Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,552
- 139,890
Kiongozi katili na korofi wa Liberia akizungushwa mitaani akiwa kakatwa masikio na uume
Maisha haya kuna watu wanajisahau sana,wanajiona kama wao ni wadogo zake Mungu na maisha yatabaki hivihivi siku zote.
Orodha ni ndefu lakini watu hawa ni wale wanaotumika kupokonya haki na maisha ya wengine. Mateso yanayowapata kina Lissu, Ben Saanane na wengine yanauma sana. Ajabu hakuna mwenye time nao.
Angalia watu walivyoumia wakati wa uchaguzi mdogo. Wengine wamekufa. Wenye mamlaka wanasema uchaguzi ulikuwa huru na haki
Nimewataja kwa uchache lakini ni wale wote wanaopokonya haki na maisha ya wengine wasio na hatia.
Nawakumbusha hapo zamani tulikuwa na kina Lowasa, Sumaye, Malechela, Sitta nk
Wako wapi sasa hivi hawana nguvu tena. Kulikuwa na Idi Amini, Mugabe aibu walizopata wote tunazijua
Mnajifanya hamkumbuki kina Rugemalila na Seth Habinder walivyokuwa enzi za JK nani aliamini kama wangepigishwa magoti
Magufuli mwenyewe anaweza kuvuliwa kinga anayoitumia sembuse nyinyi?
Sisi hatuna cha kuwafanya lakini ni suala la mda tu,ipo siku