Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
Mwambie amuulize kuwa "bwana Rostam kimya ni silaha kubwa sana kuliko kujibu na kutengeneza habari, mengi kama mwana habari atafaidika na hii habari. kwanini umeamua kuandaa hii conference na kutumia hela zaidi ya Tshs moja uliyoamua kumdai Mengi?"
Nadhani unam-reflect Manji mkuu.
 
Mwambie amuulize kuwa "bwana Rostam kimya ni silaha kubwa sana kuliko kujibu na kutengeneza habari, mengi kama mwana habari atafaidika na hii habari. kwanini umeamua kuandaa hii conference na kutumia hela zaidi ya Tshs moja uliyoamua kumdai Mengi?"

Nafikiri aliyedai Tshs 1 ni Manji Mkuu hebu pitia upya threads ujiridhishe
 
Mwambie amuulize kuwa "bwana Rostam kimya ni silaha kubwa sana kuliko kujibu na kutengeneza habari, mengi kama mwana habari atafaidika na hii habari. kwanini umeamua kuandaa hii conference na kutumia hela zaidi ya Tshs moja uliyoamua kumdai Mengi?"
Anayemdai mengi Shilingi moja ya kitanzania ni Manji siyo Rostam. Naona RA ameogopa kwenda mahakamani, maana jamaa wanaweza sema tulikuwa tunakutafuta afadhali umejileta.
 
Fina Mango na kampuni yake ambayo ndo imepewa tenda ya kuandaa hii Press Conference. Mabaunsa wamekaa as if kuna vita inakaribia, sijui ni wa Rostam au ndo wa kampuni ya Fina Mango!?
 
Hapa naongea na mwandishi wetu anadai mpaka dakika hii Rostam hajafika.

Wanahabari waliowasili hapo ni takribani 30 hivi. Pindi akifika tu basi kila kitakachoongelewa tutajitahidi kuwafahamisha.

Kama kuna maswali ambayo tungependa kuongeza katika yale yaliyopendekezwa jana basi ni vema mkanitupia hapa na mwandishi wetu nitamwakilishia ili ikiwezekana atafute wa kuuliza mengine naye walau aulize moja.

'Kama' Rostam ataamua kumshambulia Mengi kwa kudai naye ana mabaya ambayo amefanya...aulizwe ni kwanini anataja hayo mabaya sasa hivi baada ya yeye kutuhumiwa kuwa ni fisadi papa, na hadhani kufanya hivyo anajaribu kujikosha kwa kusema hata mwenzangu anafanya hivyo?
 
Tuko pamoja na tumekaa mkao wa kula! Tuombe mungu atoe nafasi ya maswali. Hatari nyingine ni waqulizaji kuwa wamepangwa na muulizwaji!....:)
 
Haya bwana nini kinaendelea mpaka hivi sasa
na hao mabaunsa wa nini au kunaweza kutokea mpigano leo hapo jamani?
 
Naam,

Anasema ameitisha mkutano huu kujibu tuhuma za kipuuzi zilizotolewa na Mengi kwa wafanyabiashara 5 hivi huku akitumia kituo chake binafsi.

Anasema alisema hatojibizana na mzee ambaye anastahili kuwa mzazi wake lakini ameona athari ya uzushi uliomo kwenye alichoongea akaona anastahili kujibu kilichoongelewa.

Anaelewa serikali kwa kupitia kwa Sophia Simba na Mkuchika imemjibu lakini yeye sasa anamjibu rasmi leo.
 
Anasema Mengi ana kiherehere na tuhuma zote dhidi yake ni za uwongo na ni upuuzi mtupu. Ni mwendelezo wa chuki binafsi dhidi yake na Mengi
 
Anasema, alimpa Mengi masaa 48 awasilishe ushahidi wa aliyomtumu kwenye vyombo vya sheria na vinginevyo amwombe radhi hadharani. Na sasa hakufanya hivyo mpaka hii leo ameamua kumwanika wazi hadharani maana alitunga uzushi na chuki zake.
 
Pia aulizwe kwa nini yeye (Caspian constractions - 19 %) na rafiki yake wa karibu Peter Noni (Planetel-16 %) wameuza share zao Vodacom kwa kampuni ya Mirambo? Na je nani anamiliki kampuni ya Mirambo?
 
duh! nakuaminia mkuu invisible...hivi jirani na Kempiski hakuna kambi ya ghala la silaha za jeshi??
 
Anasema kuendelea kukaa kimya kungepelekea watanzania kuamini propaganda za Mengi dhidi yake na yeye sasa hakai kimya tena kama mjumbe wa NEC na mtu anayeaminiwa na wananchi wa Igunga na taifa kwa ujumla kwa uchafu anaopandikiziwa na Bwana Mengi.
 
usisahau kumuuliza biashara halali walizofanya babu zake enzi za ukoloni zilijumlisha nini na nini!!??
 
Anasema, alimpa Mengi masaa 48 awasilishe ushahidi wa aliyomtumu kwenye vyombo vya sheria na vinginevyo amwombe radhi hadharani. Na sasa hakufanya hivyo mpaka hii leo ameamua kumwanika wazi hadharani maana alitunga uzushi na chuki zake.

haya mbona yale yale ya kumwaga mboga nimwage ugali. Yeye alitakiwa ampeleke Mengi mahakani. Wamekaa kamati kuu ya CCM, IKULU wameona kumpeleka mahakamani ni hatari kwa mafisadi sasa wakampa RA yellow light ya kujibu kwa mkutano.
 
Pia aulizwe kwa nini yeye (Caspian constractions - 19 %) na rafiki yake wa karibu Peter Noni (Planetel-16 %) wameuza share zao Vodacom kwa kampuni ya Mirambo?

Hilo sio swali la msingi ndugu mashauri. Mtu kuuza share ni uamuzi wake binafsi, akijibu kwamba alikuwa broke ndio maana akauza?

Kama una uhakika na mmiliki wa Kampuni ya Mirambo, uliza swali vizuri so kuzunguka mbuyu ndugu Mashauri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom