Tamko la Mwigamba la uchakachuaji wa katiba ya CHADEMA na ombi kwa msajili wa vyama kuchukua hatua

Kazi kweli kweli. Miaka yote aliyokuwa M/kiti mkoa Arusha kipengele hicho anacho kilalamikia alikuwa hajakiona kweli? Huo nao ni unafiki.
 
Zitto abakishwe akiwa mwanachama wa kawaida ila Mwigamba na Kitilya wapigwe chini maana wao ndo waliandaa Waraka
 
sasa hapa mi ndo huwa nashindwa kuelewa katiba imeandikwa upya mwaka 2006 na niwazi kuwa msajili alipelekewa nakala mwaka huo sasa huyu alimesahau kitu gani na alikuwa wapi kipindi chote kulalamika mpaka leo hivi anataka kutuaminisha kitu gani jamani hawa watu ndo pinda anaagiza kwamba wapigwe tu maana tumechoka sasa alaah lijitu linakuwa kin'gan'ganizi kama nini! Loh hebu nenda magambani wewe hii ni cdm ulijisahau siyo...---- weee

mpango wao wa kuua chama umefeli wamebaki na matamko tu. KAMATI KUU INATAKIWA IWAFUTILIE MBALI HAWA.
 
Hapo ndipo utajua mpango wa kuiondoa cdm kwenye siasa ulisukwa vizuri na isingelikuwa waandaaji kuwa na 'akili ndogo' hakika isingelivuka 2013.
 
We mwigamba nakujua tangu ulipokuwa mwalim wew,ulikuwa ukiwasema walim wenzako kwa wanafunzi eti ni form 4 levers,ulikiwa ukijiona ww ndo ww tu,hatimae ulifukuzwa...
Leo unatudanganya hapa..et ukomo wa uongoz haupo kwenye katiba,siku zote ulikuwa wapi? Na kwann mjiite waasi wa MM? Hiv kama we ni chadema kweli kwann uende kwa msajili ili akusaidie nn sasa? Kuna mgogoro wa kikatiba!!!! Upi huo mbn hakuna mgogoro chadema tena? Ninyi si mnasubiriwa na kamat mkavuliw uanachama???
Hayo ndo maelezo ya kujitetea? Waandish wa habar ndo kamat kuu??? Huna maana ww na wenzako,wote ni kupigwa chini tu..na hatukuhitaj chadema..nenden mkaanzishe chama chenu..------- wewe...
 
Mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.

Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasoma:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya
1 >> kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.

Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.
Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.

MillardAyo
 
Rafiki angu Mwigamba ...umekengeuka kwa kuambatana na wahuni kina MM M1 pole. Umemalizika already
 
baada ya tumaini yao ya kuvuruga ziara ya Dr kushindikana sasa wamepagawa , matamko kila wakati na kila mtu anatoa tamko. majuto ni mjukuu watakoma kulinga.
 
nilisema tangia mwanzo kuwa zile tuhuma zilisukwa very technical hazijibiki kirahisi.ndo maana wameanza kutapatapa kutafta pa kutokea.
 
Mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.

Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
Kiongozi aliyemaliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.
Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi inasoma:
Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi.

Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya
1 >> kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.

Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.
Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.

MillardAyo

Msajili atamsaidiaje maana na yeye si ataonekana zuzu.Katiba ya mwaka 2006 ilipitishwa na wanachama na mkutano halali.Na imekua.ikitumika mara kadhaa .

They are so paranoid,hallucinating and for God's sake they should stop day dreaming !
 
Siamini kama Mwigamba amekuwa mtu wa kutapatapa namna hii, nimeamini maisha yanabadilika
 
Mi nafikiri kutapata huku....umeishiwa sera sijui kama msajili wa vyama anaweza kuingilia swala la katiba....na sijui huo mgogoro wa katiba ni baina yako Mwigimba na ubongo wako?? Utatapata sana huna pa kushika sasa
 
pole sana.....

dhambi ya unafiki na usaliti haitamuacha, itamtafuna kokote, popote.

na kama kweli ana nia njema kwanini miaka yote hajauliza au kutoa hoja hii kwenye vikao halali vya chama?

ndugu mwigamba kwisha habari yako....
unalo hili, pole sana.
 
Baada ya kufikiria na kuona kinachokwenda kuwakuta siku si nyingi zijazo wameanza kufa ganzi taratiibu na kujitoa akiri,wangekuwa hata na busara walau robo kijiko wasingefanya haya yote,wangekimbilia kwenye chama wakatubu na waombe kusamehewa ila nimekumbuka huyu alishasema hatakuja kuomba msamaha,kumbe ndo maana anakwenda kwa msajiri ...na sisi hapohapo as turn around,we completely send you off with a red card.
 
Back
Top Bottom