Tamko la Kanisa la Morovian

Tamko la Kanisa la Morovian

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,351
MAASKOFU NA WACHUNGAJI, KEMEENI MAOVU! MSIWAOGOPE WANASIASA, WATAWALA NA MATAJIRI!

Hawa ni watu ajabu sana! Walipokuwa katika Vyuo vya Theologia na Biblia walisoma sana kuhusu ujasiri wa Askofu Mkuu Janani Luwum wa Kanisa Kianglikana Uganda jinsi alivyomkabili Iddi Amin na kumueleza aache kuua watu wake; wengi wao walisoma na kutiwa moyo na ujasiri wa Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Kanisa Anglikana Afrika Kusini jinsi alivyopambana na mfumo wa Ubaguzi wa Rangi ambao ulitweza na kufedhehesha utu, na kuwaua watu weusi kama ndege; wapo waliosoma na kufurahia sana maandishi kuhusu Liberation Theology yaliyotolewa na Padre Gutierrez Gutierrez Gutierrez wa Roman Catholic Church kule Latin America jinsi alivyopinga unyonyaji na ukandamizaji wa wananchi wanyonge uliokuwa ukifanywa na matajiri waliokuwa wameunda ushirika muovu na watawala wakandamizaji; wapo waliotamani sana wamuone Martin Luther King Jr., yule Mchungaji wa Kibatisti jinsi alivyopambana kutokomeza ubaguzi na ukandamizaji kule Marekani, mbengu za haki zilizopiganiwa na yeye zilizopelekea Mmarekani mwenye asili ya Kiafrika Barack Obama kutawala Marekani bado inasimuliwa hadi sasa; wengine wamejaza maandishi ya Padre Profesa Martin Luther jinsi alivyotetea wanyonge na kusimamia matengenezo ya Kanisa kule Ulaya hasa Ujerumani; wengine hadi leo wanatukuza ujasiri wa Padre Profesa Jan Huss yule mwanzilishi wa u-Moravian alivyopinga uovu hadi akachomwa moto hadharani. Wengi wanafundisha na kuhubiri nadharia kuhusu haki kwa mujibu na mtazamo wa ki- Biblia huku wakikesha kusoma vitabu vya manabii kama Amos, Yeremia, Ezra, nk.

Kinachoshangaza ni kuwa wanaposikia na kuona maovu ya aina hiyo hiyo au hata yanayokithiri katika jamii zao wanafumba macho. Waumini wao wanapofanyiwa maovu na kuonewa na hata kupoteza maisha hawafumbui kinywa. Watu wengine wasiokuwa waumini wao wanapofanyiwa ukatili ndio haiwahusu kabisa! Wanasahau kuwa Nabii Amos alikemea maovu yaliyokuwa yakitendwa hata nje ya mipaka ya Nchi yake ya Yuda kwani aliwaonya watawala wa Damaska, Gaza, Tiro, Edomu, Amoni, Moabu, Israeli, nk.

Watumishi wengine wachache wakijitokeza kukemea maovu basi wao (wasiotaka kukemea) hugeuka kuwa watesi wa watumishi wanaokemea maovu! Maaskofu wengine wanadiriki hata kuwatishia kuwatimua katika makanisa Wachungaji walio majasiri wa kukemea uovu! Wanawanyamazisha kiaina. Kwao ujasiri wa Yohana Mbatizaji aliyemkemea Herode ni nadharia ya kuisoma Kanisani tu lakini isiyofaa kuiishi. Wanafikiri kuwa kukemea uzinzi na ulevi madhabahuni ndio wito pekee walioitiwa lakini ubadhilifu na uporaji wa mali ya umma pamoja na ukandamizaji na utekaji na unyanyasaji wa watu siyo dhambi ya kukemewa madhabahuni. Kwao kutumia madhabahu kukemea ulevi na uzinzi kila Jumapili ndio utumishi lakini kutumia madhabahu hiyo hiyo kukemea watu wanaoeneza chuki katika jamii na wanaotesa, kuteka na kuua watu wengine ni 'kuingiza siasa Makanisani'! Kwao kutumia madhabahu kukemea unyanyasaji katika familia ndio utumishi lakini kutumia madhabahu hiyo hiyo kukemea unyanyasaji mahali pa kazi, na katika mifumo ya kisiasa na uendeshaji wa serikali ni kufanya siasa. Kwao wanaona ni ujasiri kuwaambia waumini kuacha kuwasingizia majirani zao kama moja ya Amri Kumi za Mungu inavyotaka lakini kuwaambia wanasiasa na watendaji katika mifumo ya kiserikali na kisiasa kuacha kuwasingizia watu na kuwabambikia kesi na kuwachafua wenzao ni 'kuleta siasa Kanisani'!

Ee Mungu uturehemu na ututie ujasiri tusiache kuwaonya hata hawa Wachungaji na Maaskofu wanaoupa kisogo wito wao wa kuonya, kukemea na kushauri katika jamii ulimowatuma kukutumikia kama Maandiko yanavyotaka (Ezekieli 33:1-20). Kama tunao ujasiri wa kuwaonya na kuwakemea matajiri, wanasiasa, na watendaji wa serikali, tupe pia ujasiri wa kuwakemea viongozi wa Makanisa walio waoga. Tupe hekima na neema ya kutokuwachukia tunaowakemea. Tupo uangavu wa kiimani ili tuone pia maovu yanayoweza kutendwa na hao tunaojua wanateswa na kunyanyaswa. Ee Bwana! Fufua kazi yako katikati ya mataifa!

Ujumbe huu nimeutoa leo nikiwa nimetimiza miaka 25 ya utumishi wangu tangu nilipojiunga rasmi katika kazi ya kumtumikia Mungu (full time ministry) siku ile ya tarehe 4 Agosti 1994.

Mwana Kondoo Ameshinda Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

1565034293475.jpeg
 
Baba askofu Bagonza
SERIKALI SI MALAIKA

Mwaka 2015 hatukuchagua malaika kuwa serikali. Tulichagua watu wenye ubinadamu. Watu hao na udhaifu wao wakaunda serikali. Serikali iliyoundwa na binadamu dhaifu, haiwezi kuwa takatifu kama malaika.

Kwa hiyo serikali ni dhaifu, kwa sababu imeundwa na watu dhaifu, na ilichaguliwa na watu dhaifu. Udhaifu maana yake ni "si kamilifu", "si takatifu" na ina uwezekano wa kufanya makosa.

Madaraka hayaondoi udhaifu. Madaraka si chanjo ya kuzuia kufanya makosa.

Kwa hiyo, nafasi au madaraka hayakingi uchoyo, ubabe, ulafi, uwongo, fitna, ukatili, upendeleo, ukabila, udini, ujinga, maradhi, na hila. Kisingizio cha "kufanya siasa" si kinga ya kuzuia madhara ya udhaifu huo.

Hali kadhalika, kutambua udhaifu si tiketi ya kuendelea kufanya makosa.
Kukubali kuwa unaweza kufanya makosa, ni ibada inayokubalika mbele za Mungu kwa sababu ni ukiri (admission) kuwa wewe si Mungu bali mwanadamu.

Kukiri udhaifu ni kupata nguvu, si kupoteza nguvu. Kunyenyekea ni kuhifadhi nguvu si kuogopa. Hapa ndipo tunakutana na tofauti kati ya ukatili na ujasiri, uungwana na unyonge.

Kama ningechagua, ningemheshimu anayenipa chakula kuliko anayeninyima chakula ili nimjue ana madaraka juu yangu.

Haki huanzia pale tunapokubaliana kuwa sisi ni binadamu wenye udhaifu katika kufikiri, kunena, kutenda. Waliopewa mengi, wadaiwa mengi. Yatosha siku kwa uovu wake.

Hasira ya Mwanadamu haitendi haki ya Mungu. Kisasi ni kwa Bwana wa visasi vyote, anayependa rehema kuliko sadaka.
 
Viongozi wa dini waweza kuungana na wale wa kisiasa katika kuwadhibiti kondoo wasiweze kufurukuta hata kidogo.
Hali hiyo ni mbaya sana kwa ustawi wa jamii na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Katika kuhakikisha system of checks and balances inaimarika, viongozi wa dini na wale wa serikali wasiungane dhidi ya raia.
 
Viongozi wa dini waweza kuungana na wale wa kisiasa katika kuwadhibiti kondoo wasiweze kufurukuta hata kidogo.
Hali hiyo ni mbaya sana kwa ustawi wa jamii na ustawi wa taifa kwa ujumla.
Katika kuhakikisha system of checks and balances inaimarika, viongozi wa dini na wale wa serikali wasiungane dhidi ya raia.
 
Mleta mada hv umewahi shuhudia Askofu au mchungaji wa Moravian kaombea mgonjwa yeyote akapona ?Hili ni moja ya makanisa ambayo wauminia wao ni fuata upepo sijawahi ona. Wakisikia Mwakasege kaja wote wanakimbila huko,sjui kaja muhubiri fulani wote wanakimbilia huko .(The likes of KKT na Anglican).Hakuna kinachoendelea huko kwenye makanisa yao zaidi ya michango,na harambeee hasa kipindi cha uchaguzi. Hayo ni mapango ya biashara ,nawaonea huruma washirika wa hayo makanisa ni wasindikizaji wa safari ya mbinguni. Mi nilikua muumini wao nikagutuka kule sio kusali ni kupoteza mda.
 
Mleta mada hv umewahi shuhudia Askofu au mchungaji wa Moravian kaombea mgonjwa yeyote akapona ?Hili ni moja ya makanisa ambayo wauminia wao ni fuata upepo sijawahi ona. Wakisikia Mwakasege kaja wote wanakimbila huko,sjui kaja muhubiri fulani wote wanakimbilia huko .(The likes of KKT na Anglican).Hakuna kinachoendelea huko kwenye makanisa yao zaidi ya michango,na harambeee hasa kipindi cha uchaguzi. Hayo ni mapango ya biashara ,nawaonea huruma washirika wa hayo makanisa ni wasindikizaji wa safari ya mbinguni. Mi nilikua muumini wao nikagutuka kule sio kusali ni kupoteza mda.
Tunajadili The contents za kiongozi wa dini. Kuombea na Karama hata wewe unaweza kuwa na hiyo karama ukiwa na imani.

Kama wana kibali cha serikali ku operate in Tanzania, we don’t have a mora authority to judge them.
 
Mkurugenzi wa Taasisi moja,nyeti sana hapa nchini,ni mchungaji, sasa huwezi jua kwamba aliingia katika uchungaji akiwa na mission ya kupandikiza wachungaji ambao ni feki ila watumishi wa idara yake.

Baadhi si wachungaji, ni simba katika ngozi ya kondoo, wanawinda kwa niaba ya aliyewatuma,

Ndiyo yaleyale ya kwenda kumwambia mchungaji shida zako au kutubu kwake,jioni taarifa ziko makumbusho
 
Mleta mada hv umewahi shuhudia Askofu au mchungaji wa Moravian kaombea mgonjwa yeyote akapona ?Hili ni moja ya makanisa ambayo wauminia wao ni fuata upepo sijawahi ona. Wakisikia Mwakasege kaja wote wanakimbila huko,sjui kaja muhubiri fulani wote wanakimbilia huko .(The likes of KKT na Anglican).Hakuna kinachoendelea huko kwenye makanisa yao zaidi ya michango,na harambeee hasa kipindi cha uchaguzi. Hayo ni mapango ya biashara ,nawaonea huruma washirika wa hayo makanisa ni wasindikizaji wa safari ya mbinguni. Mi nilikua muumini wao nikagutuka kule sio kusali ni kupoteza mda.
Wewe ni mpumbavu kama wale wapumbavu wa chama cha mazwazwa
 
Nilifikiri ni askofu wa MORAVIAN.....

MORAVIAN ni kanisa lenye kujitambua, kuchanganya mtu anayejiita askofu wa Moravian na kanisa la Moravian ni kulikosea kanisa
 
2020 hakika hakika tunataka kuona kwa wazi wagombea wetu wakiwa jasiri kusema na kuweka bayana misimamo yao na kutetea:
Haki dhidi ya udhalimu , wema dhidi ya udhalimu,
Uokoaji dhidi ya Utesaji .
Utawala wa hekima na Busara dhidi ya utawala wa Maguvu.
Upendo dhidi ya Chuki.
Upotoshaji wa kuhesabu Kura dhidi ya kupindua matokeo ya kura.
Demokrasia dhidi ya udikteta.
Uokoaji dhidi ya Utekaji.
Uponyaji dhidi ya uuaji wa makusudi.
Utajiri dhidi ya umaskini.
Ukabila /Ukanda dhidi ya Utaifa.


Hii itawasaidia wale wanaotetea upande wowote kupata muda wa kueleza ni kwa nini anasimama upande mmoja wa kati ya hayo hapo juu.
Mana kama ni utekaji na utesaji ni wazi vijana wa UVIVUSisemi walishajipambanua kuwa wao watamshughulikia yeyote wanayetofautiana naye. Na wakasema dola ni la kwao kwa hiyo watafanya chocho wanachotaka.
2020 ni wakati wao wa kueleza Dunia na wapiga kura kuwa kwa nini waliamua kuhamasisha uhalifu dhidi ya binadam? Na kwa nini kwao Watu walioumbwa na Mungu sio muhimu??

Na yeyote atakayejidai kuwa anakemea wakati wa Kampeni tuu wakati alikaa kimya binadam wakiwa wanapotea na kuuawa na kutekwa atuambie kwa nini alikaa kimya wakati alikua alikua na uwezo wa kukemea ?

Nampongeza sana Baba Askofu, Hakika ameisoma na kuielewa Vizuri Biblia anayoiamini.
Mambo Mazuri yaliyoko katika vitabu vya Dini ni pamoja na kupinga uovu unaotendwa na binadam.
Wanasiasa nao ni binadam hivyo nao pia watakemewa kama binadam wengine wanavyokemewa. Hakuna binadam aliyeko juu ya Maandiko ya Mwenyezi Mungu na maelekezo na AMRI ZAKE.

Katiba yetu na Dini zote kuanzia za asili zinakataza kuua ,kutesa ,dhulma,uonevu,uongo, usingiziaji, uporaji ,wizi, rushwa, Upendeleo ,ubaguzi,dharau n.k.
 
Wangempiga marufuku asitie mguu kanisani dhalimu huyo.
Sipichi yangu iliyo andikwa na watu na kunifanya nipande ngazi ndefu ya kitaaluma leo hii imegeuka na kunaka damu kuna safari za milele zimehusishwa nazo.
 
Back
Top Bottom