TAMISEMI toeni vibali Halmashauri ziajiri walimu na manesi

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
Huu ni ushauri wa bure.

TAMISEMI shughulikieni matatizo ya msingi sio kujipa makazi mengi msiyoweza kuyamaliza.

Toeni vibali Halmashauri ziajiri waalimu na watumishi wa afya kisha taarifa zao zitumwe huko kwenu/DODOMA.

Halmashauri zina wasomi wa kila aina hivi kweli hawawezi kuajiri waalimu wa Primary na Secondary.

DC, DED, DSO, HR, MAAFISA ELIMU, CWT N.K MNAWEZA KUUNDA PANEL MKAFANYA HILO ZOEZI KWA MAFANIKIO KABISA.
 
TCU ilikuwa na utaratibu huu wa wao kuchagua na kupangia wanafunzi vyuo, ila baadae wakaamua vyuo ndiyo vihusike kuchagua na kutuma majina TCU.

Wazo lako ni nzuri, ila labda wanaona ajira siyo nyingi zinazotolewa ndiyo maana kwao wanachukulia kazi ndogo na kitu cha kawaida.
 
Na kwa namna hiyo wakivuruga zoezi wakuwajibishwa watakuwa wanajulikana,ila tu wapewe vibali kwa maana ya idadi kulingana na mahitaji na uwezo wa bajeti ya halmashauri husika.
 
Na kwa nanna hiyo wakivuruga zoezi wakuwajibiwa watakuwa wanajulikana,ila tuwapewe vibali kwa maana ya idadi kulingana na mahitaji na uwezo wa bajeti ya halmashauri husika.
Ndio mkuu yaani zoezi lingekuwa rahis sana.
 
TCU ilikuwa na utaratibu huu wa wao kuchagua na kupangia wanafunzi vyuo, ila baadae wakaamua vyuo ndiyo vihusike kuchagua na kutuma majina TCU.

Wazo lako ni nzuri, ila labda wanaona ajira siyo nyingi zinazotolewa ndiyo maana kwao wanachukulia kazi ndogo na kitu cha kawaida.
Kweli mkuu. Unakuta wilaya inahitaji mwalimu wa hesabu TAMISEMI wanawaletea mwalimu wa Kiswahili.
 
Zamani ilikuwa hivyo lakini ajira zilijaa rushwa, undugu na kujuana ndio maana mfumo wa kuajiri ukabadilishwa na sishauri turudi huko tena
Kwani TAMISEMI hakuna rushwa na kujuana?
 
Kweli mkuu. Unakuta wilaya inahitaji mwalimu wa hesabu TAMISEMI wanawaletea mwalimu wa Kiswahili.
Yes, upo sawa mkuu. Itasaidia kukidhi mahitaji kuliko kuajiri tu in general bila kujali wapi kuna upungufu gani kwa wakati huo.

Wana assume walimu wa sayansi wachache wanapewa kipao mbele kumbe kuna shule waalimu wa sanaa ni shida. Shule kupata mwalimu wa literature tu mtihani.
 
Back
Top Bottom