DOKEZO TAMISEMI na upendeleo uhamisho wa walimu Karagwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bay of pigs

Senior Member
Jan 5, 2014
158
196
Naam! Nadhani inajulikana kuwa Innocent Bashungwa ni Waziri wa TAMISEMI.

TAMISEMI iliweka utaratibu wa uhamisho wa watumishi wa umma, mfano walimu wanapotaka kuhama vituo vyao vya kazi, sharti wapate walimu wenzao wa kubadilishana nao.

Sasa ni hivi, inakuwaje mmeruhusu watumishi hasa walimu ambao ni Wanyambo wa Karagwe anakotoka Waziri Bashungwa kurudi karagwe bila kufuata utaratibu wa kubadilishana?

Awamu ya kwanza ya walimu waliorudishwa karagwe ilipita na walimu wengi toka sehemu mbalimbali za Tanzania waliripoti katika shule mbalimbali za karagwe na jana 21/09/2022 awamu ya pili ilitangazwa tena kwa walimu wanaohitaji kurudi Karagwe.

Je, kwanini kunakuwa na double standards kwa suala hili la uhamisho?
 
Walimu wanae maswahiba. Sijui kwann serikali haiweki posho ya mazingira magumu
Kuna maeneo walimu wanahama haswa
 
Ukabila utawaua nyie wanyambo ndio watu gani yaani wote ni wahaya lakini bado mnatengana, sijui mkoje.
 
Back
Top Bottom