababu hiyo ni haki yako ya msingi.

Ninacho amini mimi na wenzangu kadhaa hapa jamvini ni ukweli kwamba sheria za nchi zimeainishwa vyema, lakini watendaji wake pamoja na vyombo vyake wanatia mikingamo ya makusudi ili sheria zisiwabane Mapapa wa Uhalifu.

Vipi tukianzisha Mahakama ya Wazi kwa mtindo wa kutajana hadharani
hadi hapo mambo yatakapo rudi kwenye mstari wake????

Swanu eeh!
Naungana na wewe kwa hili, hata aliyoyasema Mangi, ningeyasema kapuku mimi, ningeshaozea Segerea.
Kwenye mjadala huu, mimi pia nasimamia upande wa haki, taratibu na sheria,
Sitetei mafisadi ila alichokifanya Mengi, ni kinyume cha sheria, ila pia serikali ama inamuogopa Mengi kama inavyowaogopa mafisadi, ama inajipanga kimya kimya kumtosa Mengi na kuendelea kukumbatia mafisadi.
Kitu kimoja ambacho ni dhahiri kuhusu Mzee Mengi, ni jasiri wa ukweli mwenye uthubutu wa ajabu ambao hata ikibidi kuvunja sheria za nchi, atazivunja na kwa kusema wazi kile anachokiamini.
Ujasiri wa aina ya Mengi ni sehemu muhimu ya Falsafa ya Ukombozi kwa wanyonge.
Majasiri wa aina ya Mengi, ni aina ile ile ya wale watu watakaosema ukweli daima hata kama at the end, ukweli huo utakuja kuwacost, huu ndio ukombozi wa kweli na ikibidi uwe na mapenzi ya mshumaa ya kumulikia wengine huku yeye akiteketea.
Kwa hakika, mimi ni mmoja wanaoamini kitendo cha Mzee Mengi kuyasema haya aliyoyasema, 'Huu ndio mwanzo wa mwisho wa Mengi'
Nimeiita ni falsafa ya ukombozi ambayo ilianza miaka mingi nyuma, toka enzi za Sodoma na Gomola, Mungu aliuteketeza ule mji kutoikana na uchafu uliokuwa ukifanyika, akamuepusha Lutu mkewe na binti zake wawili ili angalau ulimwengu uendelee, mke wa Lutu aligeuka nyuma na akageuka jiwe la chumvi, Lutu na bintize waliendelea mpaka kufika mahali salama. Pamoja na hasira zote za Mungu, kuhusu uchafu wa Sodoma na Gomola, Mungu huyo huyo aliruhusu uchafu wa wale mabinti wa Lutu, kumlewesha baba yao mzazi na kumlala na wote walishika mimba, Lutu alikufa na kizazi kiliendelea.
Falsafa ya Ukombozi wa Wana wa Israeli toka utumwani Misri, pia ilimuhusisha Musa kujitoa muhanga, kukubali kutokuwa mwana mfalme ili awaokoe ndugu zake lakini matokeo yake, waliishia bkutangatanga jangwani kwa miaka 40 bila Musa kuiona nchi ya ahadi.
Hata falsafa ya ukombozi kwa Wakristu ni kile kitendo cha Masiya kukubali kuteswa na hatimaye kufa msalabani ili "Kwa kupigwa Kwake, sisi tunaponywa"
Ukombozi wa weusi wa kusini, pia ulipitia kwa Mandela kupata kifungo kirefu jela, huko kina Steve Biko, Sisulu na wengine wakitolewa muhanga na kafasi ili hatimaye ukombozi upatikane.
Hii ndivyo ninavyoina ndio dhamira ya Mengi, anataka kuwa kama Lutu, Musa, Mandela na Masiya wa ufisadi wa Tanzania, swali ni will he stand the consequenses?.
Anachofanya kwa sasa ni kupiga kelele to rally the public behind him. Anajifanya anamsaidia Kikwete kwenye vita hivi, huku ukweli he is infact undermining him in front of public eye.
Kuwataja mafisadi papa ni hatua ya kwanza, anatulia kusoma public reaction na kuhimili vishindo na mikiki mikiki ya mahakamani.
Hatua ya pili ni kuidiscredit serikali, kwa kusema publicly, JK ni safi, ila amezungukwa na serikali ya mafisadi ili watu wampende rais wao na kuichukia serikali yake.
Baada ya hapo will be waiting to launch the final blow on JK himself!.
Kitu kinachoniogopeshe ni jee ataachiwa afike kote huko ama atamaliziwa hapo katikati kabla ya safari yake?.
Nimesoma kichwa cha habari mahali kuwa "Mengi ni Mgonjwa", inawezekana baada ya kulijua hili, ameshatambua kuwa his end is near and inevitable, hivyo ameamua kujitoa mhanga kupigania watanzania kwa kujitoa sadaka?.
Kadri siku zinavyokwenda, tutakuja kuijua ajenda halisi ya mzee wetu huyu na kumuunga mkono kwa dhati hata kama anavunja sheria za nchi kwa lengo la kusaidia ukombozi wa kweli wa Mtanzania.
 
1. Sitetei mafisadi ila alichokifanya Mengi, ni kinyume cha sheria,

- Sasa mkuu vipi alichokifanya Makamba kule CC ilikuwa ni sawa kisheria?

- Maana unasema Mengi anayemjibu Makamba amevunja sheria, sijui sheria ipi hiyo mkuu labda tuwekee hapa, au?

FMES!
 
- Tujikumbushe kidogo ripoti ya kamati ya Mwakyembe:-

Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2007 siku ilipowasilisha taarifa yake kwako, Kamati Teule ilikuwa imewahoji jumla ya mashahidi 75 na kuuliza maswali 2717 na kuzipitia nyaraka na kumbukumbu 104. Mashahidi 4 kati ya hao walikuja kwa hiari yao bila kupelekewa hati za kuitwa. Mashahidi 7 waliitwa mara mbili. Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mhe. Rostam Aziz, (Mb) walipelekewa hati za kuitwa mbele ya Kamati Teule lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Ndugu Daniel Yona alitakiwa na Kamati Teule atoe maelezo kuhusu msingi wa uamuzi wake wa kuipa Richmond Development Company LLC, haki maalum ya kipekee (exclusive right) ya miezi 18 kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza mwaka 2004 wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Maelezo ya ziada ya mradi huu nitayatoa baadaye.

Mheshimiwa Spika, vilevile Mhe. Rostam Aziz alitakiwa atoe maelezo kuhusu uhusiano wake na Kampuni za Richmond Development Company LLC na Dowans Holdings S.A baada ya mashahidi kadhaa kudai kuwa ana uhusiano nazo. Aidha, alitakiwa na Kamati Teule aeleze kwa nini anwani ya barua pepe ya kampuni yake ya Caspian Construction Ltd ilitumiwa na Dowans. Kamati Teule ilitaka vilevile kupata ufafanuzi kutoka kwake kuhusu baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake wanaosemekana kuwa ni watumishi vilevile wa Dowans Holdings S.A.

Mheshimiwa Spika, leo tunapowasilisha taarifa hii mbele ya Bunge lako tukufu, tunajisikia kuutua mzigo mzito sana ulioanza kutuelemea kutokana na kuzongwa kila kukicha na kila aina ya uzushi, uchochezi, uchonganishi na hata vitisho. Tumezushiwa kuhongwa magari ya kifahari na fedha taslimu; tumetuhumiwa kuendesha vita dhidi ya Waislamu na mara nyingine tuhuma hiyo ikageuka kuwa vita dhidi ya Wakristo ndani ya Serikali; tumesingiziwa kuibadilisha taarifa yetu mara mbili, baadhi wakisema kwa ushawishi wa fedha, wengine wakidai kwa shinikizo la Mhe. Spika na wengine kwa shinikizo la Waziri Mkuu; tumeshuhudia pilikapilika za usiku na mchana za kujipanga na kuwashawishi baadhi ya Mawaziri na Wabunge kuikana taarifa hii na mapendekezo yake kiasi cha wengine wetu kujiuliza: kulikoni mtu asiye na hatia kuweweseka?

Mheshimiwa Spika, naomba kwa niaba ya wajumbe wenzangu wa Kamati Teule, kukuhakikishia wewe binafsi na Bunge lako tukufu kuwa tumekamilisha kazi tuliyopewa kwa uaminifu na ujasiri mkubwa, dhamira safi, moyo wa uzalendo na kwa kumtanguliza mbele Mwenyezi Mungu katika kila tulilolifanya. Tulichukua kila tahadhari tusibanwe na mgongano wowote wa kimaslahi kiasi kwamba mjumbe mwenzetu, Mhe. Eng. Stella Manyanya, mwajiriwa wa muda mrefu wa TANESCO ambaye alikuwa kwenye likizo isiyo na malipo, akaamua kukatisha ajira yake kwa kujiuzuru. Aidha, tunakuhakikishia Mheshimiwa Spika kuwa hatukupokea senti tano ya mtu wala baiskeli yake. Mwenye ushahidi tofauti, basi alithibitishie Bunge hili tukufu. Mimi na wajumbe wenzangu wa Kamati Teule tuko tayari kuwajibika kisiasa.

- Sasa mkuu vipi alichokifanya Makamba kule CC ilikuwa ni sawa kisheria?

- Maana unasema Mengi anayemjibu Makamba amevunja sheria, sijui sheria ipi hiyo mkuu labda tuwekee hapa, au?

FMES!
Akili ya Makamba unaijua, shule ya Makamba unaijua, uwezo wa Makamba unaujua, na busara zake pia zinajulikana na hata sababu za kufanywa katibu mkuu wa ccm zinajulikana, kumfananisha Mengi na Makamba ni kumtukana Mengi.
Mkuu FMES, amini usiamini, pamoja na sifa na mapambio kwa kitendo cha Mengi kutaja majina ya mafisadi papa na kuonekana shujaa, kuna kundi la wapembuzi yakinifu wanaojiuliza his motive behind, na kuishia kumuona Mengi pia ni mwendawazimu fulani. Sorry to say this, lakini hatimaye ukweli utajulikana.
Uzuri wa eundawazimu, sio wote lazima waokote makopo, bali ni pale unapoona only one point of view as the right way, sasa inapotokea hiyo point of view yako is the wrong way, only the right thinking members of the society ndio watakuona you are wrong, na wale wote who can't see the point, watakuona shujaa. Ndivyo anavyoonekana Mengi shujaa for doing the wrong thing.
Ila pia na mimi, naweza kabisa kuwa ndiye mwendawazimu fulani kudhani kufuata sheria, taratibu na kanuni ni suluhisho la matatizo ya ufisadi. If this is a wrong way, na mimi ninaamini is the right way, basi nami Nakiri mwenywe, na mimi ni mwendawazimu!.
 
Walau tumefanikiwa kumwingiza mtu wetu kwenye conference hii na sasa tunawaletea kinachojiri katika ukumbi wa Kempinski ambapo mhusika mkuu (Rostam) hajafika lakini anatarajiwa kufika dakika yoyote kuanzia sasa.

Conference hii imekuwa tofauti na matarajio ya wengi kwani hii leo wanahabari wa IPP wameruhusiwa kuingia na vyombo mbalimbali vimewakilishwa na wahariri na wapiga picha wao ambao ni Seniors.

Wachache ambao wapo ni pamoja na Muhingo, Bwire, Danny Mwakiteleko na Jacquiline na Channel 10 yupo Dinna.

Tutaendelea kupashana kinachoendelea na baadae tutawaletea audio version ya kilichoongelewa.

Audio clip hii hapa Bonyeza PLAY:

[mp3]http://www.jambovideos.com/mahojiano/RAPC09.mp3[/mp3]

Tupo pamoja...
 
Mpaka dakika hii mheshimiwa hajafika, anasubiriwa kwa hamu kweli. Wengi wameshikilia zana zao za kazi tayari kwa shughuli hii.

Akianza tu tutafahamishana kinachoendelea.
 
Ahsante mkuu...Tunasubiri kwa hamu.
Hapa naongea na mwandishi wetu anadai mpaka dakika hii Rostam hajafika.

Wanahabari waliowasili hapo ni takribani 30 hivi. Pindi akifika tu basi kila kitakachoongelewa tutajitahidi kuwafahamisha.

Kama kuna maswali ambayo tungependa kuongeza katika yale yaliyopendekezwa jana basi ni vema mkanitupia hapa na mwandishi wetu nitamwakilishia ili ikiwezekana atafute wa kuuliza mengine naye walau aulize moja.
 
Kubenea pia yupo.

Ndani ya dakika 5 conference itaanza. ITV wapo, Channel 10, Star Tv wapo, TBC1 wapo na wapiga picha wa magazeti kadhaa wapo.
 
Mwambie amuulize kuwa "bwana Rostam kimya ni silaha kubwa sana kuliko kujibu na kutengeneza habari, mengi kama mwana habari atafaidika na hii habari. kwanini umeamua kuandaa hii conference na kutumia hela zaidi ya Tshs moja uliyoamua kumdai Mengi?"
 
Lini Rostam aliamua kumdai Mengi Tshs moja? Hebu usiwaingize wenzio mkenge. Umeshasema kuwa kimya ni silaha kubwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom