TAMISEMI leo ndo tarehe 25 timizeni wajibu wenu

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Kutokana na taarifa iliyotolewa na Waziri wa Utumishi siku ya tarehe 02/02/2017 kuwa ajira kwa Walimu wa Sayansi na Mafundi sanifu wa maabara zitakuwa tayari ifikapo March.
Ilifahamika kuwa huenda zingetolewa mwishoni mwa mwezi uliopita lakini haikuwa hivyo. Sasa March yenyewe ndo hii inaishia. Tunaomba ahadi itekelezwe au maelezo ya kuwa ajira hakuna yatolewe. Hatutaki tena habari za kuwa itakuwa muda fulani, maana mlianza na sentensi za baada ya bajeti kupitishwa, hivi karibuni, hivi punde, muda wowote kuanzia sasa hadi mkataja mwezi kabisa, sasa mwezi wenyewe ndo huu.
Tuthibitishieni imani yetu juu serikali hii au tuondoleeni kabisa imani juu ya serikali hii.
Tangazeni tu hata mkifanywa kama Nape watanzania watakuchukulieni kuwa ninyi ni mashujaa wa nchi hii.
All the best. Sitegemei ifike saa kumi na moja jioni mkiwa bado kimya, maana hamkosi sababu mara oooh tulishindwa kutangaza kutokana na sababu za kimtandao.
 
Tareh 31 mwisho wa maombi harafu tunakaa kimya hadi tarehe 12 tunawaambia wa shule ya msingi walio faulu hesabu watume vyeti tunawapa wiki 3 ya siku 21 hadi May 2 au 3 tunatoa tena nafasi kwa walimu wa arts kama nafasi 500 tunawapa wiki 3 hadi june 2 au 3 tunakaa kimya hadi june 12 tunawaomba tena walimu wa sayansi walio staafu watume vyeti tunawapa wiki mbili hadi june 25 hapo tunangojea harafu tunatoa majibu ku report july 5
 
Hapo ndio umetibua. Mwajiri wenu (rais) hataki mmpangie lini atoe ajira, kwa kifupi mmejila subirini july mtafikiriwa
 
Tareh 31 mwisho wa maombi harafu tunakaa kimya hadi tarehe 12 tunawaambia wa shule ya msingi walio faulu hesabu watume vyeti tunawapa wiki 3 ya siku 21 hadi May 2 au 3 tunatoa tena nafasi kwa walimu wa arts kama nafasi 500 tunawapa wiki 3 hadi june 2 au 3 tunakaa kimya hadi june 12 tunawaomba tena walimu wa sayansi walio staafu watume vyeti tunawapa wiki mbili hadi june 25 hapo tunangojea harafu tunatoa majibu ku report july 5
Kama ulikuwepo kwenye mipango yao! Hii ndo dhana halisi.
 
Back
Top Bottom