Tamko la Kamati Kuu ya CCM; Muda waongezwa kujivua gamba

Miruko

Senior Member
Feb 8, 2008
173
46
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).

2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.

3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea.
Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.

7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake. Imetolewa na:-

Nape M. Nnauye (MNEC)

KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011
 
8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama. Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.

Hamna kuvua gamba wala nini. Mara siku 90 mara 120, wote ma vuvuzela tu.
 
4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwakwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.

Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha beiya mafuta ya taa kama suluhisho.

Kweli haya sasa ni maigizo, Mhe. amepitisha bajeti na kukubali bei ya mafuta ya taa ipande akiwa kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, then huku akiwa kama mwenyekiti wa CC anasema hapana bei ya afuta ya taa ishushe tena anaiamuru serikali hiyo hiyo anayoongoza yeye!!
 
yaani pamoja na kuamuru simu za wajumbe wa CC kuzimwa ndiyo mnakuja na hii "soft statement" ? kweli magamba vilaza. Halafu unajiita katibu mwenezi, duuuh!
 
4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwakwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.

Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha beiya mafuta ya taa kama suluhisho.

Kweli haya sasa ni maigizo, Mhe. amepitisha bajeti na kukubali bei ya mafuta ya taa ipande akiwa kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, then huku akiwa kama mwenyekiti wa CC anasema hapana bei ya afuta ya taa ishushe tena anaiamuru serikali hiyo hiyo anayoongoza yeye!!

It is impossible kutoka na la maana CCM!!!! Hii ndio wamekaaa mpaka saa 7 usiku. Si mtu mmoja anaweza kuamua hayo. Gumu ni nini. hawa watu wa ajabu. Kikwete dhaifu.
 
8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama. Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowoto mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.

Jamani tukisema Lowassa CCM haimwezi, mnabisha. Haya sasa gamba mnakufanalo
 
Hamna kuvua gamba wala nini. Mara siku 90 mara 120, wote ma vuvuzela tu.

Kauli ya kujivua gamba ilikuwa ni usanii tu ndio maana sasa wanaikimbia kauli yao wenyewe. Lowassa na Chenge wamegoma kung'oka na hakuna mwenye ubavu wa kuthubutu kuwafukuza maana chama chote kimejaa mafisadi.
 
Kumbe kuna watu wameambiwa wajipime???Mbona Bwana Mukama alikanusha hii kitu kwenye mkutano wake na wahariri??? Na Mbona Rostam anasema kujiuzulu kwake hakuna uhusiano na mambo hayo ya kujivua gamba?? By the way, Taarifa hii haikuwa ya kukaa usiku mzima na kuja kupatikana saa hizi kumeshakuchwa! Nape alipaswa kuitoa kabla ya kwenda kuuza sura bungeni ama angeweza pia kuiweka kwenye ukurasa wake wa FB mapema, haina kipya saaannaaaa
 
Kuna waliyoyasahau nini?
Ilo suala la mafuta ya taa wanalipinga ccm wameamua kuwa chama cha upinzani?
Au iliamriwa na serikali ingine sio hii ya magamba
 
Sidhani kama kuna umuhimu wa kuwa na vikao vya cc taifa vya ccm.na muda umefika sana kutovichukulia kwa umuhimu vikao vyao,wanapanga mipango ambayo hawawezi kuifanyia maamuzi.take this: don't start a thing that you don't finish.
 
4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwakwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.

Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha beiya mafuta ya taa kama suluhisho.

Kweli haya sasa ni maigizo, Mhe. amepitisha bajeti na kukubali bei ya mafuta ya taa ipande akiwa kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, then huku akiwa kama mwenyekiti wa CC anasema hapana bei ya afuta ya taa ishushe tena anaiamuru serikali hiyo hiyo anayoongoza yeye!!

Ni usanii wa hali ya juu!!!! Tangu bajeti ilipotangazwa kakaa kimya kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ya taa mpaka kwenye kikao cha CC!!! Ili kutaka kuonyesha kwamba Magamba inawajali Watanzania!!!! Ni kichekesho cha hali ya juu.
 
Muundo wa CCM wa uongozi haujakaa sawa. Nadhani Raisi wa nchi na baraza lake la mawaziri hawakupaswa kuwa wajumbe wa kamati kuu ya CCM. Hapo chama kingeweza kweli kuiwajibisha, kuionya na kuishauri ipasavyo. Vinginevyo tamko lao ni usanii mtupu.
 
Pesa ya kuwasafirisha na malazi pamoja na chakula vimetumika kwa utumbo kama huo. Tz tuna kazi kubwa sana.
 
Taarifa raini kama lotion.tunahitaji kujua kuhusu magamba.yako wapi maamuzi magumu?mia
 
Loh yamekuwa hayo, ama kweli Magamba si chama kile enzi zile, ikiwa wanaweza kuwa mstari wa mbele kuwakolimba walio safi kivipi wanashindwa kuwakolimba EL na AC "Lo..kazi ni kwako!
 
..hawa jamaa kila wakikutana wanatoka na msamiati mpya.. sasa wametoka na "Maslahi mapana".
 
Back
Top Bottom