Tambwe hiza ndani ya radio one live | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tambwe hiza ndani ya radio one live

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by segwanga, Apr 23, 2012.

 1. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Anaongelea mambo ya matusi na kupakana matope kwenye kampeni,msikilizeni ana hoja za msingi
   
 2. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu amemaliza vyama vya upinzani, amefilisika na ameishia ccm!
   
 3. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Namsikia hapa anasema awali Richmond walikuwa the "lowest bidder". Sina hakika kama anajua tofauti ya hilo neno na the "lowest evaluated bidder"
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Tambwe:
  Badala ya kuleta megawati 220 alileta 100. (eti anaona hapa haoni ufisadi)
  mbona anachanganya mada?
  hana hoja huyu mpuuzi
   
 5. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Antony Komu- CDM
  • Anamshangaa Tambwe hasa akimkumbuka alikotoka
  • Anajua watanzania wanakumbuka aliyosema huko nyuma
  • Udhaifu wa CCM lazima uzungumzwe ili kuwe na justification
  • CDM ni chama cha mlengo wa kati
  • Vyama vya upinzani vina sera tofauti kabisa na CCM (Sera ya majimbo) sababu zipo
   
 6. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kiherehere kilimfanya afe kifo cha kisiasa huyo. Hata wengine tulishamsahau kwenye midani ya siasa za tz. Simtofautishi na mtu mmoja aliyegombea ubunge miaka fulani aliyekuwa anaitwa KIHIYO.
   
 7. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Anasema vyama vya upinzani havina sera,kila siku ni mambo yale yale ya kuongelea richmond.Na anasema richmond haikuwa ni tatizo kwa sababu serikali ilichukua kampuni ambayo ilikuwa na alternative nzuri ya kutengeneza umeme wa bei rahsi yaani sh 9 badala ya sh 40 kwa kampuni nyingine.Kwa hiyo yeye haoni ufisadi kwenye suala la richmondi
   
 8. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mwanagu anasema bora tuangalie kipindi cha watoto ITV kuliko kusikiliza hiki kipindi.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,440
  Likes Received: 19,798
  Trophy Points: 280
  yuko chama gani kwani?
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Anthony Temu:
  Tambwe alikuwepo NCCR, akaenda CUF, na leo yupo CCM. kitendo cha kusema chadema hawana sera namshangaa sana.
  Ili kuwe na justification lazima tutumie udhaifu wa ccm.
  CHADEMA ni chama chenye mrengo wa kati.
  CHADEMA tuna sera tofauti na ccm
  Ili nchi hii iweze kufikia malengo sisi tunasema tuwe na sera za majimbo
  Kwa mfano kule Arumeru tulizungumzia sera ya maji, ccm wameshindwa, lakini sisi tumechukua jimbo leo hii kuna watu wanatumia maji, tumechimba visima kule watu wanatumia maji
  Tumezungumzia sera ya Ardhi Arumeru, ndiyo maana tumepewa kura na wananchi
  Ili kukabiliana na mazingira haya, watu wanatakiwa waandaliwe kielimu ili waweze kushindana katika ulimwengu wa utandawazi
   
 11. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  ANTHONY KOMU:
  Nashindwa kumwelewa Tambwe sijui anataka CHADEMA wawe na sera za namna gani
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,455
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Sikiliza na fuata ushauri wa mwanao katika hili. Mgongee thanks hapo on mebehalf
   
 13. C

  CHAMULILE Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hapo kuna shida kubwa
   
 14. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  Aongelee ya mawaziri wanaotakiwa kung'oka leo na aachane na mavi ya kale. Au ndio kusema pale alikolalia ndio kaamkia leo. Nape alimpaki huyu kutokana na kila issue sisiem kuipropagate. Leo hii wamemkumbuka kwenye kabati alilofungiwa? Ama kweli gamba limebanwa mbavu. Wanaonaje kama wakimpa cheo cha Millya?
  .
   
 15. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  keshapoteza mvuto kisiasa huyo...
   
 16. j

  jembe la kigoma Senior Member

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tambwe hiza kwangu me namchukulia kama limbukeni wa siasa asiye na namna nyingne ya kupata kipato isipokuwa kuburuza mtumbo wake kwa magamba ili apate kuishi,that y nimeandika jina lake kwa herufi ndogo kuweka mcctizo kuwa ni mtu mdogo sana kma ccmizi kwenye siasa za bongo na makamanda wa CDM,Atajisalimisha tu.
   
 17. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Ni kweli watu wengi na hata wasomi hawaelewi tofauti kati ya term hizo mbili kwenye mchakato wa ununuzi kwa njia ya zabuni.
   
 18. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Kwanza bosi gani kawalika Radio one,atakuwa ni kilaza kama tambwe mwenyewe.whom'z tambwe nowdayz,kafa kisiasa.
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  (b) Njia kuu za uchumi ni chini ya wakulima na wafanya
  kazi:

  Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha ujamaa ni
  kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
  zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi

  wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
  vyao vya Ushirika. Pia ni lazima kuthibitisha kuwa Chama
  kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.


  Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
  maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
  usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
  biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
  simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
  ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
  kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
  mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
  katika viwanda vikubwa. SEHEMU YA PILI

  SIASA YA UJAMAA

  (a) Hakuna Unyonyaji:

  Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina
  ubepari wala ukabaila
  . Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya
  chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
  watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
  kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
  hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
  aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
  hayapitani mno.

  Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
  kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
  ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
  kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
  kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.

  Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
  chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
  vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
  ikapanuka na kuenea.


  Haya ni mambo ya CCM?


  [FONT=&amp]Falsafa ya Chama[/FONT]

  1. [FONT=&amp]Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao. [/FONT]
  2. [FONT=&amp]Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni. [/FONT]
  3. [FONT=&amp]Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.[/FONT]
  4. [FONT=&amp]Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.[/FONT]
  5. [FONT=&amp]CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.[/FONT]
  6. [FONT=&amp]CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.[/FONT]
  7. [FONT=&amp]Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki. [/FONT]
  [FONT=&amp]Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

  Haya ni ya CDM

  Yapi yanatekelezeka? Nani asiye na sera?
  [/FONT]
   
 20. D

  Darwin JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tambwe Hiza msambaa hana adabu yule, samahani wasambaa kwani naongelea baadhi ya wasambaa wanaorubuniwa na chama tawala wakasahau maslahi ya wasambaa wenzao.
  Tukimuuliza huyo Tambwe pale kwao Mazinde CCM imefanya nini toka miaka hiooooo na mpaka leo hii hata maji bomba yenye uhakika hawana wakati Mazinde iko bondeni na maji yote kutoka milima ya Usambara yanapitia Mazinde.
  Mvua zikinyesha Mazinde hawana maji masafi bali kunywa matope.
  Wakati wa jua wananchi wamekua kama ngamia.

  Msambaa mwingine anaitwa Makamba
  Ukiuliza huko anakotoka amefanya nini hatakupa jibu.
  Kinachoonekana ni binti yake kununua jumba la kifahari kwa pesa za ufisadi.
  Kiukweli msambaa aliyekua na akili nakujali wasambaa alikua Shekilango lakini hawa wasasa ni vibaraka wa mafisadi.

  Samahani kama nimewakwaza baadhi ya wasambaa ambao sio vibaraka wa mafisadi.
   
Loading...