Kanisa ndilo lilisababisha mauaji ya kimbari Rwanda.
Muogope Mungu na uwe mkweli achana na Imani za Chuki na uongo.
Unajidhalilisha na kuudhalilisha uislam wako.
Wapo Waislam wengi tu Leo hii ni waelewa sana kwenye mambo ya imani za dunia nzima kwa sasa.
Watu wanajua uko mpango wa siri wa Kishetani na umejiingiza kwa waumini na viongozi wa Dini zote. Ndio maana Dunia nzima kuna vurugu na chanzo chake ni uonevy unaotikana na watawala.
Hakuna Dini ya kweli inayoweza kukaa kimya dhidi ya udhalimu ,iwe ni ukristo au uislam au Ubudha au Upagani.
Tuwasaidie watu kujua Haki na dhulma.
Haya mambo ya kueneza Chuki za watu kidini ni upuuzi na ujinga mtupu.
Dini bila haki kwenye jamii ni upumbavu.
Rwanda Makanisa ndipo walipokua wanakimbilia watu dhaifu kama inavyokuwa kwenye nchi za kiislam kwenye Vita ambapo wale watu wasio na vurugu hukimbilia kujihifadhi.
Wanapokua wengi ni dhahiri viongozi wa Dini wanajitokeza kukemea serikali kuwa iache kuua watu wake mana inasababisha Wakimbizi kujaa kwenye nyumba za ibada na wanaotwishwa mzigo na hata kuuawa au kuandamwa ni Viongozi wa Dini waliowapokea na kuwahifadhi.
Mara nyingine wanakimbilia hata wale wanaotafutwa na wanaogombana nao.
Siku zote adui wa serikali na Chama Tawala ni yule anayehatarisha madaraka yao kwa kuwapinga.
Ni kanisa lipi Rwanda liliwahi kuingiza Sialaha na kuanzaisha Jeshi au Kundi Rasmi la kuua?
Kama ilitikea kwa kanisa moja au mawili ndio kusema ni nchi nzima?
Hivi nani anaweza kuishinda vita inayoanzishwa na Kanisa?
Hayupo Duniani hata yule baba yenu Lucifer hawezi .
Kanisa ni Kazi ya Kristo au Masihi Mwenyewe ndio maana hata Utawala Mkubwa kama wa Rumi ulinyoosha mikono na kujisalimisha chini ya Kanisa.
Kanisa kazi yake ni kusimama kwenye Ukweli.
Kanisa haliwezi kukaa kimya na kuangalia wanadam wanauawa bila sababu hasa watu wasio na madhara.
Yaani watu wasiotumia silaha kwa nini wauawe bila hata kuhukumiwa mahakamani?
Kama MTU anakosa afikishwe mahakamani mana tumejiwekea sheria.
Kwa nini wakae kimya kisa eti Rwanda walihusika kwenye mauaji?
Hivi ni namna gani Vita ya Watusi na Wahutu ingekwepeka ?
Kwa nini haikua vita kati ya Dhehebu moja na lingine au Kanisa na Misikiti au Uislam kule Rwanda?
Kwa nini ilikua ni kati ya Wahutu na Watutsi ambao wengi ni Wakristo??
Hapo inakuaje vita ya Kanisa?
Watawala wasimamie haki na sheria hakuna vurugu inayoweza kutokea mahali penye haki hiyo ni kanuni ya Imani zote kuanzia zile za asili.
Tusidanganyane kwa sababu ya kuona kuwa tunaweza kutumia risasi muda wote.
Hatuna Jeshi kubwa kama la Sadam au Gadaf lakini watu walipochoka kuongozwa kwa Risasi waligeuka na kupuuza mema yote yaliyofanywa na watawala wao.
Hata IDD Amini alikua malendo sana kwa Taifa lake kosa alilofanya ni kutojali uhai wa watu wake na haki zao za msingi akawaza kuimarisha tu utawala wake,watu wakamchoka na kumtoa kwa kushirikiana na majeshi ya wageni.
Tunayashangila haya Leo lakini Kesho wakinyamaza hawa maaskofu ujue kesho kutwa atatekwa Shekhe na kuuawa halafu wataaminishwa watu kuwa alikua gaidi na jamaii itakaa kimya mana magaidi wanaogopwa . Kumbe ni ugomvi wa kimadaraka tu au ameoneka kuwa huyo Shekhe a anaukaribu na Mtu Fulani ambaye ni tishio la Madaraka ya watu Fulani.
Haki ibaki kuwa haki hata kama imesemwa na Mpagani.
Leo hii tunamuenzi Kinjekitile Ngwale pamoja na kuwa alikua na Dini zake za asili kwa sababu tu alipigania HAKI.