Naona sasa MACHUYA yameanza kujitenga na MCHELE hii inaonyesha wazi huyu jamaa ni mfinyu wa Fikra na hakustahili kuwa kiongozi wa Juu ngazi ya Mkoa. Haya anayoyawasilisha yaliisha jadiliwa na ukweli uliwekwa wazi juu ya nini kilifanyika wakati ule wa kuunda katiba Mpya hii anayozungumzia ya mwaka 2004 ni katiba MFU ambayo haipo.
Nakubaliana nawe kwa asilimia mia na moja kasoro moja! Wasifukuzwe uanachama ila wasigombee uongozi wowote ndani ya chama na/au kwa tiketi ya chama kwa kipindi hico ulichopendekeza.
Lakini je, katiba na miongozo ya chama inaruhusu hili?!
Leo tarehe 11/12/2013, mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa Vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.
Taarifa kwa vyombo vya habari
Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili
katika cheo kimoja kwa ngazi moja
Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi unasoma:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya 2 kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.
Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.
Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.
Asanteni
Samson Mwigamba
Mwanachama CHADEMA
11/12/2013
Kusoma TAMKO la Zitto Kabwe la Kukata Rufaa na Kukiukwa kwa Katiba ya chama ingia hapa>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...o-akijibu-yanayodaiwa-makosa-11-ya-zitto.html