Tamko la chama cha madaktari Tanzania (MAT)

stun

Member
Nov 20, 2010
63
43
[h=6]Tamko la Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT)

Kikao cha mkutano mkuu wa dharura wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) kilichofanyika leo siku ya jumamosi, tarehe 14/01/2012 ukumbi wa JAFFARY COMPLEX kimejadili kwa kina yafuatayo:

1. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimejadili na kuazimia kutoa masaa 72 kwa serikali kuwa “Intern doctors” wote waliohamishwa warudishwe Muhimbili mara moja wakamalizie muda wao. Na kwamba ifahamike kuwa interns huomba kwenda kufanya internship katika hospitali Fulani kutegemeana na malengo ya baadaye waliojiwekea. Na pili kuna baadhi ya vifaa vipo mf. Muhimbili na huko kwingine haviko. Madaktari wemesikitishwa sana na uamuzi huu kwa vile haieleweki ni kwa nini “intern doctors” waadhibiwe wakati walidai walipwe mishahara yao tu na serikali ilikiri kosa hilo. Wanachama wangependa kuona waliofanya uzembe huo wanawajibishwa mara moja na sio kuachwa waendelee kuwaadhibu madaktari wasio na kosa.

2. Kwamba, kwa kuwa Intern doctors wamekuwa wakifanya kazi bila malipo kwa muda mrefu na hali hiyo ikapelekea kusitisha kazi ndipo serikali ikaamua kuwalipa mishahara yao. Kufuatia kuendelea kusababisha adha kwa madaktari na wataalamu wengine wa afya na hatimaye kusababisha huduma mbovu kwa wagonjwa, Chama cha madaktari kimeona kimshauri Mh. Rais atafute ajira nyingine kwa ajili ya maafisa waandamizi wafuatao:
a. Katibu Mkuu, wizara ya Afya , Ms. Blandina Nyoni b. Mganga Mkuu wa serikali, Dr. Deo Mtasiwa
3. Kwamba waziri wa afya Dr. Hadji Mponda (MB) afute kauli yake inayoashiria kwamba “intern doctors” ni wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa 5. Ieleweke kwamba ni madaktari kamili, waliohitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari. Na chama cha madaktari kimesikitishwa sana na upotoshwaji huuu wa mara kwa mara. Kutokana na hayo hapo juu basi chama cha madaktari Tanzania kina msamehe kwani inaonekana hajui atendalo. Ijulikane kwamba mjadala wa hivi ulishawahi kuibushwa mwaka
2005 na waziri wa afya kipindi hicho alikiri bayana kwamba intern ni daktari kamili aliyefuzu.

4. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimeamua kumsimamisha uanachama wa chama hiki Dkt. Deo Mtasiwa, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali (CMO), kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa kushindwa kumshauri waziri wa afya vizuri kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania. Mkutano huu unamsimamisha rasmi Uanachama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taratibu za kumrejesha zitajadiliwa kwenye Mkutano mkuu wa kawaida wa chama. Hii itakuwa fundisho kwa madaktari wengine wote nchini.

5. Kwamba chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimeazimia kuitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote siku ya jumatano tarehe
18/01/2012, kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea kwenye ukumbi
utakaotangazwa. Agenda za mkutano huo, pamoja na mambo mengine, zitakuwa zifuatazo:
i. Hatma ya heshima ya fani ya udaktari na mustakabali wa huduma za afya kwa watanzania
ii. Kwa nini serikali haijaanza kulipa posho ya kazi muda wa ziada (on call allowance) kama ilivyopitishwa mwaka 1990 na kufanyiwa maboresho mwaka 2008.
iii. Mshahara mpya wa daktari unaoendana na elimu, ujuzi, umuhimu, hadhi, majukumu, na hali ya uchumi wa sasa na mfumuko wa bei.
iv. Maslahi mengine ya madaktari kama nyumba, posho ya mazingira magumu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi( Risk allowance).
v. Kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61
vi. Mengineyo

RAIS – CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT)

[/h]
 
Jamani Madaktari hakuna atakaye wakomboa ni nyinyi wenyewe wenzenu wanacheza na makaratasi wizarani wanakula hela ya nguvu nyinyi mnahangaika na wagonjwa mnaambulia magonjwa ya migongo na maTB
 
Hakuna kiongozi kilaza kama Deo Mtasiwa yaani anaboa sana aliwekwa na Luhanjo sasa ametoka na yeye aende!!hana uwezo kabisa hata maamuzi yake hovyo siku zote!
 
Kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61

wenyewe kumbe tunao wachache hivi halafu tunawazingua zingua ..wakiondoka na kwenda botswana huko mtamlaumu nani?
oooh gosh kumbe nyie mnakimbilia India ndio maaa hajalia wala nini
 
Kama hakuna unafiki ndani yake na hizo agenda mkasijadili kwa upana wake pamoja na maamuzi mliyofikia kwenye mkutano wenu basi mtakuwa mmeamuka na tayari mtaanza safari ya kusaidia ukombozi wa nchi hii chini ya mkoloni mweusi CCM.haiwezekani mkawa mnadharauliwa kana kwamba mmekariri Sungura akasema,haiwezekani mkaaishi kwa kujipendekeza huku mnaumizwa na wanasiasa uchwara,nawapongeza kama hamtatilia unafiki na fitina,umoja wenu na tafakuri za kina ni ukombozi wenu na kwa taifa zima,lakini pia ni kurudisha heshima ya taaluma yenu.
 
Naunga mkono hoja mara laki moja na mia moja

safi sana primus, namala, rodrick na timu nzima ya weledi
 
kumepambazuka madaktari....nawapongeza sana tena sana. Hata Idd Amin pamoja na uovu wake aliwaheshimu madaktari.
Unganeni pamoja, nia,sababu na uwezo wa kuleta mabadiliko mnao....TANA mpo?
 
Back
Top Bottom