Tamko la Kamati Kuu ya CCM; Muda waongezwa kujivua gamba

Wanatafuta nani wa kumfunga paka kengele????. Hawajui wanachofanya, wameishiwa sera.
 
Jamani..Kikwete hakujua kama mafuta yameongezwa bei,mnamuonea buree..hata yeye ameona kwenye magazeti hizi taarifa kama sisi tu!
yap!!!! Wakati bajet inapitishwa alikuwa nje ya nchi kikazi so alimtuma mwakilishi wake aiptishe kwa niaba. Shughuli za kitaifa na kimataifa zimemzonga sana. Pole braza!!! Next tyme chagua mwakilishi mzuri, huyo anakupoteza.

 
dah siasa za nchi hii za ajabu kweli,kwani kabla ya kuja na huo mpango mkakati eti 'wa kuzuia uchakachuaji wa mafuta' hawakua wametathimini kwa kina impact yake kwa wananchi walio wengi? Halafu m/kiti si ndie raisi alieridhia hii kitu? Na ni haohao waliokuwa mstari wa mbele kuwapuuza wapinzani waliopinga huo mkakati! Iweje tena leo waanze kufungua kurasa za nyuma ambazo hawakua tayari kuzipitia kisawasawa hapo kabla ambapo mambo yalikua bado machanga?! Siasa za nchi hii zinatia hasira,khaaaa! Mpaka zatia kinyaaa,waweza tapika eti
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).


2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.

3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea.
Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine. Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.

7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama.
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake. Imetolewa na:-


Nape M. Nnauye (MNEC)

KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI
DODOMA
1/8/2011
[/QUOTE

Hii jamani si kutukejeli? Iwapo Serikali wanayo wao na wajumbe wengi ni viongozi wa Serikali hawaridhishwi na nani zaidi ya wenewe kwa wenyewe.
 
Yani kwenye kikao cha baraza la mawaziri wameamua mafuta ya pande bei, kwenye halmashauri ya magamba wanasema bei ishuke eti inamuumiza mtu wa chini, vikao vyote hvyo mwenyekiti mmoja. Hakika bora tz bora hata tungempa DOVUTWA tujue moja.
<br />
<br />
1.ccm mwatuchangana bajeti si ilishapitishwa sasa huu upinzani kutoka ndani ya ccm vipi tena. 2.Siku vigogo hao watakapojivua magamba yao basi itatokea tetemeko kubwa na baadhi yao ndani ya cc hawatasalimika. Ushauri: yamalizeni kiutu uzima.
 
Back
Top Bottom