Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,360
We jamaa yangu wee, hivi unataka serikali yetu ichukue hatua gani tena zaidi ya kutoa tamko kwa vyombo vya habari, na wakubwa kukaa mkao wa kula?
hivi jamani kuna mtu anajua makadirio ya ujenzi wa daraja la kigamboni? Badala ya serikali kupitisha bakuli kwanini isipeleke pesa hiyo yote either kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni au hata kutatua tatizo la umeme Kigoma au pengine pesa hiyo ikatumika kuweka mtandao wa maji toka kimbiji kuja temeke,kitunda,pugu na maeneo mengine ambayo yana uhaba mkubwa wa maji safi na salama?
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Southwark mjini London, Uingereza kuiamuru Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kulipa faini ya Paundi za kiingereza laki tano 500,000 kwa kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kihasibu kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni ya BAE Systems kwa Mfanyabiashara Shailesh Vithlani wa Tanzania miaka mitano iliyopita.
Serikali ya Tanzania,kupitia Ubalozi wetu nchini Uingereza imeomba taarifa rasmi kutoka Serikali ya Uingereza kuhusu uamuzi huo. Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.
Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems.
Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
22 Desemba, 2010
Source: issamichuzi.blogspot.com
Taarifa ya foreign affairs kuhusu chenji ya radar, nimependa hapo kwenye red, swali wanasuburi kwa hamu kwa nia njema na manufaa ya walalahoi au zitarudi tena kulekule???????
Mbona mambo ya ndani wako kimya kuhusu hili pamoja na kuwa BAE wamekiri kosa la Rushwa lilikuwa merinated kutoka kosa la rushwa na kwenda mwenye kosa la kutoweka kumbukumbu sahihi huku kwetu wahusika mustakabali wao unakuwaje????
Kweli nchi ya majuha!
Kweli nchi hii ina majuha wa kupitiliza. Hivi serikali ya CCM wan akimbilia hizo pesa huku kuna kesi dhidi ya Chenge na wengine ambayo upelelezi wake uliisha na kungojea tu kufika mahakamani kama inavyoeleza dokezo la Wikileaks hapa chini akinukuliwa si mwingione bali Hosea mwenyewe?
Mimi naona serikali ya UK iweke sharti kwamba isilipe fidia hiyo hadi watuhumiwa wa rada hapa TZ wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa, kama vile serikali ya UK ilivyofanya kwa BAE (mtuhumiwa waliotoa rushwa) -- walifikishwa mahakamani na kutozwa faini. Ni lazima serikali yetu huku nayo ionekana inalishughulikia suala hili la radar. Kweli JK na timu yake hawafai kuongoza nchi hii ki-uadilifu.
PCB: Ready to Prosecute the BAE Radar Deal
------------------------------------------
¶2. (C) Edward Hoseah, Director General of the Prevention of
Corruption Bureau (PCB) told the DCM that the PCB was almost
finished with its investigation of the U.K.- Tanzanian BAE
radar deal and that it intended to prosecute the case. We
are focused on the 31 percent commission paid to BAE. We
understand that businessmen need commissions but the question
is whether 31 percent is lawful or not, Hoseah said. He
called the deal dirty and said it involved officials from
the Ministry of Defence and at least one or two senior level
military officers.
¶3. (C) Hoseah said that the two primary suspects, XXXXXXXXXXXX and Shailesh Vithlani, CEO of
Merlin International, were currently out of the country but
that when they returned the GOT would begin to prosecute. I
have obtained President Kikwetes support to prosecute the
culprits once they return to Tanzania, he said, stressing
that prosecution of the case would mark an important
milestone in the PCBs struggle. The real signal of the
GOTs political commitment will be when we take this radar
case to court, Hoseah said.
¶4. (C) Note: Shailesh Vithlani is a British citizen who
reportedly grew up in Tanzania. He heads Merlin
International, a Dar es Salaam based company. Merlin
International has been implicated as the agent for Britains
BAE Systems which sold a USD 40 million military radar system
to the GOT in 2002. Beyond the BAE radar deal, Merlin has
been linked in the media to a range of other high profile
government deals including the sale of a Gulfstream
presidential jet to former President Benjamin Mkapa.
According to a July 13 report in This Day, a local newspaper,
at the time of the BAE deal, Vithlanis local partner was
Tanil Somaiya of Shivacom Tanzania Ltd.
wizara iseme pia Watanzani waliosababisha aibu hiyo watachukuliwa hatua gani?
Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani
hivi jamani kuna mtu anajua makadirio ya ujenzi wa daraja la kigamboni? Badala ya serikali kupitisha bakuli kwanini isipeleke pesa hiyo yote either kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni au hata kutatua tatizo la umeme Kigoma au pengine pesa hiyo ikatumika kuweka mtandao wa maji toka kimbiji kuja temeke,kitunda,pugu na maeneo mengine ambayo yana uhaba mkubwa wa maji safi na salama?
Taarifa kwa vyombo vya Habari
... Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.
Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems. ...
[/SIZE]