(b) Njia kuu za uchumi ni
chini ya wakulima na wafanya
kazi:
Namna ya pekee ya kujenga na kudumisha
ujamaa ni
kuthibitisha kuwa njia kuu zote za uchumi wa nchi yetu
zinatawaliwa na kumilikiwa na Wakulima na Wafanyakazi
wenyewe kwa kutumia vyombo vya Serikali yao na Vyama
vyao vya Ushirika. Pia ni lazima
kuthibitisha kuwa Chama
kinachotawala ni Chama cha wakulima na wafanyakazi.
Njia kuu za Uchumi ni: kama vile ardhi, misitu, madini,
maji, mafuta na nguvu za umeme; njia za habari, njia za
usafirishaji; mabenki, na bima; biashara na nchi za kigeni na
biashara za jumla; viwanda vya chuma, mashini, silaha, magari,
simenti, mboleo; nguo, na kiwanda cho chote kikubwa
ambacho kinategemewa na sehemu kubwa ya watu katika
kupata riziki zao au kinachotegemewa na viwanda vingine;
mashamba makubwa na hasa yale yanayotoa mazao ya lazima
katika viwanda vikubwa. SEHEMU YA PILI
SIASA YA UJAMAA
(a) Hakuna Unyonyaji:
Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi:
haina
ubepari wala ukabaila. Haina
tabaka mbii za watu: tabaka ya
chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya
watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa
kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi
hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi
aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali
hayapitani mno.
Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi
kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao
ni
watoto wadogo,
wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao,
kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya
kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe.
Nchi yetu ni nchi ya
Wakulima na Wafanya kazi, lakini sin
chi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na
vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza
ikapanuka na kuenea.
Haya ni mambo ya CCM?
- Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
- Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
- Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
- Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
- CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
- CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
- Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.
Haya ni ya CDM
Yapi yanatekelezeka? Nani asiye na sera?