Kwa maoni yangu, rais wa chama cha waalimu ndg. Gratias Mkoba na kaimu katibu mkuu mwl. Oluoch wanapaswa kujihuzuru kwa kuandaa mgomo ambao kwa tafsiri yangu ulikuwa ni kiini macho, hawakuwa na dhamira ya dhati ya kuwataka waalimu wagome kwa kuishinikiza serikali kuwapa waalimu madai yao. Nina sababu zifuatazo kwa kusema haya: 1. kama viongozi waandaji wa mgomo, sikutegemea kukiukwa kwa masharti ya mgomo na hivyo kuufanya mgomo ni halari kisheria. Kitendo cha kutoa masaa 48 siku ambazo si za kazi, upigaji kura bila kuwepo afisa wa kazi, na makosa mengine yaliyoufanya mgomo uwe batili binafsi siamini kama hawakujuwa sheria ila walifanya makusudi kwa sababu zao binafsi. Naamini kabisa wanasheria wapo, wangeweza kuwatumia kwa ishu seriou kama hii kama wao ni wajinga wa sheria. Wametuzalilisha waalimu kwa kutafsiriwa kuwa mambo yetu ni ya ovyo ovyo. 2. kuwadanganya na kuwaaminisha waalim, ambao ni wanachama wao kuwa mgomo ni halari, umefuata misingi na taratibu zote za kisheri, na kwamba wasiwe na wasi wasi, kila wakati walipohojiwa katika vyombo vya habari unaonyesha kuwa viongozi hawa ni waongo na si watendaji. Waalimu watashindwa tena kuitikia matamko yao ya migomo kwa kuwa hawatakuwa na uhakika na maneno yao. wakiendelea kutuongoza kamwe mgomo wowote utakaotangazwa hautafanikiwa. 3. Uongozi wa juu wa CWT chini ya mr. Mkoba haukufanya maandalizi ya mgomo ipasavyo kwa kuwashirikisha wanachama wake wote ambao ndio wagomaji. Hakuna elimu ya uamusho iliyotolewa kwa wanachama na ndiyo maana mwitikio wa mgomo haujaweza kutikisa sana. Najuwa wadau wa elimu, hasa waalimu wenzangu mnasababu nyingine nyingi za kumfanya huyu mtu ajihuzuru. Naomba tuziweke zitusaidie kumtoa huu jamaa, hana lolote juu ya maslahi ya waalimu.