George Jinasa
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 399
- 52
tunapotoa maoni ni vizuri sana tukajua mantiki ya mgomo wa madaktari ili tujue kama ni tatizo la serikali ya awamu ya nne au ni tatizo la athari ya uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni. Ni wakati gani katika historia ya tanzania ambapo maslahi ya madaktari yalikuwa bora kuliko sasa? Ni wakati gani katika historia ya tanzania ambapo madaktari wangeachiwa kugoma huku watu wakipoteza maisha yao bila hatua kali sana kuchukuliwa?
Kuhusisha mnaouita udhaifu wa raisi wa sasa na maslahi duni ya madaktari kunatia wasiwasi kama tatizo ni maslahi duni ya madaktari au uraisi wa tanzania?
Mkutano wa Wanaharakati na Waandishi wa Habari: Sehemu ya tamko: "...kama kweli Rais Jakaya Kikwete ana nia ya dhati ya kutetea maisha ya Watanzania, tangu Jumamosi hadi leo angelikuwa amekwishachukua hatua ili kuzuia maafa yatakayotokea ikiwemo vifo zaidi vya Watanzania kutokana na mgomo mwingine wa Madaktari.
Wananchi tunamtaka Rais atekeleze madai ya madaktari mara moja, yakiwemo yafuatayo:
1. Waziri wa Afya na Naibu wake, ambao wameshindwa kujiuzulu hadi sasa wawajibishwe na Rais aliyewaweka madarakani ili wapishe mchakato wa kutatua mgogoro walioshindwa kuudhibiti, uweze kutatuliwa;
2. Huduma ya afya na mazingira ya kazi yaboreshwe haraka iwezekanavyo, kwani hali hiyo ndiyo inawafedhehesha madaktari katika kutumia taaluma walizo nazo;
3. Iwapo serikali haitatimiza hayo, italazimisha umma wa Watanzania kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika kwa njia ya nguvu za umma, kuanzia Tarehe 07/03/2012;
4. Tunawasihi Watanzania wote wanaojali utu wao na utu wa Watanzania wenzao wawe tayari kuinuka kuchukua hatua itakayoifanya serikali kutimiza wajibu wake katika kuzuia watu zaidi kupoteza maisha.
Ni sisi Watanzania wenye uchungu na nchi yetu na maisha yetu. Imesainiwa leo, Tarehe 06/03/2012"
hivi ninyi wanaharakati wanasiasa au ni wanaharakati??? hivi uwanaharakati, ni kwa kuangalia haki za madaktari tu??..hivi mbona hamuongelei wananchi wanao kufa kwa ajili ya migomo ya hawa dr's???.. hivi mnazani wodi za watoto au wazazi zinajengwa siku moja??kweli mnaakili ninyi???mbona sasa hamuongelei kuhusu mahitaji ambayo tayari wametekelezewa???. serikali haitishiwi ninyi wanaharakati uchwala ambao mnangoja matukio ndo mjitokeze.tumewachoka ninyi na hao madaktari wenu wapenda fedha. wala msitudanganye muandamane ninyi wenyewe na familia zenu
Katiba Repoti yao ya mwaka 2010/11 ya Haki za Binaadamu Tanzania wamezungumzia mauwaji yanayotokana na watu kujinyakulia sheria mikononi na kuwauwa wanaozaniwa vibaka. Hapakuwepo na nukta ya vifo vilivyotokana na migomo haramu ya madaktari wetu. Daktari yoyote anayegoma lazima atarajie kwamba mgombo wake utasababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma, wengine kupata ulemavu ambao ungeepukika na wengine kupata mateso makali ya muda mrefu bila huduma. Kwa kujua ukweli huu unaotokana na unyeti wa fani ya udaktari, ndio maana miiko yenu ya udaktari inawataka maslahi ya kuokoa maisha ya binaadamu yawe juu kuliko maslahi yote. Ndio maana kabla hamjakabidhiwa dhima ya udaktari mlikula kiapo cha kutii miiko ya kesi yenu kwa hiyari yenu wenyewe. Ndio maana Serikali ikawapa dhama ya vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na madawa. Mnapogoma ninyi hata vifaa mbalimbali vya matibabu haviwezi kutumika hata kama kuna wenzenu wenye ujuzi ambao wako radhi kuitika wito wa viapo vyao. Daktari wetu npendwa alipofanyiwa unyama na watu wasiojulikana tumeona jinsi mlivyojitahidi kuokoa maisha yake kwa kutumia vifaa na madawa mbalimbali vya hospitali zetu. Muendelee kufanya hivyo kwa wagonjwa wote wakati mnaendelea kujadiliana na Serikali juu ya haki zenu. Pia ombeni siku za mbeleni muwe na uwakilishi Bungeni na katika Wizara ya Afya ili wawepo wanasiasa wa kuwakilisha hoja zenu mahali panapohusika wakati nyinyi mkiendelea kutii viapo vyenu.
Kaka Jackbauer naiona hoja yako na nakubali kwamba Serikali kama muajiri ina dhima ya kuhakikisha kwamba madaktari wanafanya kazi katika mazingira mazuri. Hata hivyo, misingi ya maadili ya udaktari haipaswi kuyumbishwa na maslahi ya kawaida ya kimapato labda yawe ni mhimu sana katika maisha yao kiasi cha kuhalalisha udharura. Lazima kuwepo na urari kati ya maslahi binafsi na maslahi ya wagonjwa.
Ndugu yangu pamoja na pumba zangu lazima ujue kwamba suala hapa sio kulalamika bali kugoma kiasi cha kupelekea vifo vya walalahoi ambao hali yao ni duni kupindukia. Pia athari ya mgomo haiwagusi hao unaowalalamikia maana hata bila mgomo wanatibia TMJ, Tumanini, Aghakani nk.
Isitoshe mtu anapoamua kuingia katika fani ya udaktari anakuwa ameridhia miiko yake. Masuala ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya umma ni mambo yanayopaswa kutatuliwa kisisa zaidi.
Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.
Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.
Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.
Acheni unafiki
issue ingekua ni kiapo hata hao unaowashabikia waliapa wakati wanakabidhiwa office bt wanachofanya mwenyewe unakijua!
Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.
Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.
Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.
Acheni unafiki