Tamko la Mwigamba la uchakachuaji wa katiba ya CHADEMA na ombi kwa msajili wa vyama kuchukua hatua

Hivi huyu jamaa wakati ni Mwenyekiti wa CDM mkoa wa Arusha, alikuwepo madarakani kwa mujibu wa katiba ipi?

Binafsi nahisi kama anajichanganya tu na nia yake ya ndani inaonekana kupitia anachokipigania...
 
nimetoka kwenye ban leo na sitaki ban nyingine,haya ndio matatizo ya kumpiga nyoka mkiani badala ya kichwa,cdm finish the job once and for all.
 
ha ha ha haya ndo masuala ambaye wale vinara wa CDM wanajifanya ya kwao waje hapa watoe ufafanuzi mara moja kabla mamluki hwajaelewa vibaya
 
Wamelishwa ujinga wakakubali na washauri wao feki,timueni hawa vibaka wakafie mbele huko na ma maCCM yao
 
kunamtu mmoja anaitwa chabruma aliwahi kuweka nyaraka zote kuhusu katiba za chadema na jinsi chadema walivyobadili katiba kinyemela.
 
chadema wataisoma namba mwaka huu walizoea kuongoza watu ambao hawajui kuhoji ila kwa sasa wataipata fresh yao.
 
Hivi huyu jamaa wakati ni Mwenyekiti wa CDM mkoa wa Arusha, alikuwepo madarakani kwa mujibu wa katiba ipi?

Binafsi nahisi kama anajichanganya tu na nia yake ya ndani inaonekana kupitia anachokipigania...
mkuu mimi naona umtwangie simu mwigamba muulize sisi hatuna majibu mkuu.
 
Hawa wafa maji lazima wataendelea kutapatapa tu mpaka pumzi itakapowaishia!
 

1455970_630126313716110_1779562238_n.jpg

Taarifa kwa vyombo vya habari

Leo tarehe 11/12/2013, mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa Vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.

Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
‘Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili
katika cheo kimoja kwa ngazi moja”

Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi unasoma:
“Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi

Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo
. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya 2 kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.

Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.

Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.
Asanteni
Samson Mwigamba
Mwanachama CHADEMA
11/12/2013

Kusoma TAMKO la Zitto Kabwe la Kukata Rufaa na Kukiukwa kwa Katiba ya chama ingia hapa>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...o-akijibu-yanayodaiwa-makosa-11-ya-zitto.html


kwani CDM bado inakutambua km mwanachama na ww
 
Niliambiwa kuwa" ukipigwa tofari halafu litawanyikie kichwani hata akili hutawanyika. Leo naamini huu msemo wa bibi yangu {mungu akulehem} kwa bwn Mwigamba,hapa bila zindiko hakuna mtu!
 
Bwana Mwigamba that's one wrong move sijui unajaribu kuachieve nini zaidi ya kuonesha umburula tu
Katiba ya Chadema ya 2004 inahusika vipi?
 
Kwani lazima CDM? Mbona vyama vingine vipo na katiba inaruhusu vyama vingine kuanzishwa?
Kuna nini mnachokita zaidi ya kuamini kuwa nia yenu ni kuibomoa CDM?
 
Baada ya Zito, Kitila na Mwigamba kuwasilisha kwa Kamati Kuu ya Chadema barua za kujitetea kuomba wasifukuzwe uanachama, nashauri kwamba katika spirit ya forgiveness ya Mandela, wasifukuzwe uanachama, bali wasiruhusiwe kugombea nafasi yeyote ya uongozi ndani ya Chadema, isipokuwa Ubunge na na Udiwani tu, kwa kipindi cha miaka kumi. Kipindi hiki kitatosha kuwafanya watafakari upya juu ya kuwapo kwao ndani ya Chadema na kuwasaidia kukomaa kisiasa.

Maamuzi ya Kamati Kuu. hayatoki Jamiiforums.
 
Kwani lazima CDM? Mbona vyama vingine vipo na katiba inaruhusu vyama vingine kuanzishwa?
Kuna nini mnachokita zaidi ya kuamini kuwa nia yenu ni kuibomoa CDM?
Wamepagawa hawa wasaliti, wameshakula mahela ya magamba halafu hawaja timiza walicho tumwa na hela za kurudisha hawana lazima wachamganyikiwe. Wakafie mbali haya makapi
 
Back
Top Bottom