Tamko la LHRC na waandishi wa habari leo kuhusu mgomo wa madaktari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la LHRC na waandishi wa habari leo kuhusu mgomo wa madaktari!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SirBonge, Mar 6, 2012.

 1. S

  SirBonge JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2010
  Messages: 349
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 60
  Mkutano wa Wanaharakati na Waandishi wa Habari: Sehemu ya tamko: "...kama kweli Rais Jakaya Kikwete ana nia ya dhati ya kutetea maisha ya Watanzania, tangu Jumamosi hadi leo angelikuwa amekwishachukua hatua ili kuzuia maafa yatakayotokea ikiwemo vifo zaidi vya Watanzania kutokana na mgomo mwingine wa Madaktari.

  Wananchi tunamtaka Rais atekeleze madai ya madaktari mara moja, yakiwemo yafuatayo:

  1. Waziri wa Afya na Naibu wake, ambao wameshindwa kujiuzulu hadi sasa wawajibishwe na Rais aliyewaweka madarakani ili wapishe mchakato wa kutatua mgogoro walioshindwa kuudhibiti, uweze kutatuliwa;

  2. Huduma ya afya na mazingira ya kazi yaboreshwe haraka iwezekanavyo, kwani hali hiyo ndiyo inawafedhehesha madaktari katika kutumia taaluma walizo nazo;

  3. Iwapo serikali haitatimiza hayo, italazimisha umma wa Watanzania kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika kwa njia ya nguvu za umma, kuanzia Tarehe 07/03/2012;

  4. Tunawasihi Watanzania wote wanaojali utu wao na utu wa Watanzania wenzao wawe tayari kuinuka kuchukua hatua itakayoifanya serikali kutimiza wajibu wake katika kuzuia watu zaidi kupoteza maisha.

  Ni sisi Watanzania wenye uchungu na nchi yetu na maisha yetu. Imesainiwa leo, Tarehe 06/03/2012"
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  maumivu ya kichwa huanza polepole
   
 3. W

  We know next JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yalipokuwa yanatokea kama haya ktk nchi nyingine za Africa, tulidhani Tanzania ni kisiwa na haya hayawezi kutokea, sasa naona formular yetu imeprove wrong.....Nilisema zamani, kwa mgomo huu wa madaktari, hakuna atakayekuwa salama...sasa muda umewadia..
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Tunateseka kwa sababu Rais aliye madarakani hakuchaguliwa na watanzania, alitumia pesa yake kupata madaraka, viashiria ndio kama hivi, jifunzeni kwa mfano wa nabii suleiman alipoletewa kesi mbele yake kuwahusu wamama wawili wakivutania kitoto kichanga ki-hai na mwili wa kitoto kichanga kana kwamba mtoto yupi ni wa nani huku kila mmama akidai aliye hai ndiye wake! (mmama mmoja wao alifanya hila, alimlalia mwanae usiku akafa, akamchukua wa mwenzie na kumuweka wake aliyekufa ubavuni pa mwenzie. walipoamka tazama mwenzie alipomtazama kwa makini aligundua kitoto kilichokufa si chake mzozo ukaanzia hapo) mfalme suleiman alipoona kila mmoja anang'ang'ania kuwa mtoto mzima ndiye wake, aliamua aletewe shoka ili amcharange vipande viwili awagawanyishe wale wamama. yule mwenye mtoto hai aliposikia hivyo akamwambia mfalme akasema mpatie huyu mama mtoto huyu hai usimcharange! lakini yule aliyemlalia kichanga wake akamwambia mfalme akasema "bora umcharange tukose wote!!!" ndiposa mfalme suleiman alipotambua ya kuwa kichanga hai kilikuwa cha yule mama aliyebambikiwa na mwenziwe, na akaamuru akichukue kichanga chake. AMINI NAWAAMBIENI kikwete hakuchaguliwa na watanzania. Ni baba gani watoto wake wakimuomba samaki akawapa nyokaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!
   
 5. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu umegusa pale palipo nako!
   
 6. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Napita kwanza
   
 7. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tunakoelekea...!
   
 8. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #8
  Mar 6, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,506
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  capitalist at work..
  TAJIRI ataenda AGHAKHAN,masikin ATAKUFA/ATAENDA KWA MGANGA..
   
 9. m

  mashimbamang'oma Member

  #9
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani kunakiongozi yeyote anayetibiwaga kwenye hizi hospital? Kama checkup wanafanyia nje ya nchi watajuaje adha ya mgomo wa madaktari? Jukumu ni letu kupigania ukombozi wetu kwa kushirikiana na hawa wanaharakati.....
   
 10. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hii ni move nzuri, ila kweli wanaharakati watatekeleza hilo wanalosema? maana hatuchelewi kusikia "nguvu ya umma imehairishwa"... all in all serikali inafanya mzaha sana katika hili, ila mwisho wa siku si serikali itakayoumia, ni sisi walala hoi..
   
 11. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  na maumivu si mzaha na matibabu yakr lazima yawe ya haraka na ndio maana MUngu akatengeneza madaktari dawa ya kutibu kichwa dawa hii ina mchanganyiko wa mgomo na shinikizo la kuboresha afya ya watz ikiwa imefungwa kwenye paketi ya wananchi ili iweze kufungua vichwa vyao na kuviponya
   
 12. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nia tunayo, nguvu tunayo na uwezo tunao... Nakumbuka kauli za Baba wa Taifa wakati tunajiandaa na vita ya uganda
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Haya mabeberu hayajali kwa kuwa hizi hospitali za ndani haziwahusu. Wao wakiugua pamoja na familia zao wanaenda Appollo na ujerumani alikolazwa Lowasa kwa sasa.
  Amini usiamini jk ni chaguo la Mungu kutimiza madhara yaliyokusudiwa kwa taifa la Tanzania.
  .
   
 14. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  natamani che guevara angekuwa hai,najua angekuja kutusaidia kuwaondoa viongozi waovu
   
 15. n

  ngudzu Member

  #15
  Mar 6, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mungu awe na wanaharakati hawa lbada wataleta ukombozi kwa mahangaiko yao haya.
   
 16. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  Tunapotoa maoni ni vizuri sana tukajua mantiki ya mgomo wa madaktari ili tujue kama ni tatizo la serikali ya awamu ya nne au ni tatizo la athari ya uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni. Ni wakati gani katika historia ya Tanzania ambapo maslahi ya madaktari yalikuwa bora kuliko sasa? Ni wakati gani katika historia ya Tanzania ambapo madaktari wangeachiwa kugoma huku watu wakipoteza maisha yao bila hatua kali sana kuchukuliwa?

  Kuhusisha mnaouita udhaifu wa Raisi wa sasa na maslahi duni ya madaktari kunatia wasiwasi kama tatizo ni maslahi duni ya madaktari au Uraisi wa Tanzania?
   
 17. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ukiwa na madaktari wetu wanajua kwamba hospitali hizi za umma ni zetu walala hoi na sio wale wanaowaita mabeberu mbona wanaendelea kufanya migomo huku walalahoi tukifa na vigogo wakiendelea kutibiwa Appollo na katika mahospitali ya watu binafsi ambako kipindi hiki cha migomo ndiko madaktari wanakotolea huduma?
   
 18. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Nyie ndio mliowaweka madarakani hao mabeberu. Wanachofanya madaktari nikuwafungua macho ili mjue kuwa ubeberu hauna nafasi tena zama hizi.
   
 19. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Nchi ipi ya Afrika ambako madaktari walikwenda kinyume na viapo vyao na kugomea kuwatibu walala hoi na nchi ikafanikiwa? Kwani lengo la mgomo ni ili watu walale barabarani na mapinduzi ya kibabe yafanyike? Ni wapi?
   
 20. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi naona pia hili linatokana na athari ile ile ya ubeperu. Hivi leo tukisema wafanyakazi wote bila kujali fani zao walipwe mshahara sawa na wasiruhusiwe kufanya kazi zaidi ya hospital mbili ni wangapi tutakubali? Tungepiga kelele kwamba masomo ya shahada ya udaktari yawe bure ili tuwe na madaktari wengi.
   
Loading...