Tamko la Foreign Affairs kuhusu kesi ya Radar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Foreign Affairs kuhusu kesi ya Radar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngambo Ngali, Dec 23, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Taarifa kwa vyombo vya Habari

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Southwark mjini London, Uingereza kuiamuru Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kulipa faini ya Paundi za kiingereza laki tano 500,000 kwa kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kihasibu kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni ya BAE Systems kwa Mfanyabiashara Shailesh Vithlani wa Tanzania miaka mitano iliyopita.

  Serikali ya Tanzania,kupitia Ubalozi wetu nchini Uingereza imeomba taarifa rasmi kutoka Serikali ya Uingereza kuhusu uamuzi huo. Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.

  Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems.

  Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  22 Desemba, 2010

  Source: issamichuzi.blogspot.com

  Taarifa ya foreign affairs kuhusu chenji ya radar, nimependa hapo kwenye red, swali wanasuburi kwa hamu kwa nia njema na manufaa ya walalahoi au zitarudi tena kulekule???????

  Mbona mambo ya ndani wako kimya kuhusu hili pamoja na kuwa BAE wamekiri kosa la Rushwa lilikuwa merinated kutoka kosa la rushwa na kwenda mwenye kosa la kutoweka kumbukumbu sahihi huku kwetu wahusika mustakabali wao unakuwaje????
   
 2. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu, hiyo chenji inarudi kwenye mzunguko wa ufisadi mwingine , si unajua tena 2015 siyo mbali?.......................
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  grrrrrr...sometimes hili linchi bana... miviongozi inatupayukia kuhusu rejesho la hela, hali wengi wetu usongo wetu ni kuona wahusika wa huu uhujumu uchumi wanaozea jela!!

  Sijui, labda tusubirie tamko la wizara ya mambo ya ndani na la polisi wetu... ukiachilia huyo Vithlani aliyekimbia, lazima kuna viongozi waliohusika...
   
 4. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  We jamaa yangu wee, hivi unataka serikali yetu ichukue hatua gani tena zaidi ya kutoa tamko kwa vyombo vya habari, na wakubwa kukaa mkao wa kula?
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,197
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo baada ya tamko basi " The End"
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  hahahahha yaaaaani hawa watu eti inafuatilia kwa karibu.
  Karibu si wanaye chenge mbona wameshamsafisha.

  Hizi sanaa nyingine zinatia kinyaa.
  Na vipi kuhusu Ule UFISADI wa jengo na Ubalozi wa Italy
   
 7. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  hivi jamani kuna mtu anajua makadirio ya ujenzi wa daraja la kigamboni? Badala ya serikali kupitisha bakuli kwanini isipeleke pesa hiyo yote either kwenye ujenzi wa daraja la kigamboni au hata kutatua tatizo la umeme Kigoma au pengine pesa hiyo ikatumika kuweka mtandao wa maji toka kimbiji kuja temeke,kitunda,pugu na maeneo mengine ambayo yana uhaba mkubwa wa maji safi na salama?
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  wizara iseme pia Watanzani waliosababisha aibu hiyo watachukuliwa hatua gani?
   
 9. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,565
  Likes Received: 624
  Trophy Points: 280
  Utaambiwa hizi pesa zilishapelekwa kwenye mfuko maalumu tumboni kwa mtu...hakuna mtu/kiongozi mwenye mawazo kama yako...
  sometime nikifikiria hii nchi...ni kama mwanamke kahaba ambaye amekataa tamaa na yeye haangalii nani analala naye na wala hadai pesa wala chochote....
   
 10. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sisi tunstaka waliohusika huku kwetu wanashughulikiwa ipasavyo si issue ya kudai fidia.
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Kweli nchi ya majuha!
   
 12. C

  Chief JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Wa kupitiliza.
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweli nchi hii ina majuha wa kupitiliza. Hivi serikali ya CCM wan akimbilia hizo pesa huku kuna kesi dhidi ya Chenge na wengine ambayo upelelezi wake uliisha na kungojea tu kufika mahakamani kama inavyoeleza dokezo la Wikileaks hapa chini akinukuliwa si mwingione bali Hosea mwenyewe?

  Mimi naona serikali ya UK iweke sharti kwamba isilipe fidia hiyo hadi watuhumiwa wa rada hapa TZ wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa, kama vile serikali ya UK ilivyofanya kwa BAE (mtuhumiwa waliotoa rushwa) -- walifikishwa mahakamani na kutozwa faini. Ni lazima serikali yetu huku nayo ionekana inalishughulikia suala hili la radar. Kweli JK na timu yake hawafai kuongoza nchi hii ki-uadilifu.

  PCB: Ready to Prosecute the BAE Radar Deal
  ------------------------------------------
  ¶2. (C) Edward Hoseah, Director General of the Prevention of
  Corruption Bureau (PCB) told the DCM that the PCB was almost
  finished with its investigation of the U.K.- Tanzanian BAE
  radar deal and that it intended to prosecute the case. "We
  are focused on the 31 percent commission paid to BAE. We
  understand that businessmen need commissions but the question
  is whether 31 percent is lawful or not," Hoseah said. He
  called the deal "dirty" and said it involved officials from
  the Ministry of Defence and at least one or two senior level
  military officers.

  ¶3. (C) Hoseah said that the two primary suspects, XXXXXXXXXXXX and Shailesh Vithlani, CEO of
  Merlin International, were currently out of the country but
  that when they returned the GOT would begin to prosecute. "I
  have obtained President Kikwete's support to prosecute the
  culprits once they return to Tanzania," he said, stressing
  that prosecution of the case would mark an important
  milestone in the PCB's struggle. "The real signal of the
  GOT's political commitment will be when we take this radar
  case to court," Hoseah said.

  ¶4. (C) Note: Shailesh Vithlani is a British citizen who
  reportedly grew up in Tanzania. He heads Merlin
  International, a Dar es Salaam based company. Merlin
  International has been implicated as the agent for Britain's
  BAE Systems which sold a USD 40 million military radar system
  to the GOT in 2002. Beyond the BAE radar deal, Merlin has
  been linked in the media to a range of other high profile
  government deals including the sale of a Gulfstream
  presidential jet to former President Benjamin Mkapa.
  According to a July 13 report in This Day, a local newspaper,
  at the time of the BAE deal, Vithlani's local partner was
  Tanil Somaiya of Shivacom Tanzania Ltd.
   
 14. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Mi naona viongozi wetu wanalaaana...Ishu kama hii haiitaji mjadala....shame on them.
   
 15. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya mafisi na mabweha yanasubiri pesa irudi! yani hayana muda wa kuzitafuta ila wakichakarika wengine wao wanatoa macho kama manguruwe. Hawa uingereza wangeingiza hizo pesa kwenye taasisi zao za maendeleo ka ilivyo USAID- Danida Nk. kuliko kuwarudishia haya majambazi. Kwani zilizorudi BOT kwa msaada wa Dr,. Slaa kufichu wakasingizia zinapelekwa Rukwa kwa ajili ya kilimo kwanza si wamezitafuna. Tunaongozwa na mafisi. shiit.
   
 16. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hatua gani zaidi ichukuliwe kwenye nchi ya walaji?
   
 17. n

  ngoko JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa mwendo huu jamaa wanajipongeza na kujiona wajanja, pesa uweke mfukoni, halafu wazungu wanakulipa tena kama zawadi ya matendo yako machafu!!!, hizi dili chafu hazitaisha inji hii.
   
 18. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #18
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Good idea! Lakini serikali ikubali waingereza wenyewe ndio watekeleze na kuisimamia miradi hiyo nchini mwetu kwa kutumia wananchi wetu wanaowaamini. Nisiulizwe kuhusu sovereignty au kama nao (waingereza) hawatakula. Hadi hapo tumeshapoteza uhuru wa kusimamia maslahi yetu na hata kama wakijimegea kiasi sio tatizo; kwani sie tulidai tumeibiwa? Kuna chochote tulichotegemea zaidi ya kuwatetemekea na kuwaenzi wezi wetu?
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Dec 23, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280


  Bila shaka kuwa kiongozi serikalini inabidi usiwe na soni wala haya!
   
 20. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nimechoka na hili linchi! tuandamane!!
   
Loading...