GE2025 Tamko la BAVICHA kuunga mkono maandamano ya Amani Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Tamko rasmi la Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA) kuunga mkono maandamano ya vijana wa Gen Z, kesho Oktoba 29,2025.

==

Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) limeundwa kwa mujibu wa ibara ya 7.8.2 (a) ya katiba ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya mwaka 2006 toleo la 2019 likiwa na lengo kuu la kuhakikisha vijana wanatoa mchango thabiti katika kukuza na kuendeleza madhumuni ya Chama kwa maslai na ustawi wa Taifa la Tanzania kwa mujibu wa mwongozo wa BAVICHA Na.3.1 toleo la 2019.

Tunafahamu msimamo wa Chama chetu wa kuhusu uchaguzi mkuu 2025 ulikuwa ni NO REFORMS NO ELECTION. Pia, tunafahamu vijana na umma wa Watanzania wapenda haki na mabadiliko ndani ya Taifa letu kuwa wametangaza kuwepo kwa maandamano tarehe 29.10.2025 kudai haki za msingi ikiwemo uchaguzi HURU na HAKI na wenye KUAMINIKA, sambamba na kupinga ufujaji wa rasilimali za Taifa.

BAVICHA katika kuunga mkono msimamo wa Chama chetu na kuunga Taifa mkono vuguvugu la vijana wa kizazi kipya (Gen Z) wanaokabiliwa na changamoto za ukosefu mkubwa wa ajira, kuuwawa, kutekwa na kupotezwa. Hatuna budi kuwaunga mkono vijana wenzetu walioamua kupaza sauti kwa njia ya maandamano ya amani Oktoba 29.2025.

Siku zote vijana wa CHADEMA tunapaswa kuongozwa kwa na maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa, Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga akina ndio bwana mkubwa, vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyosha-bihiana na matakwa na matajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa.

Kwa uzito wa maneno haya ya Mwalimu ambayo vijana tumejiapiza kuyaishi, na kwa kuwa watawala wamepuuza maoni ya wananchi. Natoa WITO kwa vijana wa CHADEMA nchi nzima kuwa sehemu ya historia hii muhimu kwa Taifa letu kwa sababu lugha ya MAANDAMANO ndiyo ludha pekee ambayo watawala wanaweza kuielewa kwa sasa.

Maono ya Mwalimu yakawe ni taa na DIRA katika kulinda miiko na tunu za Taifa letu zenye lengo la kulinda UTU, UHANI na DEMOKRASIA YA KWELI nchini.

Tunawatakia vijana wote kila la kheri katika mapambano ya kudai haki, uhuru na maendeleo ya watu ndani ya Taifa letu.

VIJANA NI NGUVU YA MABADILIKO.
MUNGU IBARIKI CHADEMA. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Imetolewa Na;

BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA - TAIFA)


 
Mwanzo wa maandamano yasiyo koma hadi hawa waliojilazimisha kuwepo madaraka wakimbie kama rais Andry Rajoelina wa nchi jirani ya Madagascar



Andry Nirina Rajoelina (born 30 May 1974) is a Malagasy-born French politician and businessman who served as the eighth president of Madagascar before relinquished power after huge resilient pressure from GenZ,
 
TOKA MAKTABA :

VIEWS inayotafsiriwa kama idadi ya waandamanaji mtandaoni katika post moja hapo chini :

361,189 Views

View: https://m.youtube.com/watch?v=H1nHdmCnduI

Ukizisha views zote mitandao X Twitter, YouTube, Facebook account zote, mazungumzo vijiweni, mijini na vijijini ni zaidi ya waandamanaji 5,000, 000 wanaunga mkono maadamano
 
Watanzania kwa umoja wetu kesho tutoke kwa wingi tukapige kura, kura kwa maendeleo ya taifa letu
 
Toka maktaba :

Mahojiano na Prof. P.A.N Mihanjo kuhusu hali ya kisiasa nchini.

Prof. Eginald P.A.N. Mihanjo. PhD, MA in History, BA (Hon.) Educ. (UDSM) amewahi kuwa Kaimu Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu, Mhadhiri mwandamizi ndani na nje ya nchi, Mkurugenzi wa mafunzo wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa NDC kinachotoa mafunzo ya usalama -stratejia- ulinzi, mhadhiri Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Msumbiji Foreign Relation Kurasini.. pia ni mtaalamu wa Usalama, Ulinzi, Usuluhishi wa Migogoro kimataifa na kikanda ..

 
Mheshimiwa Balozi Dr. Msuya Waldi Mangachi amezungumzia nguvu ya umma hutumika, nguvu ya umma haina makosa pale inapochukua maamuzi ya kutaka hatima yao kwa nguvu ya umma

TANZANIA 2025 GENERAL ELECTIONS

Ambassador Dr. Msuya W. Mangachi - On Masses Overthrowing the King .. genesis of democracy ... fair elections ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=0iKkCMHUlaoGuests :

H.E Dr. Msuya Waldi Mangachi, former High Commissioner of the United Republic of Tanzania in Abuja, Nigeria who is also accredited to Benin, Togo, Cote D'ivoire, ..

Dr. Bravious Kayoza Doctor of Philosophy - PhD Political Economy..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…