Tamko la LHRC na waandishi wa habari leo kuhusu mgomo wa madaktari!

Declaration of Geneva (1948)
Physician's Oath[h=4]Adopted by the General Assembly of the World Medical Association, Geneva, Switzerland, September 1948 and amended by the 22nd World Medical Assembly, Sydney, Australia, August 1968.[/h][h=3]CIRP Introduction[/h]The World Medical Association is an association of national medical associations. This oath seems to be a response to the atrocities committed by doctors in Nazi Germany. Notably, this oath requires the physician to "not use [his] medical knowledge contrary to the laws of humanity." This document was adopted by the World Medical Association only three months before the United Nations General Assembly adopted the Universal Declaration of Human Rights (1948) which provides for the security of the person.

[h=3]Physician's Oath[/h]At the time of being admitted as a member of the medical profession:

  • I solemnly pledge myself to consecrate my life to the service of humanity;
  • I will give to my teachers the respect and gratitude which is their due;
  • I will practice my profession with conscience and dignity; the health of my patient will be my first consideration;
  • I will maintain by all the means in my power, the honor and the noble traditions of the medical profession; my colleagues will be my brothers;
  • I will not permit considerations of religion, nationality, race, party politics or social standing to intervene between my duty and my patient;
  • I will maintain the utmost respect for human life from the time of conception, even under threat, I will not use my medical knowledge contrary to the laws of humanity;
  • I make these promises solemnly, freely and upon my honor.

Citation:
  • Declaration of Geneva (1948). Adopted by the General Assembly of World Medical Association at Geneva Switzerland, September 1948.
 
Ebu tosome vizuri kiapo cha udaktari hapo juu na tuone kama mgomo wa madaktari ni sahihi licha ya kusababisha upotevu wa maisha ya ndugu na jamaa zetu?
 
jinasa naomba uweke na majukumu ya serikali ili tujue kiapo hiki kinatumika kwenye circumstances zipi.lets be fair my friend!
 
tunapotoa maoni ni vizuri sana tukajua mantiki ya mgomo wa madaktari ili tujue kama ni tatizo la serikali ya awamu ya nne au ni tatizo la athari ya uhuru wa vyombo vya habari na kutoa maoni. Ni wakati gani katika historia ya tanzania ambapo maslahi ya madaktari yalikuwa bora kuliko sasa? Ni wakati gani katika historia ya tanzania ambapo madaktari wangeachiwa kugoma huku watu wakipoteza maisha yao bila hatua kali sana kuchukuliwa?

Kuhusisha mnaouita udhaifu wa raisi wa sasa na maslahi duni ya madaktari kunatia wasiwasi kama tatizo ni maslahi duni ya madaktari au uraisi wa tanzania?

huna point, pumba enzi za mwalimu hali ilikuwa duni kwa kila mtu ndo maana walielewa, na hawakuweza kugoma kwani hali ilikuwa inafahamika, lakini leo embu angalia wabunge wanavyolipana, angalia mafisadi wanavyochota mahela na hakuna hatua, sasa kwanini wasilalamike? Tunahitaji pato la taifa kila mtu limnufaishe, tena ma dr wametumia busara sana, kwani mara ngapi wamejadiliana lakini hakuna kinachotekelezwa kabla ya kukaa sawa inakuja riboti watu wamechimbia mabilioni ya madola uswis... Hata kma ni mvumilivu basi lazima ufike mwisho. Waache wagome tu na wametumia unyetu wa idara yao. Mbona waalimu wakigoma wala hamsemi mnawaacha tu, ila ma dr ndo wabaya acheni unafiki tz
 
Kaka Jackbauer naiona hoja yako na nakubali kwamba Serikali kama muajiri ina dhima ya kuhakikisha kwamba madaktari wanafanya kazi katika mazingira mazuri. Hata hivyo, misingi ya maadili ya udaktari haipaswi kuyumbishwa na maslahi ya kawaida ya kimapato labda yawe ni mhimu sana katika maisha yao kiasi cha kuhalalisha udharura. Lazima kuwepo na urari kati ya maslahi binafsi na maslahi ya wagonjwa.
 
Ndugu yangu pamoja na pumba zangu lazima ujue kwamba suala hapa sio kulalamika bali kugoma kiasi cha kupelekea vifo vya walalahoi ambao hali yao ni duni kupindukia. Pia athari ya mgomo haiwagusi hao unaowalalamikia maana hata bila mgomo wanatibia TMJ, Tumanini, Aghakani nk.

Isitoshe mtu anapoamua kuingia katika fani ya udaktari anakuwa ameridhia miiko yake. Masuala ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya umma ni mambo yanayopaswa kutatuliwa kisisa zaidi.
 
Wapi prof Mwaikusa, Rwegasira?
Kweli serikali hii ni dhaifu.. Inaua bila mpango wanaharakati..
 
Mkutano wa Wanaharakati na Waandishi wa Habari: Sehemu ya tamko: "...kama kweli Rais Jakaya Kikwete ana nia ya dhati ya kutetea maisha ya Watanzania, tangu Jumamosi hadi leo angelikuwa amekwishachukua hatua ili kuzuia maafa yatakayotokea ikiwemo vifo zaidi vya Watanzania kutokana na mgomo mwingine wa Madaktari.

Wananchi tunamtaka Rais atekeleze madai ya madaktari mara moja, yakiwemo yafuatayo:

1. Waziri wa Afya na Naibu wake, ambao wameshindwa kujiuzulu hadi sasa wawajibishwe na Rais aliyewaweka madarakani ili wapishe mchakato wa kutatua mgogoro walioshindwa kuudhibiti, uweze kutatuliwa;

2. Huduma ya afya na mazingira ya kazi yaboreshwe haraka iwezekanavyo, kwani hali hiyo ndiyo inawafedhehesha madaktari katika kutumia taaluma walizo nazo;

3. Iwapo serikali haitatimiza hayo, italazimisha umma wa Watanzania kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika kwa njia ya nguvu za umma, kuanzia Tarehe 07/03/2012;

4. Tunawasihi Watanzania wote wanaojali utu wao na utu wa Watanzania wenzao wawe tayari kuinuka kuchukua hatua itakayoifanya serikali kutimiza wajibu wake katika kuzuia watu zaidi kupoteza maisha.

Ni sisi Watanzania wenye uchungu na nchi yetu na maisha yetu. Imesainiwa leo, Tarehe 06/03/2012"

hivi ninyi wanaharakati wanasiasa au ni wanaharakati??? hivi uwanaharakati, ni kwa kuangalia haki za madaktari tu??..hivi mbona hamuongelei wananchi wanao kufa kwa ajili ya migomo ya hawa dr's???.. hivi mnazani wodi za watoto au wazazi zinajengwa siku moja??kweli mnaakili ninyi???mbona sasa hamuongelei kuhusu mahitaji ambayo tayari wametekelezewa???. serikali haitishiwi ninyi wanaharakati uchwala ambao mnangoja matukio ndo mjitokeze.tumewachoka ninyi na hao madaktari wenu wapenda fedha. wala msitudanganye muandamane ninyi wenyewe na familia zenu
 
Katiba Repoti yao ya mwaka 2010/11 ya Haki za Binaadamu Tanzania wamezungumzia mauwaji yanayotokana na watu kujinyakulia sheria mikononi na kuwauwa wanaozaniwa vibaka. Hapakuwepo na nukta ya vifo vilivyotokana na migomo haramu ya madaktari wetu. Daktari yoyote anayegoma lazima atarajie kwamba mgombo wake utasababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma, wengine kupata ulemavu ambao ungeepukika na wengine kupata mateso makali ya muda mrefu bila huduma. Kwa kujua ukweli huu unaotokana na unyeti wa fani ya udaktari, ndio maana miiko yenu ya udaktari inawataka maslahi ya kuokoa maisha ya binaadamu yawe juu kuliko maslahi yote. Ndio maana kabla hamjakabidhiwa dhima ya udaktari mlikula kiapo cha kutii miiko ya kesi yenu kwa hiyari yenu wenyewe. Ndio maana Serikali ikawapa dhama ya vifaa mbalimbali vya tiba pamoja na madawa. Mnapogoma ninyi hata vifaa mbalimbali vya matibabu haviwezi kutumika hata kama kuna wenzenu wenye ujuzi ambao wako radhi kuitika wito wa viapo vyao. Daktari wetu npendwa alipofanyiwa unyama na watu wasiojulikana tumeona jinsi mlivyojitahidi kuokoa maisha yake kwa kutumia vifaa na madawa mbalimbali vya hospitali zetu. Muendelee kufanya hivyo kwa wagonjwa wote wakati mnaendelea kujadiliana na Serikali juu ya haki zenu. Pia ombeni siku za mbeleni muwe na uwakilishi Bungeni na katika Wizara ya Afya ili wawepo wanasiasa wa kuwakilisha hoja zenu mahali panapohusika wakati nyinyi mkiendelea kutii viapo vyenu.
 
issue ingekua ni kiapo hata hao unaowashabikia waliapa wakati wanakabidhiwa office bt wanachofanya mwenyewe unakijua!
 
Kaka Jackbauer naiona hoja yako na nakubali kwamba Serikali kama muajiri ina dhima ya kuhakikisha kwamba madaktari wanafanya kazi katika mazingira mazuri. Hata hivyo, misingi ya maadili ya udaktari haipaswi kuyumbishwa na maslahi ya kawaida ya kimapato labda yawe ni mhimu sana katika maisha yao kiasi cha kuhalalisha udharura. Lazima kuwepo na urari kati ya maslahi binafsi na maslahi ya wagonjwa.

Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.

Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.

Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.

Acheni unafiki
 
Ndugu yangu pamoja na pumba zangu lazima ujue kwamba suala hapa sio kulalamika bali kugoma kiasi cha kupelekea vifo vya walalahoi ambao hali yao ni duni kupindukia. Pia athari ya mgomo haiwagusi hao unaowalalamikia maana hata bila mgomo wanatibia TMJ, Tumanini, Aghakani nk.

Isitoshe mtu anapoamua kuingia katika fani ya udaktari anakuwa ameridhia miiko yake. Masuala ya ufisadi na matumizi mabaya ya mali ya umma ni mambo yanayopaswa kutatuliwa kisisa zaidi.

Hapo juu umewataja ''walalahoi ambao hali zao ni duni kupindukia''...
Je ni nani aliepelekea hali za hao jamaa kuwa duni kupindukia?
ni madaktari au ni mabepari walioko Serikalini?
 
Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.

Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.

Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.

Acheni unafiki

Kinywa cha mtu mzima kinanuka lakini maneno yake ni dawa...
Mtu mzima nimekubali madini uliyotema hapo ni next level.
 
Achana na hayo makombo ya waliokutuma uende ukasome udaktari uje utibu bure wagonjwa.

Kinachowapagawisha ni wasiwasi wenu wa utawala kuanguka halafu mnajifanya mnawapenda sana wagonjwa.

Kama mnawapenda wagonjwa na kuthamini uhai kama mnavyolalama hospitali zisingekuwa taabani na wala msingekuwa mnauwa watu msitu wa pande na kwenye maandamano ya amani.

Acheni unafiki

Kwenye hizo nukata za matusi na kashifa sitakujibu nitamuachia moderator kama yupo aamue kama umenitendea haki kunitukana kwa kuniita mnafiki na kwamba na kwamba ninaongea makombo ya watu unaodai walionituma. Mimi sijapewa kupaji cha kushindana kwa matusi na sidhani kama hivyo ndivyo tunapawa kujadiliana katika mtandao wenye hadhi kama JF.

Hamna mtu anataka madaktari wafanye kazi bure wala hamna daktari anaefanya kazi bure hapa Tanzania. Issue ni namna madaktari tunavyoweka maslahi ya kimapato juu kuliko maslahi ya maisha ya wagonjwa wetu kinyume na kiapo cha miiko ya udaktari tulikula. Suala la Serikali kupinduliwa unaliibua wewe na sijui unalihusisha vipi na maandamano ya madaktari.

Sijui unaweza kutoa ushahidi gani wa mimi kuhusika kuuwa mtu katika msitu wa Pande. Kama huna hoja ya kujibu hoja sio vibaya kukaa kimya kuliko kutoa tuhuma nzito kama hiyo kwa mtu usiomjua wala asiyekujua.

Kama kuna dosali katika posts zangu ni vizuri ukanikosoa na kunirekebisha na wala sitashangaa. Maana, haya ninayotoa ni maoni ambayo kwa nafsi yangu na upeo waangu wa ufahamu nadhani kwamba ni sahihi. Lakini kama binaadamu naweza kukosea lakini sio sababu ya kutukanwa na kuzushiwa kashifa kubwa na chafu kama hizo.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom