Tamko la Mwigamba la uchakachuaji wa katiba ya CHADEMA na ombi kwa msajili wa vyama kuchukua hatua

TeamZitto

Member
May 5, 2012
18
197

1455970_630126313716110_1779562238_n.jpg

Taarifa kwa vyombo vya habari

Leo tarehe 11/12/2013, mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa Vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.

Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
‘Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili
katika cheo kimoja kwa ngazi moja"

Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi unasoma:
"Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi."

Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo
. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya 2 kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.

Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.

Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.
Asanteni
Samson Mwigamba
Mwanachama CHADEMA
11/12/2013

Kusoma TAMKO la Zitto Kabwe la Kukata Rufaa na Kukiukwa kwa Katiba ya chama ingia hapa>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...o-akijibu-yanayodaiwa-makosa-11-ya-zitto.html

Naona sasa MACHUYA yameanza kujitenga na MCHELE hii inaonyesha wazi huyu jamaa ni mfinyu wa Fikra na hakustahili kuwa kiongozi wa Juu ngazi ya Mkoa. Haya anayoyawasilisha yaliisha jadiliwa na ukweli uliwekwa wazi juu ya nini kilifanyika wakati ule wa kuunda katiba Mpya hii anayozungumzia ya mwaka 2004 ni katiba MFU ambayo haipo.
 
Mwigamba anaumwa, angeweka nyaraka na sio kutukumbusha katiba ambayo ilishakufa ya mwaka 2004 , msajili anatumia katiba ya mwaka 2006 , na hana ya mwaka 2004 kwani ilishakufa, ni sawa na mtu CCM kwenda kwa msajili kudai katiba ya CCM yenye azimio la Arusha na kusema kuwa kuna mgogoro wa Kikatiba.
 
Dr. Slaa alijiabisha sana alipodanganya watu kuwa kipengele hicho hakijawahi kuwepo kwenye katiba. Tangu wakati huo Slaa haaminiki tena maneno yake!
 
Naona sasa MACHUYA yameanza kujitenga na MCHELE hii inaonyesha wazi huyu jamaa ni mfinyu wa Fikra na hakustahili kuwa kiongozi wa Juu ngazi ya Mkoa. Haya anayoyawasilisha yaliisha jadiliwa na ukweli uliwekwa wazi juu ya nini kilifanyika wakati ule wa kuunda katiba Mpya hii anayozungumzia ya mwaka 2004 ni katiba MFU ambayo haipo.

Chadema ingeshinda uchaguzi mkuu huyu ndio angekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha.
 
Huu ni ujinga kama sio ujuha , katiba anayosema ilibadilishwa vipengele na sio kuandikwa upya , yeye anataka msajili atumie kifungu cha 5.3.2 c cha mwaka 2004 , wakati huo huo anasema katiba ya Chadema kifungu cha 6.3.2 c ......kuchanganyikiwa ni kubaya sana .........atafute njia mpya ya toke vipi sio hii.....
 
TeamZitto Mwigamba, nilikuwa nakuheshimu sana, ila kwa ulipofikia naona kama una mtindio wa ubongo, siamini kabisa kama huyu ni yule kamanda mpambanaji tulie kuwa tunakuheshimu na kukutii A town, kumbe wewe ni kaa yule kiumbe asiye na mbele wala nyuma, it does not cost you chochote ukikaa kimya, mstaaranu huheshimika kwa busara zake, hebu kuwa mstaarabu usituharibie image tamaa zako zinakuponza, wewe sio zaidi ya CHADEMA
 
Last edited by a moderator:
Naona matamko yanaendelea mwigamba ameona asijifiche sasa aingie mzimamzima na sio maskin mkulima tena
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia mia na moja kasoro moja! Wasifukuzwe uanachama ila wasigombee uongozi wowote ndani ya chama na/au kwa tiketi ya chama kwa kipindi hico ulichopendekeza. Si urais, ubunge, udiwani wala nafasi yoyote katika chama. Waruhusiwe kupiga tu kushiriki katika kampeni za wagombea wa chama. Baada ya miaka mitano ifanyike tathmini kuona kama wana mwelekeo wa kutubu na kubadilika kama itakuwa bado waendelee kutumikia adhabu kwa miaka hiyo kumi na baada ya miaka hiyo kumi, cc ya chama ifanye uamuzi wa mwisho juu ya adhabu wanayostahiki.

Lakini je, katiba na miongozo ya chama inaruhusu hili?!
 
TeamZitto
===>Anae chamba sana lazima atoke na mavi,nyie endeleeni na ujinga wenu.
===>Naamini DK Kitila hataendelea na upuuzi huu na atawakimbia tu.
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana nawe kwa asilimia mia na moja kasoro moja! Wasifukuzwe uanachama ila wasigombee uongozi wowote ndani ya chama na/au kwa tiketi ya chama kwa kipindi hico ulichopendekeza.

Lakini je, katiba na miongozo ya chama inaruhusu hili?!

Swali zuri sana mkuu. Siijui kiundani katiba ya Chadema, lakini kama itakuwa haijaongelea au kurejezea masuala ya ku-discipline wanachama basi itakuwa ni upungufu unaostahili kurekebishwa. Si kwamba katiba itasema mwananchama anaekiuka misingi ya katiba asigombee kwa miaka kumi, bali inaweza kutaja kwamba atachukuliwa hatua stahili za kinidhamu na chombo fulani, kwa mfano Kamati Kuu. Mambo yanayohusu kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni muhimu kuwapo ndani ya katiba ya chama au kikundi chochote kilichosajiriwa rasmi kisheria.
 
Haya haya hayaaa tena! Naona Mwigamba na Zitto wamegoma kujibu tuhuma 11 badala yake wanakuja na matamko na kukata rufaa ambayo hata kesi ya tuhuma hizo haijatolewa maamuzi. Wanatakiwa wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama wa CHADEMA? Wao wanakata rufaa.

Naona kwa mbaaaaali Dr. Kitila Mkumbo amewakacha hawa wahaini.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari

Leo tarehe 11/12/2013, mimi Samson Mwigamba, mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ninawasilisha malalamiko yangu kwa Msajili wa Vyama na ninaomba atoe mwongozo kuhusu mgogoro wa kikatiba uliopo ndani ya Chama kufuatia kipengele cha katiba kinachogusia ukomo wa uongozi kubadilishwa kinyume na utaratibu.

Katiba ya Chadema ya mwaka 2004 kipengele 5.3.2 (c) inasomeka ifuatavyo kuhusu Muda wa Uongozi:
‘Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi kwa muda usiozidi vipindi viwili
katika cheo kimoja kwa ngazi moja”

Hata hivyo katiba ya chama ya mwaka 2006 kipengele cha 6.3.2 ( c) inayozungumzia muda wa uongozi unasoma:
“Kiongozi aliyemaliza muda wa ungozi ana haki ya kugombea
na kuchaguliwa tena mradi awe anatimizamasharti ya
kuchaguliwa kuwa kiongozi

Sentensi kuhusu ukomo wa uongozi haipo
. Ni kweli kuwa Marekebisho ya Katiba yalifanyika mwaka 2006, lakini hoja ya 2 kubadili kipengele hicho haikuwepo na muhtasari zinaonyesha wazi kuwa kulikuwa hakuna mjadala wa kipengele hicho au kuhusu suala zima la ukomo wa uongozi.

Hivyo napenda nisisitize kuwa si kweli kwamba Chadema haijawahi kuwa na Katiba ambayo ina ukomo wa uongozi. Pia si kweli kwamba mwaka 2006 Katiba mpya iliandikwa upya bali marekebisho yalifanywa kwa baadhi ya vipengele. Ila kipengele 5.3.2 (c ) haikujadiliwa.

Natumaini kuwa Msajili wa vyama ataweza kutupatia hekima zake na kutoa mwongozo ili suala hili lipatiwe suluhisho la kudumu ndani ya chama chetu.
Asanteni
Samson Mwigamba
Mwanachama CHADEMA
11/12/2013

Kusoma TAMKO la Zitto Kabwe la Kukata Rufaa na Kukiukwa kwa Katiba ya chama ingia hapa>>https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...o-akijibu-yanayodaiwa-makosa-11-ya-zitto.html

sasa hapa mi ndo huwa nashindwa kuelewa katiba imeandikwa upya mwaka 2006 na niwazi kuwa msajili alipelekewa nakala mwaka huo sasa huyu alimesahau kitu gani na alikuwa wapi kipindi chote kulalamika mpaka leo hivi anataka kutuaminisha kitu gani jamani hawa watu ndo pinda anaagiza kwamba wapigwe tu maana tumechoka sasa alaah lijitu linakuwa kin'gan'ganizi kama nini! Loh hebu nenda magambani wewe hii ni cdm ulijisahau siyo...---- weee
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom