Tamko la CHADEMA kuhusu uteuzi wa Biswalo Mganga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu

Safari hii sidhani kama bwana Biswalo atachomoka..uzuri Mama yupo slow but sure..waongezwe ,Dotto James,Bashite,et al..
 
Hiki chama kina maono ya mbali sana. Baada ya miaka miwili ndipo Mh. Rais ana ona yale yaliyosemwa na Chadema.
 
Itakumbukwa kwamba tarehe 11.05.2021 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu alitangaza uteuzi wa nafasi za Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanywa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na unyeti wa nafasi hizo katika kusimamia haki nchini tumeona ni muhimu kusema baadhi ya mambo ambayo tunaamini yalipaswa kufanyiwa kazi zaidi ili kuweza kupata Majaji wenye sifa zisizotiliwa shaka na umma.

Uteuzi wa Biswalo Mganga ambaye alikuwa DPP na ukizingatia aliyoyafanya na kusababisha kuongeza mahabusu katika Magereza kwa kuongeza wigo wa makosa yasiyokuwa na dhamana, hali iliyopelekea Raid Magufuli kuanza ziara ya kutembelea magereza na kuagiza utafutwe utaratibu wa kuondoa msongamano katika magereza nchini.

Kuna uwezekano wa yeye kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa sababu mashauri yanaweza kwenda mbele yake kwa rufaa au kuanza kusikilizwa wakati yeye alishiriki moja kwa moja katika kuyaandaa.

Aidha , kuna tuhuma dhidi ya aliyekuwa DPP Biswalo Mganga katika kufuatilia na kushughulikia mchakato wa kampuni ya MR.KUKU FARMERS LIMITED iliyokuwa imesajiliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela)na kupewa cheti cha usajili Namba 141097253 tarehe 21 February, 2020.

Kampuni tajwa hapo juu ilikuwa inatambuliwa na Mamlaka zote za kodi nchini na ilikuwa na TIN namba pamoja na cheti cha kulipia kodi ya ongezeko la thamani (VAT), na ilipewa cheti cha kuthibitisha kuwa walilipa Kodi (tax clearance) kilichotolewa na TRA.

Kampuni hii ilichukua fedha za wananchi kwa njia ya kuwapatia hisa ili wawe sehemu ya wamiliki wa Kampuni.

Jeshi la Polisi lilimkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na kumfungulia mashtaka ya kuendesha biashara kinyume na sheria na hivyo akafunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Shtaka hilo liliendeshwa kwa utaratibu wa plea bargain uliosimamiwa na DPP , na hatimaye fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Kampuni zaidi ya shilingi Bilioni 10 Zilichukuliwa na DPP, na kuwaacha waliokuwa wamenunua hisa bila kujua wafanye nini .Jambo hili linahitaji kuchunguzwa ili kuona kama Biswalo alitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Aidha , DPP Biswalo anatuhumiwa kuwa alikuwa akiwataka wale wote waliokuwa wamekubalina kwa utaratibu wa plea bargaining kumlipa yeye fedha kinyume na kanuni kifungu cha 21 ambacho kinawataka watuhumiwa kumlipa msajili wa hazina ambaye atapokea malipo hayo kwa niaba ya serikali.

Vilevile, aliyekuwa DPP Biswalo anatuhumiwa kuendesha kesi mbalimbali za viongozi wa Chadema kisiasa badala ya kufuata misingi ya sheria. Ana tuhuma za kuzuia Mahakama kutoa dhamana kwa kesi za viongozi wa Chadema kwa misukumo ya kisiasa kama alivyofanya kwenye kesi ya Mhe. Godbless Lema, Mhe.Freeman Mbowe na wengine wengi.

Mapendekezo

1. Tunapendekeza kuundwa Baraza la nidhamu dhidi yake hasa kwenye masuala ya makubaliano ya kukiri kosa (plea bargaining) ambayo yana malalamiko mengi ya wananchi na kubambikia watu kesi mbalimbali wamchunguze mwenendo wake alipokuwa DPP na kama bado anazo sifa za kuteuliwa kuwa Jaji.

2. Tunapendekeza uanzishwe utaratibu wa wazi wa kuwapata Majaji kama vile kuwashindanisha kwa vigezo ikiwa ni pamoja na kufanya usaili wa wazi na sio kuteua watu moja kwa moja. Mfano mzuri ni namna ya upatikanaji Majaji nchini Kenya na nchi nyingine.

3. Tunashauri kusitishwa kwa mchakato wa kumuapisha kuwa Jaji aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga hadi hapo malalamiko dhidi yake yatakapokamilika kuchunguzwa na yatakapoamuliwa na Baraza la Nidhamu (Tribunal) litakaloundwa ili kuchunguza malalamiko na tuhuma dhidi yake.

4. Kwa kuwa Katiba iliyopo Ibara ya 112 (1) wajumbe wa tume ya kuajiri ya mahakama, mawakili hawana uwakilishi.
Kwa hiyo tume ya sasa inatekeleza majukumu yake bila uwakilishi wa mawakili wa kujitegemea, uwakilishi wa kijinsia na sifa zinazoainishwa katika Katiba. Hivyo tunapendekeza uwekwe utaratibu wa kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na uwakilishi sawia.

5. Tunapendekeza kuwa uwekwe utarataibu wazi wa kuwapata Majaji ikiwa ni pamoja na kuweka wazi uwepo wa nafasi za Ujaji kwa kutangaza ili watu wenye sifa waombe, washindanishwe kwa vigezo na masharti mbalimbali hii ingesaidia kupata Majaji wenye uwezo usiotiliwa shaka, Majaji huru na wasiopendelewa au wasiozua minong’ono ya kubebwa au wenye nasaba za kisiasa.

6.Katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mahakama ,Bunge linajukumu la kutunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa majukumu ya Tume.

Imetolewa Leo Jumapili Mei 16, 2021

John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.View attachment 1787263

View attachment 1787264
Hii inadhihirisha ufinyu wa uelewa miongoni mwa wasaliti wetu. Majaji wote wana security of tenure, huwezi kumtoa hivi hivi. CHADEMA wanamchukia Biswalo kwa vile aliwafunga walipoinyea mavi na kuikojolea Tanzania kwa kuimba wimbo wa Taifa eti Mungu Ibariki CHADEMA, nchi kama Saudia au Pakistan wangepigwa risasi hazarani.
Halafu ni DPP pekee ambaye kesi zake zote dhidi ya CHADEMA, moja tu iliyopita ni ya Mbunge Lema wa Arusha aliposhinda Mahakama ya Rufaa. Jaji ni Jaji huwezi kumtoa just like that. Hivi inakuingia akilini eti pleabargaining hela aweke mfukoni mwake. My friend, wanaofanya pleabargaining ni majambazi sugu, drugpushers, moneylaunderers, killers and murderers, terrorists, ambao ushahidi pekee ni maiti, utakubalije uchukue hela zote hizo? Zitakaa wapi? Chuki ya Jaji Biswalo inawatafuna.
 
Back
Top Bottom